Sauti ya Umma
Member
- Aug 26, 2010
- 37
- 20
CHAMA CHA SAU CHAWASHAURI WANASIASA KUIUNGA MKONO SERIKALI YA AWAMU YA 6
Katibu Mkuu wa Chama cha siasa cha Sauti ya Umma (SAU ) Majalio Kyara akizungumza na Mtandao huu+ ofisini kwake Mgomeni Kagera jijini Dar es salaam.
NA MUSSA KHALID DAR ES SALAAM
Katibu Mkuu wa Chama cha siasa cha Sauti ya Umma (SAU ) Majalio Kyara amewashauri viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa nchini kuendelea kuonyesha ushirikiano kwa serikali ya awamu ya sita ili taifa liendelee kukua kimaendeleo.
Kyara amezungumza hayo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii ofisini kwake ambapo amesema mwenendo unazidi kuimarika kwa nyanja tofauti tofauti za kisiasa tangu kuingia serikali ya awamu ya sita ikiwemo pia kuwasikiliza wananchi wake hasa baada ya kupunguza tozo za simu kufuatia wananchi na wadau mbalimbali kupaza sauti zao.
Katibu huyo mkuu amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kutosikiliza maneno ya wanasiasa wasiopenda mafanikio yake badala yake aendelee kuchapa kazi ili kuendelea kufanikisha taifa kuwa na maendeleo.
‘Namuomba Mhe Rais asisikilize miluzi mingi atapotea yeye apige kazi ameanza vizuri anakwenda vizuri kwani tunanaona jinsi gani anavyokwnda na sisi tunamatumaini naye asijali binadamu kwani hata ufanye jema ataangalia yale mabaya lakini mema hatusemi’amesema Kyara.
Aidha akizungumzia suala za tozo za simu Kyara amesema malengo ya Rais Samia anataka nchi kukimbia kimaendeleo iweze kufika mbali jambo ambalo amewaasa wasaidizi wake kuangalia namna ya kupunguza tozo hizo ili wananchi wachangangie kwa amani na furaha.
‘Kubwa zaidi ninaloliona watendaji au wasaidizi wa Mhe Rais wengi hawajajua nini lengo la Rais wao wakishaona sababau wanatafuta fedha basi wanapiga mabei makubwa makubwa lakini ukija kuangalia lengo la rais anataka twende mbele tukusanye mapato makubwa tujenge nchi yetu lakini sisi wenyewe kuishi maisha bora’amesema Kyara.
Katibu huyo hakusita kuwashauri baadhi ya viongozi wa chama kilichopo madarani kuwa wamsaidie Mhe Rais kwa kufanya maamuzi yaliyosahihi na siyo kutaka kushindana na mienendo yake kwa taifa linalojengwa ni moja.
Katika Hatua nyingine Kyara amemuomba Rais kukutana na viongozi wa vyama vya siasa ili kujadili masuala mbalimbali yeny nia ya kujnga mustakali wa Taifa la Tanzania.