Satta wa Zambia aendelea kufanya makubwa, chadema 2015 tunataka haya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Satta wa Zambia aendelea kufanya makubwa, chadema 2015 tunataka haya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gwota, Feb 5, 2012.

 1. Gwota

  Gwota JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hakika, ya Michael Sata yatatua Tanzania siku moja!

  Johnson Mbwambo

  Si siri, nasi twamhitaji King Cobra wetu

  WIKI iliyopita hakuna habari zilizonisisimua katika duru za kimataifa kushinda zile zilizotawala vyombo vya habari vya Zambia.
  Habari hizo ni hatua ya Rais Michael Sata kurejesha serikalini umiliki wa kampuni kubwa ya simu ya nchi hiyo – Zamtel.

  Kilichotokea huko Zambia ni kile ambacho nilimtarajia Rais wetu, Jakaya Kikwete, angekifanya alipoingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 2005, lakini hakukifanya, na hajakifanya hata sasa anapomaliza awamu yake ya pili na ya mwisho ya uongozi.

  Lakini kabla ya kulijadili hilo, nirejee kwanza kwenye hatua hiyo ya aina yake iliyochukuliwa na Rais huyo wa Zambia ambaye ni maarufu nchini humo kwa jina la utani la King Cobra.


  Wakati wa kampeni za urais za mwaka jana, King Cobra aliwaahidi Wazambia kwamba kama watamchagua kuingia Ikulu, moja ya mambo atakayoyafanya haraka ni kuirejesha Zamtel mikononi mwa umiliki wa serikali kwa kuwa iliuzwa kifisadi kwa kampuni ya LapGreen ya Libya.


  Nina hakika ahadi hiyo ya King Cobra ni miongoni mwa zilizowafanya wapiga kura wa Zambia wampigie kura nyingi zilizomwezesha kuwa rais mpya wa nchi hiyo.


  Tofauti na marais wengine wa Afrika ambao wakati wa kampeni huwaahidi wapiga kura kuwa wakichaguliwa urais watapambana na ufisadi lakini wakishaingia ikulu hawafanyi kitu, Michael Sata yeye alianza mara moja kutekeleza ahadi zake dhidi ya ufisadi.


  Novemba mwaka jana aliunda timu maalumu ya wataalamu kuchunguza mauzo ya kampuni hiyo ya umma kwa mwekezaji huyo kutoka Libya (LapGreen). Timu hiyo iliongozwa na Waziri wa Sheria, Sebastian Zulu.


  Katika ripoti yake, timu hiyo ilithibitisha kile ambacho Wazambia wengi walikuwa wakikilalamikia kwa muda mrefu; yaani kwamba Zamtel iliuzwa kwa ‘bei poa' kwa kampuni hiyo ya Libya.


  Kwa maneno mengine, bei ambayo LapGreen iliuziwa Zamtel na Serikali ya Rais wa wakati huo, Rupiah Banda, ilikuwa hailingani na thamani halisi ya kampuni hiyo. Licha ya kuwa na mali nyingi (majengo nk) Zamtel iliuzwa kwa dola milioni 257 tu.


  Lakini pia timu hiyo iligundua kwamba kulikuwa na ufisadi mkubwa ulioshamiri katika ngazi zote za mchakato wa kuiuza kampuni hiyo ya umma kwa mwekezaji huyo wa Libya.


  Ni baada ya kuipokea ripoti hiyo na kuisoma, King Cobra aliamua, wiki iliyopita, kushambulia kwa kuirejesha kampuni hiyo serikalini.


  Alifanya hivyo kwa kutengua mauzo hayo, kusimamisha akaunti zake na kuvunja bodi iliyokuwepo na kuweka mpya.

  Ingawa pia, wiki hiyo hiyo, Rais Sata alitengua mauzo ya benki iliyokuwa ya umma ya Finance Bank iliyouzwa kwa dola milioni 5.4 tu kwa kampuni ya Afrika Kusini inayoitwa First Rand Group, utenguzi wa mauzo ya Zamtel ndio uliopokewa kwa furaha kubwa mno na Wazambia wengi.

  Ndugu zangu, kilichonisisimua kuhusu King Cobra si tu ujasiri aliojipa wa kufanya kitu ambacho marais wengi wa Afrika (akiwemo Kikwete wetu) hawana ujasiri wa kukifanya, lakini pia ni namna alivyoliendesha zoezi la kuirejesha kampuni hiyo mikononi mwa serikali kwa ufanisi mkubwa.


  Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Zambia, hakuna huduma zozote zilizotetereka Zamtel wakati wa utekelezaji wa mchakato huo. Aidha, hakuna ajira hata moja iliyopotea kati ya 1,700 zilizomo katika kampuni hiyo.


