Saudi Arabia, Uturuki, kuswali Iddi Jumanne Juni 4, 2019

Vipi kama ungeonekana Tz na usionekane Saudi Arabia je wangekubali leo Eid????
Mbona jana umeonekana dodoma na haikutangazwa?

Kama una mtu yupo dodoma barabara ya saba mpigie muulize atakuambia.
 
wameuona lini huo mwezi?
Kiufupi mambo ya mwezi haitakiwi uweke tarehe maalum kwamba ni siku fulani.

Ukiangalia kalenda imeandika iddi ni tarehe 5 na 6 manake serikali inatambua hivyo.
Sasa wewe ungekuwa mufti ungetangaza IDDI NI tarehe 4 na wakati kiserikali inachojulikana ni tarehe 5 na 6?
 
Akhy! Tumuogope Mungu! Mwezi uonekane Dodoma halafu usitangazwe? Dodoma ni karibu hapo, taarifa zingesambaa kwa kasi sana kuliko hata kutangazwa kwenye medias tofauti.

Kama unafuatilia mwenendo wa mwezi siku ya Jumapili swalatu subhi mwezi (kwa wakazi wa Dar) ulivyoonekana si mwezi wa kuandama jana. Bali ni mwezi wa kuandama Jumatano jioni.

Bakwata ni kweli wana mapungufu yao na ni kweli ilianzishwa na Nyerere kwa maslahi ambayo tuyaloweke kwanza kuyaanika ni mada nyengine. Lakini kwa hili hapana! Hizi ikhtilafu zimekuwa za kibinafsi mpaka tuna transgress against the limits of Allah.

Kingine Radio Imaan mamlaka ya kutangazwa mwandamo wa mwezi kwa hapa Tanzania wamepewa na nani?
Mwezi umeonekana Radio imam wametangaza na hata Dodoma umeonekena ukitaka uadio ni dm what's up yko
 
Kiufupi mambo ya mwezi haitakiwi uweke tarehe maalum kwamba ni siku fulani.
Ukiangalia kalenda imeandika iddi ni tarehe 5 na 6 manake serikali inatambua hivyo.
Sasa wewe ungekuwa mufti ungetangaza IDDI NI tarehe 4 na wakati kiserikali inachojulikana ni tarehe 5 na 6?
Kwa hiyo mkuu unataka kusema nini hapa? Serikali ndiyo inaamua hatma ya Eidd kwa kuweka tarehe mahsusi kwa ajili eidd? Al akhy tufuate muongozo wetu unasemaje, Quran na Sunna
 
Akhy! Tumuogope Mungu! Mwezi uonekane Dodoma halafu usitangazwe? Dodoma ni karibu hapo, taarifa zingesambaa kwa kasi sana kuliko hata kutangazwa kwenye medias tofauti.

Kama unafuatilia mwenendo wa mwezi siku ya Jumapili swalatu subhi mwezi (kwa wakazi wa Dar) ulivyoonekana si mwezi wa kuandama jana. Bali ni mwezi wa kuandama Jumatano jioni.

Bakwata ni kweli wana mapungufu yao na ni kweli ilianzishwa na Nyerere kwa maslahi ambayo tuyaloweke kwanza kuyaanika ni mada nyengine. Lakini kwa hili hapana! Hizi ikhtilafu zimekuwa za kibinafsi mpaka tuna transgress against the limits of Allah.

Kingine Radio Imaan mamlaka ya kutangazwa mwandamo wa mwezi kwa hapa Tanzania wamepewa na nani?
Kwanza kusema kwamba ni wa kuandama j5 wewe ulijuaje kama utaandama j5?

Kuhusu waliopewa mamlaka ya kutangaza mwezi kwanza tujue kwamba hayo mamlaka ya kuutangaza katoa nani ?
 
Kwa hiyo mkuu unataka kusema nini hapa? Serikali ndiyo inaamua hatma ya Eidd kwa kuweka tarehe mahsusi kwa ajili eidd? Al akhy tufuate muongozo wetu unasemaje, Quran na Sunna
Kuna mwaka ilitokea bakwata wakatangaza eid kinyume na eid ya kwenye kalenda ?

Qurani na sunna mimi vimenitosheleza kufuata mwezi wa popote unapoonekana kwa kigezo cha taarifa.
 
Marejro katika Qurani na sunna.lakini pia nilitaka nikuambie kwamba licha ya kuwa kufuata mwezi wa popote ni kauli ambayo ipo katika sheria ya kiislamu na kuna wanachuoni wamezungumza hilo basi pia sheria ya nchi haihesabu kama ni kosa la jinai kusali iddi.

Lengo ni kumsahihisha huyo ndugu anaesema kwamba ingekuwa saudia basi salafy waliotangulia wangepewa adhabu za kinidhamu.

