Saudi arabia imeshikwa pabaya Yemen?makombora yanapiga kila mahali ina maana silaha za mabilioni kutoka kwa trump zimefeli?

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Mashambulio manne ya makombora katika siku tatu; tukio la aina yake katika vita vya Yemen
Aug 04, 2019 10:50 UTC
Ikiwa ni katika kujibu mashambulio na jinai za kinyama zinazotekelezwa na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya Yemen, katika kipindi cha siku tatu, jeshi na kamati za wananchi wa nchi hiyo zimetekeleza mashambulio manne muhimu ya makombora katika maeneo tofauti ya Saudia na vilevile kusini na kaskazini magharibi mwa Yemen ambapo makumi ya askari na mamluki wa nchi hiyo ya kifalme wameuawa na kujeruhiwa.
Shambulio la kwanza la makombora lilifanyika siku ya Alkhamisi katika kambi ya kijeshi ya al-Jala'a katika mji wa al-Barqiya magharibi mwa mkoa wa kusini wa Aden.
La pili na ambalo lilikuwa kubwa zaidi kuliko hilo la kwanza, kwa kuzingatia kuwa lilifanyika katika kituo muhimu cha kijeshi katika eneo la Sammam, mji mkuu wa eneo la As-Sharqiya mashariki mwa Saudi Arabia, lilifanyika siku hiyo hiyo ya Alkhamisi.
Shambulio la tatu pia lilitekelezwa katika kambi ya kijeshi ya Saudia katika mkoa wa al-Hujja, kaskazini mwagharibi mwa Yemen na ambayo inawajumuisha mamluki wanaokodiwa na Saudia kutoka Sudan.
Shambulio la nne lilifanyika jana Jumamosi ambapo kituo kingine kipya cha kijeshi cha Saudia kililengwa katika eneo la Najran, kusini mwa nchi hiyo.
Mashambulio hayo ya kufuatana yametekelezwa yakiwa yamebeba ujumbe maalumu na muhimu wa kistratijia.
Mosi ni kwamba, shambulio la kwanza lililotekelezwa siku ya Alkhamisi katika kambi ya kijeshi ya al-Jala'a katika mkoa wa Aden, lililenga gwaride la askari wa serikali kibaraka na iliyojiuzulu ya Yemen ambapo zaidi ya askari 40 waliuawa. Jambo hilo linathibitisha wazi ulengaji makini wa shabaha wa makombora ya jeshi la Yemen.
Nukta ya pili ni kuwa mashambulio ya ad-Dammam yana umuhimu wa kistratijia. Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi 52 iliyopita, jeshi na kamati za wananchi wa Yemen zimefanikiwa kulenga shabaha ya kijeshi katika nukta ya mbali zaidi ndani ya ardhi ya Saudi Arabia. Kulengwa kituo hicho cha kijeshi kunaonyesha wazi mafanikio makubwa ya jeshi na kamati hizo za wananchi wa Yemen katika kukusanya habari za siri kuhusiana na vituo muhimu vya kijeshi vya adui. Kabla ya hapo jeshi na kamati hizo za wananchi zilikuwa zimetangaza kuainishwa kwa vituo muhimu na nyeti 300 ndani ya ardhi ya Saudia na Imarati vinavyoweza kulengwa wakati wowote na makombora pamoja na ndege zisizo na rubani za Yemen.
Nukta ya tatu inahusiana na kuchaguliwa masafa marefu ya kilomita 1300 kwa ajili ya kurushwa kombora hilo. Katika kuchambua shambulio hilo, kanali ya habari ya Russia al-Yaum imesema kuwa tukio hilo ni la aina yake na kuongeza kuwa: Jambo linalotofautisha shambulio hilo na mashambulio mengine yote ya makombora ambayo yamewahi kutekelezwa katika maeneo tofauti ya kijeshi ya Saudia ni kwamba hiyo ni mara ya kwanza kwa kombora la Yemen kuweza kurushwa kwa masafa marefu kama hayo. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kabla ya hapo Riyadh ndiyo iliyokuwa nukta ya mbali zaidi ambayo makombora ya Wayemen yangeweza kufika.
Nukta ya nne ni kuwa mji wa Dammam ni kituo muhimu cha mashirika mengi ya kiuchumi na pia makao makuu ya shirika la uuzaji nje mafuta la Saudia, Aramco. Hivyo kulengwa mji huo wa kistratijia kuna maana ya kuwafikishia watawala wa Saudia ujumbe huu kwamba wao na washirika wao wa Imarati wanapasa kulipa gharama kubwa za kiuchumi kutokana na mashambulio yao ya kichokozi dhidi ya Yemen. Akizungumzia suala hilo, Abdulwahhab al-Mahshabi, mwanachama wa Ofisi ya Kisiasa ya Ansarullah amesema: Operesheni ya ad-Dammam itaharakisha kuondoka kwa askari wa Imarati nchini Yemen.
Nukta ya tano kuhusiana na mashambulio hayo ya makombora ni kwamba yanatoa ujumbe wa 'kulipiza kisasi' na pia ni hatua ya kujilinda.
Brigedia Jenerali Yahya Saree', Msemaji wa Jeshi la Yemen anasema kuhusiana na mashambulio hayo: Mapigo hayo yametolewa kama radiamali kwa jinai zinazotekelezwa na wavamizi, kuzingirwa Yemen, kuendelea uvamizi na kumwagwa damu ya watu wa Yemen.
Nukta ya mwisho ni kwamba mashambulio ya makombora ya karibuni ya jeshi na kamati za wananchi wa Yemen yanathibitisha wazi kwamba Saudia imekwama kwenye kinamasi cha vita vya Yemen na kwamba kuendelea vita hivyo vya kivamizi bila shaka kutakuwa na gharama kubwa kwa nchi hiyo na washirika wake wa Imarati.
4bsjf4da72d9e91gbej_800C450.jpeg
4bsjb41044943f1good_800C450.jpeg
 
Mmarekani yeye hawezi kurusha kombora la moja kwa moja kutoka kwake yeye anatumia nchi nyingine kumpa silaha kwa kigezo cha kumuuzia yeye anafanyia biashara hapo hapo
 
hata mi nashindwa kuelewa kwanini patriotic Ant Air misile system ya mmarekani inashindwa kuyatungua hayo makombora kutoka Yemen
Mmarekani anauza utaalam na silaha kotekote. Utakuja kusikia story za CIA kuwapelekea ujuzi wa drones na silaha haohao wanamapinduzi wa Hauthi miaka si mingi ijayo.

Marekani hasa Trump anataka mataifa yote ya waislam ikiwepo Saudi Arabia yawake moto. Tatizo la Saudi Arabia ni uongozi wa ki-nguruwe.

Afadhali ya Irani iliyogundua mapema kuwa kushirikiana na Marekani ni sawa na kujitumbukiza kwenye tenki la petroli. Dakika yoyote Trump akipandwa na mapepo anawasha kiberiti.
 
Mashambulio manne ya makombora katika siku tatu; tukio la aina yake katika vita vya Yemen
Aug 04, 2019 10:50 UTC
Ikiwa ni katika kujibu mashambulio na jinai za kinyama zinazotekelezwa na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya Yemen, katika kipindi cha siku tatu, jeshi na kamati za wananchi wa nchi hiyo zimetekeleza mashambulio manne muhimu ya makombora katika maeneo tofauti ya Saudia na vilevile kusini na kaskazini magharibi mwa Yemen ambapo makumi ya askari na mamluki wa nchi hiyo ya kifalme wameuawa na kujeruhiwa.
Shambulio la kwanza la makombora lilifanyika siku ya Alkhamisi katika kambi ya kijeshi ya al-Jala'a katika mji wa al-Barqiya magharibi mwa mkoa wa kusini wa Aden.
La pili na ambalo lilikuwa kubwa zaidi kuliko hilo la kwanza, kwa kuzingatia kuwa lilifanyika katika kituo muhimu cha kijeshi katika eneo la Sammam, mji mkuu wa eneo la As-Sharqiya mashariki mwa Saudi Arabia, lilifanyika siku hiyo hiyo ya Alkhamisi.
Shambulio la tatu pia lilitekelezwa katika kambi ya kijeshi ya Saudia katika mkoa wa al-Hujja, kaskazini mwagharibi mwa Yemen na ambayo inawajumuisha mamluki wanaokodiwa na Saudia kutoka Sudan.
Shambulio la nne lilifanyika jana Jumamosi ambapo kituo kingine kipya cha kijeshi cha Saudia kililengwa katika eneo la Najran, kusini mwa nchi hiyo.
Mashambulio hayo ya kufuatana yametekelezwa yakiwa yamebeba ujumbe maalumu na muhimu wa kistratijia.
Mosi ni kwamba, shambulio la kwanza lililotekelezwa siku ya Alkhamisi katika kambi ya kijeshi ya al-Jala'a katika mkoa wa Aden, lililenga gwaride la askari wa serikali kibaraka na iliyojiuzulu ya Yemen ambapo zaidi ya askari 40 waliuawa. Jambo hilo linathibitisha wazi ulengaji makini wa shabaha wa makombora ya jeshi la Yemen.