  Labda nisisitize hapa mapema kabisa kwamba King Cobra, hakuchukizwa na kuuzwa kwa Zamtel kwa LapGreen ya Libya; bali alichukizwa na kitendo cha kampuni hiyo ya umma kuuzwa kwa ‘bei poa' mno kiasi cha kuwafanya Wazambia wote waonekane ni mabwege.


  Kwa maana hiyo, LapGreen au kampuni nyingine yoyote inaweza kuanzisha mazungumzo mengine na Serikali ya King Cobra ya kuinunua upya Zamtel – tofauti tu ni kwamba safari hii itauzwa kwa bei stahiki, na si ya kutupa!


  Tukirejea ya kwetu hapa nyumbani Tanzania, swali la kujiuliza ni hili: Je, tuna fundisho lolote tunalolipata kutoka katika hicho kilichojiri Zambia wiki iliyopita?


  Jibu langu ni kwamba lipo funzo kubwa tunalolipata; nalo ni kwamba ipo siku moja hayo yaliyotokea Zambia yatatokea pia Tanzania.


  Kwa maneno mengine, watawala wetu waliosimamia uuzwaji wa makampuni yetu ya umma kwa "bei poa" baada ya kukatiwa ten percent zao, hawako salama kabisa kama ambavyo pia hazipo salama kabisa hizo kampuni zilizoyanunua.


  Ningeweza kutaja hapa orodha ndefu ya makampuni yetu mengi ya umma yaliyouzwa kwa ‘bei poa' za kifisadi (ya hivi karibuni ikiwa UDA), lakini niishie tu kwenye uuzwaji wa iliyokuwa benki ya umma – NBC (1997) Limited.


  Nimechagua kuzungumzia NBC tu kuliko makampuni yetu mengine ya umma yaliyouzwa kifisadi, kwa sababu mauzo hayo ya NBC yalipigiwa kelele mno na Watanzania wengi akiwemo Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, lakini aliyekuwa Rais wetu, Ben Mkapa (Mr. Clean?), aliziba masikio yake kwa pamba!


  Benki hiyo iliyokuwa imesheheni raslimali nyingi, yakiwemo majengo karibu miji mikuu ya mikoa yote na wilaya, iliuzwa na Mr. Clean wetu kwa Sh. bilioni 15 tu kwa ABSA ya Afrika Kusini!


  Tena jambo la kushangaza ni kwamba wakati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, akiendesha kampeni ya kuinusuru benki hiyo ya umma isiuzwe, Mr. Clean alikuwa akiendelea na mchakato huo kwa kasi; huku wakati huo huo akiwa ameomba mkopo wa Sh. milioni 500 kutoka ABSA kwa ajili ya kampuni aliyoianzisha na mkewe ya ANBEM.


  Hapo, huhitaji kuwa msomi kuuona mgongano wa kimaslahi (conflict of interest) wa waziwazi katika uuzaji huo wa NBC.

  Na pengine ndiyo maana uuzaji wa benki hiyo unaisumbua nafsi ya Mkapa mpaka leo, na pengine ndiyo sababu vilevile hupendelea kujikosha kuhusu uuzaji huo kila anapopata fursa nzuri ya kufanya hivyo kama alivyofanya wakati wa kampeni za ubunge za Igunga, Septemba mwaka jana.

  Akihutubia mkutano wa kampeni huko Igunga, Mkapa alisema hivi: "Wakati naingia madarakani kulikuwa na benki moja ya biashara – NBC, lakini ilikuwa inaomba ruzuku serikalini; kitu ambacho hakikuwa sahihi.


  "Tukaibinafsisha kwa kuwa huwezi kuwa na benki ya biashara inayoomba ruzuku. Wanasema nimeuza benki yetu, si hivyo. Nimeuza madeni yetu na kusaidia nchi."


  Huo ndio umekuwa utetezi wa Mkapa kila mara anapozungumzia uuzaji wa NBC; kwamba eti aliiuza kwa kuwa ilikuwa inaomba ruzuku serikalini! Anasahau kwamba tuhuma zinazomwandama si tu kuuza benki ya umma kwa mwekezaji aliyekuwa na maslahi naye ya kibiashara (ABSA), lakini kuiuza kwa ‘bei poa' mno sawa na ya kutupa!


  King Cobra
  (Michael Sata) hamshutumu Rais aliyemtangulia, Rupiah Banda, kwa kuiuza Zamtel kwa NetGreen ya Libya; bali anamtuhumu kwa kuiuza kampuni hiyo kwa ‘bei poa' mno!


  Nasi katika Tanzania hatumtuhumu Mkapa kwa kuiuza NBC kwa ABSA, lakini kwa kuiuza kwa ‘bei poa' mno sawa na ya kutupa – bei inayotufanya Watanzania tuonekane wote mabwege!


  Nina hakika hata kama itaundwa timu ya wataalamu leo (miaka 15 baada ya mauzo hayo) na kuchunguza bei ambayo NBC (1997) iliuzwa kwa ABSA, bado matokeo yataonyesha kwamba kwa mali iliyokuwanazo zama hizo (majengo mikoa yote), bei ya shilingi bilioni 15 haikuwa stahiki yetu hata kidogo!


  Nihitimishe hivi:
  Yaliyotokea Zambia, wiki iliyopita, yanatuthibitishia kwamba tunachohitaji Tanzania ni kumpata King Cobra wetu atakayechunguza mashirika yetu yote ya umma yaliyouzwa kifisaadi, na kisha kutengua mauzo hayo; hata kama miaka 20 imepita tangu yauzwe!


  Kwa maneno mengine, watawala waliojineemesha kifedha kwa kuuza mashirika yetu ya umma kifisadi, wasijione salama kabisa hata kama miaka 20 itapita hawajaguswa. Vivyo hivyo kwa hao ‘wawekezaji' walioyanunua kwa bei poa.


  Na wala sizungumzii NBC peke yake. Nazungumzia pia viwanda vyote vya nguo, nazungumzia pia viwanda vyote vya ngozi, nazungumzia pia mashamba ya Mbarali na ya mkonge, nazungumzia pia migodi yetu, nazungumzia pia mashirika kama UDA nk, na nazungumzia pia nyumba zetu za serikali katika maeneo maalumu ambazo wakubwa waliuziana wenyewe kwa wenyewe kwa bei poa.


  Tunachosubiri tu Watanzania ni kumpata King Cobra wetu; yaani rais mpya mwenye ari na nia ya kweli ya kupambana na ufisadi, atakayewapindulia meza mafisadi kwa kutengua mauzo hayo na kuyarejesha mashirika hayo serikalini ili yauzwe upya!

  Nina hakika Kikwete siye rais huyo tunayemsubiri kumpindulia meza Mkapa na wenzake waliouza mali za umma kwa ‘bei poa'.

  Lakini pia naamini King Cobra wetu hawezi kuibukia CCM hii ya sasa iliyopoteza kabisa mwelekeo!


  Tafakari.


  Source: Raia mwema
   
 2. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2012
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kachukua kutoka LapGreen ambayo ni kampuni ya Libya. Kimsingi walibya kipindi hiki wana mgogoro sana kiasi hawataweza kufuatilia mali zao zilizopo nje. Satta namkubali lakini ajaribu kugusa maslahi ya wazungu kama akina chavez wa venezuela hapo pengine anaweza kutushawishi otherwise......but so far so good
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja,mimi nina asira na nyumba walizojiuzia mil nne nne huko masaki na maeneo mengine
   
 4. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2012
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,986
  Likes Received: 1,043
  Trophy Points: 280
  Inanikera zaidi kukumbuka jinsi Kiwanda Cha Sigara (TCC) kilivyouzwa kwa Tshs. 700m (milioni mia saba tu). Wakati thamani tu ya ardhi ya eneo lake lote kwa wakati huo ilikuwa ni zaidi ya hiyo 700m bila ya majengo na mitambo, kweli Tanzania HAKUNAAAAGA!!
   
 5. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Heshima itarudi tu iwapo wananchi wataamua kurudisha nguvu yao kutoka kwa watawala kwa kubadilisha chama na kuweka kingine ambacho watakisimamia kwa nguvu ya umma. Siyo ya leo watawala ndo mabwana wananchi ni watumwa hawana say juu ya mstakabal wa taifa lao wenyewe.
   
 6. BINARY NO

  BINARY NO JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,778
  Likes Received: 587
  Trophy Points: 280
  Mkapa ndie RAIS alie uza rasilimali za waTanzania kuliko yeyote yule...waTanzania tunadanganywa eti Mkapa alijenga BARABARA nyingi ni kweli we ulitegemeea nini na uku MIGODI yote almost ilikua ameuza kwa mikataba ya miaka mpaka 100....BARABARA lifespan yake inaweza kua ata miaka 20 lakini MWADUI na migodi kibao, KIWIRA, ANIBEN, NBC,IPTL,DEEP GREEN, MEREMETA n.k..............

  Laiti km TANZANIA kungekua na TRUE DEMOCRACY huyu alie jihita Mr CLEAN angeozea jela na adhabu ya viboko 12 wakati anaingia na 12 wakati anatoka uku akawaoneshe wakina BAYPORT wake.....

