Sauli ni mfano wa wamiliki wa mabasi waliofilisiwa na madereva fake

Asante CCM

JF-Expert Member
Jun 22, 2023
459
1,678
Biashara ya mabasi ya abiria kwa Dunia ya leo si ya kushadadia ma mbio yasiyo na tija bali ni akili yenye wingi wa ubunifu ndaniye kwa mambo yatakayomvutia abiria taraji.

Mfano Sauli ni wazi alifilisiwa na madereva wake kwa kushadadia sifa za kijinga za mwendo kasi hali iliyosababisha mabasi mengi kuharibika na kwayo kutumia gharama kubwa kwenye matengenezo na mwisho kushindwa kujiendesha na wadai wakafilisi vyao.

Mwisho wa siku Sauli imebaki simulizi.

NB: Kisbo ana bahati ya kung'amua mapema kurejea kwenye ustaarabu vinginevyo naye ingeshabaki simulizi.
 
Biashara ya mabasi ya abiria kwa Dunia ya leo si ya kushadadia ma mbio yasiyo na tija bali ni akili yenye wingi wa ubunifu ndaniye kwa mambo yatakayomvutia abiria taraji...

Mtanzania gani utampa investment ya mamilioni akakutafutie pesa kama wanavyoita wao?

Ukweli mchungu hakuna mwenye bus au Lori atatoboa.

Hata latra hilo wanajua.

Wote unaowaona ni just a matter of time.
 
Biashara ya mabasi ya abiria kwa Dunia ya leo si ya kushadadia ma mbio yasiyo na tija bali ni akili yenye wingi wa ubunifu ndaniye kwa mambo yatakayomvutia abiria taraji...
Unaweza kuwa sahihi mkuu, ila tu kwa taarifa yako Marehemu Sauli alikuwa kishaagiza unit 6 za yutong. Sema mipango ya Mungu si ya mwanadamu. Aendelee kupumzika alipojiandalia.
 
Unaweza kuwa sahihi mkuu, ila tu kwa taarifa yako Marehemu Sauli alikuwa kishaagiza unit 6 za yutong. Sema mipango ya Mungu si ya mwanadamu. Aendelee kupumzika alipojiandalia.
Marehemu Sauli akiwa na mawakala wa Yutong nyakati za mwisho za uhai wake
 
Attachments

  • IMG-20240805-WA0003.jpg
    IMG-20240805-WA0003.jpg
    63.1 KB · Views: 8
Kwani wewe unayo mangapi?
Mimi sina maana na kushangaa unavyosema hakuna mtanzania anaweza pata mamillioni kwenye biashara ya usafirishaji wakati hayo magari tu ni ya mamillioni ya pesa au huwa wanayaokota?
 
Kiswahili unaelewa lakini ndugu? Hebu rejea kusoma kama nimeandika au hata kumaanisha unachosena hapa.

Wazi wazi nimesema nunua bus la mamilioni, mpe dereva na konda uone kama watakuletea lolote!
 
Wenye mabasi wajifunze kwa Zuberi, miaka zaidi ya 20 kwenye njia ya Dar -Mwanza, wengi wamekuja kwa mbwembwe nyingi na wamemuacha mpaka leo.

Kwenye Malori kuna kampuni zinapiga pesa, watu wana mikataba mikubwa. Ingekuwa usafirishaji haulipi wasingenunua magari 100+.
 
Biashara ya mabasi ya abiria kwa Dunia ya leo si ya kushadadia ma mbio yasiyo na tija bali ni akili yenye wingi wa ubunifu ndaniye kwa mambo yatakayomvutia abiria taraji...
Hakuna sayansi inayokubaliana na hoja zako. Gari hata ikitembea kwa speed 5km/ hour itachakaa tu.

Kwani walioweka gari ifike 180 km/ hour walimaanisha nini?

ACHENI HOJA ZA KIJINGA. leta sababu zingine
 
Back
Top Bottom