Nukta ya pili ni kuwa mashambulio ya ad-Dammam yana umuhimu wa kistratijia. Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi 52 iliyopita, jeshi na kamati za wananchi wa Yemen zimefanikiwa kulenga shabaha ya kijeshi katika nukta ya mbali zaidi ndani ya ardhi ya Saudi Arabia. Kulengwa kituo hicho cha kijeshi kunaonyesha wazi mafanikio makubwa ya jeshi na kamati hizo za wananchi wa Yemen katika kukusanya habari za siri kuhusiana na vituo muhimu vya kijeshi vya adui. Kabla ya hapo jeshi na kamati hizo za wananchi zilikuwa zimetangaza kuainishwa kwa vituo muhimu na nyeti 300 ndani ya ardhi ya Saudia na Imarati vinavyoweza kulengwa wakati wowote na makombora pamoja na ndege zisizo na rubani za Yemen.
Nukta ya tatu inahusiana na kuchaguliwa masafa marefu ya kilomita 1300 kwa ajili ya kurushwa kombora hilo. Katika kuchambua shambulio hilo, kanali ya habari ya Russia al-Yaum imesema kuwa tukio hilo ni la aina yake na kuongeza kuwa: Jambo linalotofautisha shambulio hilo na mashambulio mengine yote ya makombora ambayo yamewahi kutekelezwa katika maeneo tofauti ya kijeshi ya Saudia ni kwamba hiyo ni mara ya kwanza kwa kombora la Yemen kuweza kurushwa kwa masafa marefu kama hayo. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kabla ya hapo Riyadh ndiyo iliyokuwa nukta ya mbali zaidi ambayo makombora ya Wayemen yangeweza kufika.
Nukta ya nne ni kuwa mji wa Dammam ni kituo muhimu cha mashirika mengi ya kiuchumi na pia makao makuu ya shirika la uuzaji nje mafuta la Saudia, Aramco. Hivyo kulengwa mji huo wa kistratijia kuna maana ya kuwafikishia watawala wa Saudia ujumbe huu kwamba wao na washirika wao wa Imarati wanapasa kulipa gharama kubwa za kiuchumi kutokana na mashambulio yao ya kichokozi dhidi ya Yemen. Akizungumzia suala hilo, Abdulwahhab al-Mahshabi, mwanachama wa Ofisi ya Kisiasa ya Ansarullah amesema: Operesheni ya ad-Dammam itaharakisha kuondoka kwa askari wa Imarati nchini Yemen.
Nukta ya tano kuhusiana na mashambulio hayo ya makombora ni kwamba yanatoa ujumbe wa 'kulipiza kisasi' na pia ni hatua ya kujilinda.
Brigedia Jenerali Yahya Saree', Msemaji wa Jeshi la Yemen anasema kuhusiana na mashambulio hayo: Mapigo hayo yametolewa kama radiamali kwa jinai zinazotekelezwa na wavamizi, kuzingirwa Yemen, kuendelea uvamizi na kumwagwa damu ya watu wa Yemen.
Nukta ya mwisho ni kwamba mashambulio ya makombora ya karibuni ya jeshi na kamati za wananchi wa Yemen yanathibitisha wazi kwamba Saudia imekwama kwenye kinamasi cha vita vya Yemen na kwamba kuendelea vita hivyo vya kivamizi bila shaka kutakuwa na gharama kubwa kwa nchi hiyo na washirika wake wa Imarati.View attachment 1172119View attachment 1172120

Hawa wanapigana vita kama wanaenda holiday wakati wenzao wana maanisha. Vietnam ilikuwa hivyo hivyo kwa bwana mkubwa
 
Mmarekani yeye hawezi kurusha kombora la moja kwa moja kutoka kwake yeye anatumia nchi nyingine kumpa silaha kwa kigezo cha kumuuzia yeye anafanyia biashara hapo hapo
Yes wazungu wajanja sana
 
Back
Top Bottom