Ahuko saudia wameshajiwekea kwamba wao wanaangalia nchi yao tu manake ni taratibu rasmi ambayo hata mfalme naye amenaaifahamu na wamekubaliana kwa dola na wanachi wake na wanazuoni wake.

Lakini licha ya kukubaliana kwako basi hakuna katika sheria ya kiislamu kwamba watu watakaofungua mapema katika mji eti waadhibiwe ,labda iwe Dola imeweka msimamo maalum alafu watu wakakengeuka.

Hii serikali ya tanzania ina msimamo gani kuhusu mwezi?

Inawachukulia vipi kisheria wale waliotangulia ?
Kuna Taasisi za kidini zimepewa mamlaka na Serikali ya Tz ndizo ziwe vipaza sauti kwa dini husika na ni suala ambalo lipo kwenye nchi nyingi(zilizo za Kiislamu na sisizo za Kiislamu).

Ikhtilafu kuhusu suala la mwandamo wa mwezi Sheikh Ibn Baaz alitembele Afghanistan( kama nimekosea itakuwa ni Pakistan). Aliulizwa swali na raia wa Saudi Arabia wanaosoma huko wafuate mwezi upi(?) Wa nyumbani Saudia au wa nchi waliyopo? Kufupisha "insha" Sheikh aliwajibu wafuate mwezi wa nchi waliyopo.

Sheikh ibn Uthaymiin aliulizwa swali kama hili akajibu ni swala ambalo haliwezekani kuwa na mwezi mmoja kwa Dunia. Na ndiyo fatwa iliyotolewa na jopo la wana wa zuoni wa Kisunni al Jamaa mkutano ambao uliyofanyika Saudi Arabia. Na ndiyo fatwa ambayo iliyopo na ndiyo fatwa inayoishi mpaka muda huu.

Kwenye mkutano huo maulamaa wakasema masuala ya mwezi muandamo yaachwe kwa Mufti na Qadhi. Sheikh Muhammad Bin Abdul Rrahman Al Arifi wa Saudiya akasema mantiki ya suala hilo kuachwa kwa Qadhi na Mufti ni kufanya ummah wa kiislam uwe ni mmoja kwenye mipaka ya Tawala husika. Kila mtu/Taasisi ikitoa tamko lake tutawagawanya Waislam na ni suala ambalo halipendezi.

Bila shaka wewe ni mwenye kumbukumbu nzuri. Ikhtilafu za kimwezi kwa kutamkwa na Taasisi tofauti tofauti ilifikia pahala Waislam kwa Waislam wakawa wanaitana Makaaafir! Wengine wakachupa mipaka na kuwaambia wasiyokuwa na msimamo wao kwamba Funga yenu haiswiih. Sasa tunakwenda wapi?

Unafikiri ni nini hekima ya Mualamaa kusema hilo suala liachwe kwa Qadhi ama Mufti? Radio Imaan mamlaka ya kutangaza mwandamo wa mwezi wameyatolea wapi kama si kuugawanya ummah wa Kiislam Tanzania? Kwa sababu ndani ya Tz kuna Taasisi ndiyo imepewa mamlaka ya kutangaza mwezi.

Hata kama hiyo Taasisi ina madhaifu yake lakini ikifanya lililo sahihi tuwapongeze. Mufti tuliyenaye sasa hivi hapendi mikingamo. Ndiyo maana wakati wake mikingano imepungua. Licha ya madhaifu waliyonayo Bakwata lakini alipofikia Mufti ni pazuri. Radio Imaan anakuja analeta ikhtilafu zisizokuwa na msingi, anatangaza mwandamo wa mwezi kwa mamlaka gani.

Alaaa kulli hal! Kuna mwana wa zuoni mmoja nimemsahamu kwa jina. Yeye kauli yake imejikita kwenye hadithi ya Mtume rehma na amani ziwe juu yake kwa kusema: "Fuata lisilo kutia shaka na uache linalokutia shaka." Kwa hiyo akasema atakayeamua yoyote kuhusu mwezi mwandamo afanye lisilomtia shaka na asifanye linalomtia shaka midhali awe na uthibitisho kwa anachokisimamia. Lakini likiwa ni suala la mtu binafsi na wala si kwa kuhidhirisha kwa kuikhtalfiana na mamlaka ya Nchi. Kwa kufanya hivyo utawagawanya Waislam.
 
Mwaka Juzi(kama sijakosea) NASA walitangaza kutatokea Solar Eclipse. Wakataja nchi zikazopata hiyo eclipse na wakataja a full solar eclipse itatokea ukanda upi nchi husika! Napo palikuwa ni Mbeya a full solar eclipse ilitokea. Huu mfano unauelewaje ndugu yangu?

Wenye mamlaka ya kutangaza mwezi kwa hapa Tanzania ni BAKWATA. Nafahamu hiyo Taasisi tuliundiwa pasipo mkono wa Waislmu kutia baraka. Hatuna jinsi na ndivyo hali jinsi ilivyo na ndivyo imekuwa hivyo.

