Saudi Arabia yafuta adhabu ya kifo kwa watoto siku moja baada ya kufuta adhabu ya viboko

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Tume ya Haki za Binadamu nchini humo imesema Serikali ya Taifa hilo imepiga marufuku adhabu ya vifo kwa watoto ikiwa ni muendelezo wa hatua mpya za mabadiliko zinazotekelezwa

Kamisheni hiyo inasema hakuna mtoto atakayekutwa na hatia na kupewa adhabu ya kifo, badala yake atatumikia kifungo kisichozidi miaka 10 katika gereza la watoto

Hatua hiyo inachukuliwa, ikiwa ni siku moja tu baada ya Utawala wa Kifalme wa Taifa hilo kufuta adhabu ya kuchapwa viboko

Shirika la Kimataifa la Utetezi wa Haki za Binadamu (Amnesty International) limeiweka Saudi Arabia katika orodha ya Mataifa yenye kunyonga watu wengi zaidi, baada ya Iran na China

Ripoti ya hivi karibuni ya Amnesty International kwa mwaka 2019 inaonesha Taifa hilo limewanyonga watu 184
 
... yaani huko watoto walikuwa wanakatiwa adhabu ya kifo? Hatari sana. Waliokuwa wanasifia sheria ya zamani ndio hao hao watakuja hapa kusifia mabadiliko haya!
 
Ah huyo si rafiki yake Marekani na nasikia Marekani anaulinda huo ufalme wenye kunyonga watu ila kamzuia Makonda kwenda Marekani.
 
Back
Top Bottom