kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 8,990
- 17,879
Saudia yapeleka maski zenye virusi vya corona nchini Yemen
Apr 02, 2020 02:27 UTC
Waziri wa Habari wa Yemen amesema kuna uwezekano mkubwa kwamba ndege za kivita za muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia zimedondosha maski (barakoa) zenye virusi vya corona katika miji mbalimbali ya nchi hiyo maskini ya Kiarabu.
Shirika la habari la Middle East Monitor limemnukuu Dhaifullah al-Shami, Waziri wa Habari wa Yemen akitoa tangazo hilo ambapo pia ameviomba vyombo vya habari kuwatahadharisha wananchi wa Yemen dhidi ya kugusa au kuvaa maski hizo zinazodondoshwa na ndege za kivita za muungano vamizi katika mji mkuu Sana'a na miji mingine.
Ameashiria kuhusu taathira hasi za uvamizi wa kijeshi nchini humo ulioifanya Yemen ikumbwe na mgogoro mkubwa zaidi wa kibinadamu duniani na kueleza bayana kuwa, "tumepigwa na butwaa kuona vikosi vya muungano (vamizi) wa kijeshi vikisambaza maski katika maeneo yote ya mji mkuu Sana'a na mikoa kadhaa ya nchi hii."
Waziri wa Habari wa Yemen amesema kuwa, nchi hiyo haijarekodi kesi yoyote ya ugonjwa wa Covid-19 ambao umeshaua makumi ya maelfu ya watu katika nchi mbalimbali duniani na kusisitiza kuwa, muungano huo vamizi utabeba dhima ya mripuko wowote wa corona nchini humo.
Hii ni katika hali ambayo, hapo jana, duru za habari ziliripoti kuwa, muungano huo vamizi unaoongozwa na Saudia katika vita vya Yemen umekiuka mara 108 makubaliano ya usitishaji vita katika mji wa al-Hudaydah katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita.
Bandari ya al-Hudaydah nchini Yemen ndio njia kuu ya upelekaji misaada ya kibinadamu katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo masikini iliyoharibiwa vibaya na vita pamoja na mashambulio ya anga ya jeshi vamizi la Saudi Arabia na washirika wake tokea mwaka 2015
Sent using Jamii Forums mobile app