Suali lako nalijibu kwa swali pia. Mamlaka ya kutangaza mwezi muandamo hapa Tz kwa Radio Imaani wameyatolea wapi mpaka wewe imekukinai umetumia kuwa moja ya marejeleo yako?

Kuhusu kauli ambazo umezitoa juu ya mwezi ni sahihi mkuu zipo fatawa nyingi za ulamaa zinasema hivyo kwwmba watu wafunge na Nchi zao.

Hata pia tukirudi katika historia hapo zamani sidhani kama iliwahi kutokea kwamba mji mmoja masahaba wakala eid leo na mji ungine wakala eid kesho.

Lakini jambo ambalo nataka tuliangalie ni kuhusu muandamo wa mwezi.

Kuna dada wa mkwe wangu yupo kigoma,alipigiwa simu jana na mkwe wangu akamuuliza kuhusu mwezi akamwambia " mwezi nauona hapa na watoto wanapiga kelele na siku zangu ni 28 nafanyeje ?"

Kwamba jana yeye aliuona mwezi na yuko na siku 28.

Saudi arebia wana haki ya kufuata Nchi yao kwa sababu jitihada zao wanazozifanya kuhusu mwezi ni kubwa,na maulamaa wameshakubaliana na hilo.

Hata mimi hapa lau wakikaa wakakibaliana kuhusu mwezi pande zote za maulamaa wakatoka na tamko moja basi mimi nitafuata tamko hilo na kulifanyia kazi.

Saudia si umeona kuna kamati ya kudumu ya kutoa fatwa?
Hapa kwetu hatuoni juhudi zozote zinazofanyika kulimaliza hili suala.

Maulamaa wa saudia hawawezi kukuambia fuata mwezi wa popote wakati wao wanafuata mwezi wa Nchi yao.ni jambo linataka umoja na upendo.

Sikatai hizo fatwa lakini mimi kwa nini nisione kwamba kauli za ulamaa wanaosema kufuata mwezi wa popote ndo ina nguvu ?

Kwa maana nyingine ni kwamba kama kuna kauli za ulamaa wanaoruhusu mwezi wa popote na nikaona zina nguvu na nikazifuata pasi na kuvunja sheria za nchi,na ikawa kuna kundi la watu wanafanya hapo unadhani ukinipa faywa ya ibn uthaymeen utakuwa umenitoa shaka na tongotongp?
 
Radio imani inatambulika ni kitu gani katika serikali ya tanzania?.
 
Mwaka Juzi(kama sijakosea) NASA walitangaza kutatokea Solar Eclipse. Wakataja nchi zikazopata hiyo eclipse na wakataja a full solar eclipse itatokea ukanda upi nchi husika! Napo palikuwa ni Mbeya a full solar eclipse ilitokea. Huu mfano unauelewaje ndugu yangu?

Wenye mamlaka ya kutangaza mwezi kwa hapa Tanzania ni BAKWATA. Nafahamu hiyo Taasisi tuliundiwa pasipo mkono wa Waislmu kutia baraka. Hatuna jinsi na ndivyo hali jinsi ilivyo na ndivyo imekuwa hivyo.

Suali lako nalijibu kwa swali pia. Mamlaka ya kutangaza mwezi muandamo hapa Tz kwa Radio Imaani wameyatolea wapi mpaka wewe imekukinai umetumia kuwa moja ya marejeleo yako?
Mfano wako nimeuelewa kama ulivyoutoa.
Labda ungesema umekusudia nini katika mfano huo...
 
Kuelewa ni ufahamu.

Makusudio/kusudio ni neno lenye maana nyingi. Miongoni mwa ufafanuzi wa hilo neno ni Lengo, Maana, Azimio....

Mantiki ya suala fulani ni kulielewa suala fulani, na kuelewa ndiyo ufahamu na ufahamu unasafiri na maana kwa pamoja. Ili ufahamu kitu inabidi ujue maana ya kitu.

Umeuelewaje huo mfano?

Kwa hiyo lengo la mfano wako ule juu ya mada yetu ya mwezi ni ipi?

Habari za kuzungukana na kuleta falsafa za maneno mengi hakuna asiyeweza.

Muhimu toa mfano uweke na lengo kwa maana mifano iwe inaambatana na hoja kwa ajili ya kutilia nguvu.

Lengo la mfano wako wa mbeya ni lipi kutokana na mada yetu?
 
Naomba radhi muda wangu ni mchache. Baadae inshaallah nitarudi ili tuweze kuongezeana maarifa ya hapa na pale.

Bila shaka Iddie kwako imekuwajibikia leo, Eid Mubarakah! Hammaz ni miongoni mwa waliyofunga leo. Kila la khayr akhy.

Assalamu alaykum warahmatullahi wabarakatuh.

Back
Top Bottom