Saudi Leaks: Bin Salman anatumia pombe, ni addicted wa dawa za kulevya

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Saudi Leaks: Bin Salman anatumia pombe, ni addicted wa dawa za kulevya

Mtandao wa Saudi Leaks umefichua kuwa, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia, Muhammad bin Salman anatumia dawa za kulevya ni ni mraibu wa heroni.

Mtandao huo umeripoti kuwa, mienendo ya mwanamfalme huyo wa Saudia na wanawake ajnabi na muda mwingi anaotumia katika anasa akiwa pamoja na waraibu wa dawa za kulevya na walevi vinathibitisha kuwa, yeye pia ni mmoja wao.

Saudi Leaks imeripoti kuwa, utumiaji wa mihadarati na dawa za kulevya umeathiri sana mienendo na afya ya mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia, Muhammad bin Salman.

Mapema mtandao wa al A'hd al Jadid ulikuwa umeripoti kuwa, unazo taarifa za kuaminika zinazothibitisha kuwa Bin Salman anatumia madawa ya kulevya na kwamba ameanza kutumia kokeini.

Mtandao huo umeripoti kuwa, utumiaji wa madawa ya kulevya umeathiri sana mienendo ya Bin Salman kiasi kwamba, hakutani na watu na hawezi kushiriki mkutano wowote bila ya kutumia madawa ya kulevya.

Habari hiyo imeungwa mkono na mwandishi mashuhuri wa Marekani, Michael Wolf ambaye amesisitiza kwamba, Bin Salman anaendelea kutumia madawa ya kulevya na kwamba serikali ya Marekani inalijua vyema jambo hilo.

Wolf ameyasema hayo katika kitabu chake alichokipa jina la "Siege: Trump Under Fire" akiashiria hitilafu kubwa zinazotafuna kizazi cha watawala wa Saudi Arabia.

4bpn25ff66e4301362h_800C450.jpeg
4bpl5a1b61dd5710lxw_800C450.jpeg
 
Hii inaonyesha jinsi zile nchi zilizochukua jukumu la kusambaza dini duniani zilivyokata tamaa kuhusu Mungu. Hata ulaya waliotuletea dini huku africa matendo yao yanaonyesha kwamba hawathamini hizo dini.
 
Back
Top Bottom