Sauli Vs Imani Bus lipi bora kwa safari Dar - Mbeya?

Mfano wako hauendani kabisa mkuu, hapo ungefananisha shabaha ya zamani, na chakito ndio waliendana na sauli then Iman hapo ungeifananisha na kina kilimanjaro au Esther
Great thinker tu ndiye anaweza kunielewa, hapo sijafananisha magari.
 
Nimegundua baadhi ya watu wa mikoani ni wapuuzi na washamba bado wanafurahia na kushangilia mwendo kasi badala ya kuangalia usalama wa maisha na afya zao.
Dawa yao ni basi la Majinja, liliwamwaga mavi wakafa zaidi ya 40.

Sifa za kijinga eti basi linalokimbia wakati wanajua barabara zetu sio rafiki. Baadhi ya abiria ni vilaza kweli.
Kuna siku nimemwambia dereva apunguze mwendo abiria wenzangu wakanuna balaa, eti wanataka kuwahi.
 
Kuna Coaster huwa zinatoka Uyole saa 1 jioni zinaingia Dar saa 10 usiku au 11. Huwa zinapaaa. Ni hatari na nusu!
Huwa ninazipanda sana hizo pamoja na zile noah za magazeti. Kuna siku niliteremka Chalinze saa 9 usiku. Hatari sana.
 
Sidhan kama basi siku hizi zinakimbia.. bado kwa Sauli kufika Mbeya saa 12+,. ni mwendo wa kawaida tu .. kipindi cha nyuma akina Upendo Sauti ya Manka au Hood ya Tndm zilikuwa Tisa unusu au kumi kasoro upo Mbeya.. so Sauli bado hakimbiii kivile lbda kwa wasafiri wa siku hizi ndo mnaona zinakimbia
 
Nimeona na Super Feo kaleta scania mbili sijui michina kaona miyeyusho
Michina haina maisha marefu mkuu, Ukiiweka barabarani ipige routes kila siku ndani ya miaka 2-3 lazima ianze breakdowns za hatari usipokua makini lazima uiweke juu ya mawe au kuna baadhi wanazipelekaga routes za vijijini huko zikapambane na rough roads kibishi while Scania unaweza usilipige spana hata miaka 10 labda services ndogo ndogo tu za kawaida. Sema michina kwenye ulaji wa mafuta tu ndiyo ziko vizuri.

Siku hizi wamiliki wa mabasi washakua wajanja mkuu mfano Princes Muro na Dar Luxury ana karakana n.k, Wananunua hizi michina sijui Zhongtong, Yutong, KingLong, AsiaStar & Higer then wanazivua chesisi na injini kisha wanavika chesisi kitu cha mswedeni (Scania) afu kitu kinakaa barabarani si unajua kwenye bodi mchina gari zake anazipamba zina muonekano mzuri ila chesis zake waga nzito ya Scania nyepesi kiasi na imara haina mambo mengi.
 
Acha ujinga ww, Route ya kutoka Mwanza to Dar ni zaidi ya Kilometre 1150 unataka mtu apande gari inayoenda mwendo wa kobe? Au unataka mtu atumie masaa 24? Acha mzee safari ni ndefu mno unadhani kukaa kwenye siti ya basi masaa zaidi 10 ni kazi ndogo. Sijui tu kwanini hatuna usafiri wa usiku wa coster kama kule Mbeya.

Haya Mbeya ni mkoa wenye harakati nyingi sana na pia una mwingiliano mkubwa na wafanyabiashara wengi hata kutoka nchi za kusini magharibi mwa nchi yetu, Na ndiyo mkoa pekee wenye routes nyingi za kwenda Dar kutoka wilaya zake kila moja na mabasi yake, Kyela wana mabasi yao, Mbeya mjini wana basi zao, Tunduma wana basi zao (Before hii ilkua upande wa Mbeya kabla haijawa Songwe)! Hapo napo kuna Kilometre zaidi ya 900 na barabara iko busy muda wote kupitisha magari na foleni za kutosha. Leo hii upande gari inayoenda slow kama trip town si mtakaa barabarani masaa 24!

Mbeya ndio mkoa pekee wenye usafiri wa usiku kwenda Dar maarufu unaitwa "Hakuna Kulala" na bei 30,000 yaani unaondoka saa 12 au 1 jioni unafika kesho yake asubuhi utaona ni jinsi gani ni mkoa ulikua busy na wasafiri wengi. Kuna routes ndefu balaa unakaa mpaka mwili unakufa ganzi, Mwanza to Mbeya, Bukoba to Dar, Dar to Swax, Moshi to Mbeya hizi routes zinahitaji basi nzuri imara na zenye speed, michina huwa haidumu sana kwenye hizi routes.
....Mkuu, naomba kukujulisha kuwa hapo kwenye wino mwekundu. Mbeya sio mkoa pekee kama ulivyoandika, bali ni mkoa mmojawapo wenye mabus/coaster yanayosafiri kuanzia jioni, usiku kucha mpaka Dar.
 
....Mkuu, naomba kukujulisha kuwa hapo kwenye wino mwekundu. Mbeya sio mkoa pekee kama ulivyoandika, bali ni mkoa mmojawapo wenye mabus/coaster yanayosafiri kuanzia jioni, usiku kucha mpaka Dar.
Asante kwa masahihisho mkuu.
 
Michina haina maisha marefu mkuu, Ukiiweka barabarani ipige routes kila siku ndani ya miaka 2-3 lazima ianze breakdowns za hatari usipokua makini lazima uiweke juu ya mawe au kuna baadhi wanazipelekaga routes za vijijini huko zikapambane na rough roads kibishi while Scania unaweza usilipige spana hata miaka 10 labda services ndogo ndogo tu za kawaida. Sema michina kwenye ulaji wa mafuta tu ndiyo ziko vizuri.

Siku hizi wamiliki wa mabasi washakua wajanja mkuu mfano Princes Muro na Dar Luxury n.k, Wananunua hizi michina sijui Zhongtong, Yutong, KingLong, AsiaStar & Higer then wanazivua chesisi na injini kisha wanavika chesisi kitu cha mswedeni (Scania) afu kitu kinakaa barabarani si unajua kwenye bodi mchina gari zake anazipamba zina muonekano mzuri ila chesis zake waga nzito ya Scania nyepesi kiasi na imara haina mambo mengi.
Dar lux ni gari zipi hizo kaweka chassis ya scania?
 
Back
Top Bottom