Sasa unaweza kuifundisha Google Assistant kutamka majina kwenye simu yako

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Kama umekuwa mtumiaji mzuri wa huduma ya Google Assistant, utakuwa unafahamu ni kwa ainsi gani huduma hii ilivyorahisisha utafutaji kwenye simu yako. Ni rahisi kutafuta kuhusu hali ya hewa, matokeo ya mechi, mgahawa ulio jirani, nk., vyote kwa njia rahisi tu ya kuzungumza kwenye simu yako.

google-assistant.jpeg

Lakini Google imekutana na changamoto ya tofauti ya lugha na matamshi kutoka maeneo tofauti duniani. Hii imefanya Google Assistant kushindwa kuelewa kinachoulizwa, hasa pale unapoiamuru kumpigia mtu fulani.

Sasa, Google wamekuja na suluhu ya tatizo hilo katika sasisho la Google Assistant. Unaweza kuifundisha Google Assistant yako jinsi ya kutamka majina ya watu kama ulivyoyahifadhi katika simu yako ili iwe rahisi unapoiamuru kumpigia mtu huyo.

Sasisho hili jipya la Google Assistant inakuwezesha kurekodi sauti yako au au kuandika jinsi jina linavyotamkwa ili Google Assistant iweze kuelewa matamshi ya jina kwa jinsi unavyolitamka wewe mwenyewe.
Huu ni mwendelezo wa hatua ya Google ya kuboresha uelewa wa watumiaji wake na jinsi wanavyotafuta mambo mtandaoni, mpango ulioanza takriban miaka miwili iliyopita.

Tofauti na Alexa ya Apple inayoelewa lugha 8 tu, Google Assistant inaweza kutambua lugha 12 duniani, ikiwamo Kiholanzi, Kifaransa, Kihindi, Kiitalia, Kijapani, Kijerumani, Kiswidi, Kihispania na Kinorway. Lugha ya Kiswahili haipo katika orodha hiyo.

Video hii inakuelekeza jinsi ya kuifundisha Google Assistant kutamka jina kwenye simu yako.



Kwa sasa, huduma hii ya kuifundisha Google Assistant jinsi ya kutamka jina ipo kwa lugha ya Kiingereza tu, lakini kampuni hiyo inapanga kuongeza huduma hiyo kwa lugha zingine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom