Satellite: Kwa nini isibaki angani?

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
7,492
7,515
Kuna habari kuwa kuna satellite iliyozeeka ya Marekani ambayo inatarajiwa kuanguka kurudi huku duniani kwa mujibu wa NASA. Wanasema saizi yake ni kama basi ambapo inategemewa itaweza kuunguka wakati ikiingia kwenye anga la dunia na baadhi ya vipande vyake vitaanguka ingawa haitegemewi kudhuru watu.

Naomba kueleweshwa, ni kwa nini wao(NASA) wanategemea kuwa itaungua. Swali lingine, kwa kuwa huko kwenye anga za juu huwa wanasema kuwa hakuna gravitational force, hivyo vitu huwa vinaelea tu kwenye anga bila kuanguka kuja huku chini, sasa kwa nini satellite hiyo isibaki huko huko juu? Ni kitu gani kinaivuta kurudi huku duniani?
 
Mkuu mimi sıo mtaalam sana wa mambo hayo ıla soon watakuja wataalam
 
Dah, Physics Kwangu Ilikuwa Mwiba Sana, Lakini Swali Taamu Sana, tuwasikilize wataalam watavyosema.
 
kuna habari kuwa kuna satellite iliyozeeka ya Marekani ambayo inatarajiwa kuanguka kurudi huku duniani kwa mujibu wa NASA. wanasema saizi yake ni kama basi. ambapo inategemewa itaweza kuunguka wakati ikiingia kwenye anga la dunia na baadhi ya vipande vyake vitaanguka ingawa haitegemewi kudhuru watu. naomba kueleweshwa, ni kwa nini wao(NASA) wanategemea kuwa itaungua. swali lingine, kwa kuwa huko kwenye anga za juu huwa wanasema kuwa hakuna gravitational force, hivyo vitu huwa vinaelea tu kwenye anga bila kuanguka kuja huku chini, sasa kwa nini satellite hiyo isibaki huko huko juu? ni kitu gani kinaivuta kurudi huku duniani?

In the end, all human-made satellites will
fall back to Earth, since objects eventually
lose velocity and are overcome by the
Earth’s gravity. It may take a very long time
for this to happen, however, because
satellites are so high in space. Satellites near
the Earth in low- Earth orbit may take 10, 20,
or 100 years to fall back to Earth. Satellites
higher up in highly-elliptical or geostationary
orbits may take hundreds, thousands, or
even million of years to fall back to Earth.
Objects falling back to Earth will burn up in
the atmosphere due to the friction caused by
the Earth’s atmosphere.
 
kuna habari kuwa kuna satellite iliyozeeka ya Marekani ambayo inatarajiwa kuanguka kurudi huku duniani kwa mujibu wa NASA. wanasema saizi yake ni kama basi. ambapo inategemewa itaweza kuunguka wakati ikiingia kwenye anga la dunia na baadhi ya vipande vyake vitaanguka ingawa haitegemewi kudhuru watu. naomba kueleweshwa, ni kwa nini wao(NASA) wanategemea kuwa itaungua. swali lingine, kwa kuwa huko kwenye anga za juu huwa wanasema kuwa hakuna gravitational force, hivyo vitu huwa vinaelea tu kwenye anga bila kuanguka kuja huku chini, sasa kwa nini satellite hiyo isibaki huko huko juu? ni kitu gani kinaivuta kurudi huku duniani?

Nafikiri wengine wameshajibu ...lakini niongezee kidogo kuwa gravitational force iko huko angani wakati wote ... na mwendo wa satellite kwenye orbit yake ni mjumuisho wa gravity, uzito wa chombo hicho na umbali toka duniani. Kuiweka satellite kwenye mzunguko wake unahitaji kuwepo kwa nguvu ya mvutano wa dunia ili izunguke dunia. Kama ikiwa nje ya mvutano wa gravity ya dunia ... itavutwa na sayari (escape velocity) au chochote kingine karibu chenye gravity yake... EITHER kikazunguke huko au kuangukia huko!! Kwa hiyo kunahitajika ujuzi wa kweli kabis kufanya chombo kuzunguka sayari fulani na isiwe sayari nyingine ..au chochote kingine!!
 
