Sassatel yavamiwa na majambazi

mkonowapaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
1,493
767
Kuna habari zilizothibitishwa kwamba kampuni ya simu inayokuja kwa kasi kwenye huduma ya internet imevamiwa jana usiku wa saa 4.

Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika ni kwamba gari ndogo aina ya Toyota Hiace ilifika ofisini hapo makao makuu Oysterbay ikiwa na vijana 20 waliovalia mavazi/jezi ya kampuni ya ulinzi ya Knight Support na kisha kuwahadaa walinzi waliokuwepo zamu kwamba waliagizwa kushusha mzigo hapo..

Kilichofuata ni walinzi hao kufungwa mikono kwa kamba na kuvamia ndani ofisi za finance, customer care na kufanikiwa kuondoka na sefu lililokuwa na fedha taslimu za mauzo haijafahamika ni kiasi gani... na simu za mkononi na laptops.... wanalaumiwa Knight Supports kitengo cha Emergency kwa kuchelewa kufika...

Poleni Sassatel!
 
Whom to trust now!
Thanx God hawakuumiza mtu, japo wanastahili adhabu kali!
 
Nimeongea na mdau mmoja huko ndani ya Sasatel akanihakikishia kuwa ni kweli hili jambo limetokea ili hawakuweza kuondoka na kiasi kikubwa cha fedha kwani makusanyo mengi yalikuwa yamefanywa kwa hundi na cash kiasi zilshakuwa banked!
 
Back
Top Bottom