  Ajira zenyewe alikua Hataki kuajiri, nyongeza za mishaara ndo kabisaa na uku wanafunzi wa vyuo tulipotaka kudai haki zetu alifukuzia mbali, hakupenda kuhojiwa abadani...huyu ni zaidi ya FISADI NYANGUMI ni zaidi ya MZUNGU WORSHIPPER nani asye kumbuka ishu ya KILIMANJARO HOTELI kwa kumnyima mzalendo MENGI? huyu cku CDM ikiingia madarakani cpati picha....

  Aliwatesa sana wapinzani nani wakumsahau huyu...aliwaua waZanzabar huyu....aliwafukia watu kwenye machimbo ili awape wazungu wake waliomuahidi barabara.....ili ni km pepo Halina huluma hili eti nalo linaponda sasa.....
   
 7. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2012
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,986
  Likes Received: 1,043
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Hata ndani ya CCM anaweza patikana rais wa aina ya Satta. Je, humkumbuki Levy Mwanawasa wa Zambia?

   
 8. m

  mareche JF-Expert Member

  #8
  Feb 5, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 475
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  kinachotakiwa ni kubadili chama na kuweka jemedari ambaye atasimamia mali za taifa kwa maslai ya watanzania naye si mwingine bali drslaa
   
 9. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  ndio maana serikali ya ccm inatumia mbinu zote kushika dola. Wanajua watafumuliwa mishono tu kwa waliyoyafanya
   
 10. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kilichoenda kwa mganga hakirudi kalagha bao!
   
 11. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  kuna maduwanzi bado wanaimba kidumu ccm. Hakuna watu nawachukia kama hao. Yani ccm ni shetani, hana huruma na sisi na hawezi kutukomboa! ua ccm yote...
   
 12. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #12
  Feb 5, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wiki iliyopita Takukuru ya Satta ilimkamata na kumhoji kwa masaa kadha mke wa rais aliyemtangulia Rupiah Banda kwa tuhuma za money laundering na kwa kuporomosha jengo kabambe la mabilioni mjini Lusaka.

  Hapa kwetu Hosea anaweza kufanya hivyo kwa Anna Mkapa?
   
 13. mzamifu

  mzamifu JF-Expert Member

  #13
  Feb 5, 2012
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 3,496
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  safi sana
   
 14. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #14
  Feb 5, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Mkapa ni mtu wa kufungwa kama tutapata rais mkali na mwenye msimamo anayejali maslai ya Taifa
   
 15. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #15
  Feb 5, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hongera Mh. Satta,
  Eee Mungu Mwenye Enzi zote, nasi waTZ tunaomba utupe mtu kama huyu atuongoze. Amina.
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Feb 5, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,812
  Trophy Points: 280

  Nakubaliana nawe kabisa.
   
 17. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #17
  Feb 5, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kiongozi shupavu/hodari huongoza kwa vitendo zaidi kuliko maneno! Vp ile kauli mbivu yetu ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA...naamini sote tunalia sasa na naamini wanaolia zaidi Ni wale waliochagua CcMfsd.
  kiongozi wa aina hii hawezi kutoka CcMfsd lile chama Ni chafu. Hata Kama atakua msafi basi CcMfsd itamchafua tuuu.....uozo Ni mwingi kuliko usafi.....tuombeni na tusubiri 2015 iko around the corner naamini plus Katiba mpya!! Watang'oka tu.
   
 18. T

  Taso JF-Expert Member

  #18
  Feb 5, 2012
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,648
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Tuna taratibu rasmi na sheria za mununuzi ya Umma. Je tuna taratibu rasmi na sheria za mauzo ya Umma?

  Ukimkubalia Mkapa kwamba NBC kweli ilikuwa ni chombo cha kuzalisha hasara kwa umma, tukakiuza, lakini tatizo Mkapa kauza "kwa bei poa," akikuuliza bei moto bei gani utajibuje? Umejuaje?

  Kama umempa rais au mtu yeyote mtaani mamlaka ya kukuuzia gari lako bovu, na kupanga bei, na kutafuta mteja, hata kama mteja ni shangazi yake aliyemuahidi mkopo wa kukuza mtaji wake wa kuanzishia biashara yake ya taxi basi usimlaumu akitumia "akili zake" kukubaliana bei na mteja kukuuzia mali yako. Si mwenyewe umempa udalali bila utaratibu wowote?

  Nyerere alisema alipewa mamlaka ya kufanya lolote analotaka, isipokuwa tu uzuri wa nafsi yake mwenyewe ndio ulimzuia kufanya mabaya. Aliposema hivyo hatukukimbilia kufanya lolote kwenye vitabu vyetu vya kugawa mamlaka, tukabaki tumekaa kama watazamaji wa ngoma ya Mchiriku, akaja mwingine mkategemea na yeye ana roho ya Nyerere, kumbe jambazi, likawaliza. Kosa la nani?
   
Loading...