Natamani amos5 ianguke maeneo ya kwetu ili nipate kiPande cha solar maana nasikia huwa ni high voltage yaweza kuniondolea masaibu ya tanesco
 
since 2011 hadi Leo haijaanguka tu, basis bujibuji kaongea ukweli
 
Hivi dunia inazunguka hizo satellite na zenyewe zina zunguka au zimetulia sehemu moja?
Na kama imetulia sehemu moja inawezaje kufanya kazi muda wote?
 
Gravitation force ipo ulimwengu mzima, doesn't matter uko mbali ya sayari kiasi gani, sema unavozidi kua mbali ndivyo inavozidi kua ndogo, kwa hiyo kwenye satellite pia gravitation force ipo, satellite inavutana na dunia na bado inavutana na objects nyingine zote kwenye universe.

Satellite iliyopo angani siku zote hua inaanguka, ukiona satellite ambayo ipo sehemu moja kila siku usidhani kua ipo imesimama, pale hua inaanguka sema inaanguka kwa speed sawa na speed ya mzunguko wa dunia kwa hiyo inakua inaangukia upande kila siku.

Satellite kama hii unayosikia inakuja kuanguka duniani ni sababu imepoteza speed, manake centripetal force (nguvu inayovuta satellite towards earth) imezidi force inayolizungusha.

Natumaini umeelewa, kueleza kiswahili haya mambo hua ni mbinde, elimu ya ngeli hii noma sana.
 
kwa mujibu wa knowledge ndogo niliyonayo Sattelite huwa zina kuwa Designed to explode/Self destruct wakati life span yake inapoisha. Nilijifunza kuwa life span ya Sattellite huwa ni minimum of 15 years. Huwa kuna fuel tanks zinawekwa kwa satellite ili kuirun inapokuwa kule. hii ni Gesi ya hdrogen kama sijasahau then the solar powe is supplement.

Kwa hiyo ile fuel inapoisha huwa life ya Satellite inakuw inaelekea kuisha kwani not always Solar power ni sufficient ku generate required energy.
Kwa hiyo huwa kuna vilipuzi ambavyo huilipua auyomatically na mabaki yake huangukia duniani most hayadhuru binadamu.

Ni muda mrefu kidogo when I learnt this kama kuna michango zaidi tujifunze wote
 
Umri wa setelaiti ni miaka 15 kwa zile ambazo hurushwa juu zaidi ya kilometa 36,000 toka uso wa dunia. Kwa zile ambazo hulizunguka jua kwenye umbali huo huwa na umri wa miaka 12.

Kitu gani huifanya setelaiti ifikie ukomo wa umri? Setelaiti zina kifaa kiitwacho propellant (fueli) ambacho huifanya setelaiti ibaki kwenye orbiti yake. Kifaa hiki hufa wakati vifaa vingine vingali vinafanya kazi.

Setelaiti zile za umbali mkubwa zinapofikia ukomo wa umri husogezwa mbali zaidi toka uso wa dunia; huenda hata 2000 km. Eneo hilo huitwa kaburi la setelaiti (satellite graveyard). Aidha, setelaiti nyingi hulipuka zinapofika huko. Vipande vya setelaiti iliyolipuka huweza kuleta madhara makubwa kwa setelaiti nzima. Hivyo, husogezwa mbali ili ikalipukie huko.

Setelaiti zinazozunguka dunia chini ya umbali wa km 36,000 zinapokufa hulipuka zikidondoka. Na kila mwaka takribani setelaiti 12 hufa na huondoka katika orbiti zake.

Mbona hatuoni zikidondoka? Zile zizungukazo umbali wa zaidi ya km 36,000 hupelekwa kwenye kaburi la satelaiti. Hata zikilipuka na kusambalatika, ili mabaki yake yafike kwenye uso wa dunia huchukua miaka na miaka. Huweza kuchukua kuanzia karne moja hadi milenium moja.

Kwa setelaiti za chini. Hizi zinapolipuka vipande vyake huweza kuchukua miaka 25 au zaidi kufika duniani. Na mara zote vipande hivyo havijaleta madhara yoyote hadi sasa kwa hapa duniani. Vipande vingi vimekuwa vikidondoka katika uso wa dunia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom