Sasa umefika wakati serikali yetu kuchuka hatua madhubuti kukomesha mauwaji!!

Mtumishi Wetu

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
5,712
1,906
Wanajamvi bila shaka hamjambo, hili jambo la mauwaji ya viongozi wa kidini kweli linatisha!!!
Hata tukikataa ua kukubali hatua iliyofikiwa na mambo haya ni mbaya!

Hili swala tusiliangalie kwa misingi ya dini, bali hizi ni vurugu za ku disturbelise taifa letu lenye amani la TANZANIA!! Nadhani kuna watu wanaona wivu kwa nini tuko salama kiasi hicho, kwa kutumia watu wanye uelewa ndogo wa matokeo ya mambo watakayofanya.

Tukijifanya kunyamaza kimya mambo yanayotokea nchi za wengine yatahamia Tanzania!! Serikali iwe makini kudhibiti vitendo hivi vya kihalifu.

Tunaiomba serikali yetu inayotawala ifanye mambo yafutayo:-
1. Kupiga marufuku uenezaji wa chuki na machafuko kwa njia ya dini, iwe misikitini au makanisani kwa waumini( kupandikiza chuki kwa Watanzania).
2. Kupiga marufuku kufundisha mafunzo ya kijeshi iwe misikitini au makanisani, karate kungfu, mapanga yote hayo yanayolenga kuleta uvunjifu wa amani!1
3. Kupiga marufuku vyombo vya dini vinavyo hubiri na kueneza chuki iwe gazeti, redio, mitandao na vituo vya televisheni, wanyanganywe liseni na kufunguliwa mashitaka, ya kueneza chuki.
4. Kupiga marufuku mihadhara yenye marumbano ya dini au kashfa au kueneza chuki na kuvuruga amani ya nchi yetu!
5. Kwa matokeo haya hoja ipelekwe bungeni ili kila kitu kiwekwe wazi itafutwe suluhu ya kudumu!

Naomba tuchangie bila kuingiza udini kwa maslahi ya taifa letu na watoto wetu la Tanzania!!!
 
Kama hatua hazitachukuliwa sasa hivi mambo mabaya yanaweza kulikumba taifa letu!!!
 
Mkuu kwa kutimiza hizo marufuku na mandamano mengineyo utakuwa umewanyima haki ya msingi waabudu wa imani fulani hapa ncchini....
 
Mkuu hapa hatuangalii dini tunaangalia usalama wa nchi, tusipochuka hatua ya kukomesha hiyo mipango ya vurugu tutajutia maana gharama yake itakuwa kubwa!!!

Hawa watu wanaachiwa wanasambaza nyaraka kama hizi za uchochezi nchi hii Mungu wangu unatarajia tutafika wapi????
attachment.php
 
Mkuu hapa hatuangalii dini tunaangalia usalama wa nchi, tusipochuka hatua ya kukomesha hiyo mipango ya vurugu tutajutia maana gharama yake itakuwa kubwa!!!
Mkuu kuna kitu ambacho watanzania ama kwa unafiki ama kwa kukepwa mambo yenye ukweli mchungu wanashindwa kuyamudu na haitatokea kuyamudu...
Kiongozi wa dini anaposimama hadharani na kutoa tamko kwa wafuasi wake kuwa wauweni viongozi wa dini nyingine na baada ya muda viongozi wawili wanauwawa na mmoja kukoswa koswa unategemea nini?? Kwamba iundwe tume na timu ya majasusi wa kimataifa(say KGB, CIA labda na MOSSAD) kuja kuchunguza vyanzo na uchochezi wa mauaji?? Ili iwejee kwa kodi ya nani.Kwani hawawajui hawa wachochezi??

Nenda pale MANZESE au UBUNGO utakuta kanda za kukashifu dini za watu wengine na kuchochea chuki zinauzwa shilling BUKU MOJA..Na hili tuliundie tume na kuwaita CIA watusaidiea??

Vipi kuhusu RADIO IMAAN?? Vipi kuhusu JK na MAKAMBA kutumia udini kutafuta kura 2010?? Tunachogopa hapa ni nini??
 
Kuulwa kwa viongoz wa kdn tatzo n vp raia wa kawida wanapouliwa na kunyanyaswa ndan ya nalo tatzo serikal Inahtajka kufanya uamuzi ulio sahh kukomesha na kurekebsha hal ilyoko
 
Mkuu kuna kitu ambacho watanzania ama kwa unafiki ama kwa kukepwa mambo yenye ukweli mchungu wanashindwa kuyamudu na haitatokea kuyamudu...
Kiongozi wa dini anaposimama hadharani na kutoa tamko kwa wafuasi wake kuwa wauweni viongozi wa dini nyingine na baada ya muda viongozi wawili wanauwawa na mmoja kukoswa koswa unategemea nini?? Kwamba iundwe tume na timu ya majasusi wa kimataifa(say KGB, CIA labda na MOSSAD) kuja kuchunguza vyanzo na uchochezi wa mauaji?? Ili iwejee kwa kodi ya nani.Kwani hawawajui hawa wachochezi??

Nenda pale MANZESE au UBUNGO utakuta kanda za kukashifu dini za watu wengine na kuchochea chuki zinauzwa shilling BUKU MOJA..Na hili tuliundie tume na kuwaita CIA watusaidiea??

Vipi kuhusu RADIO IMAAN?? Vipi kuhusu JK na MAKAMBA kutumia udini kutafuta kura 2010?? Tunachogopa hapa ni nini??
Ndio maana nimesema hili jambo lipelekwe bungeni lijadiliwe ili hatua zichukuliwe, kama serilkali imeshindwa kuchukua hatua ya kukomesha hivi vitendo vya ukiukwaji wa haki, basi bunge liiwajibishe serikali kwa kuunga mkono matendo ya vurugu za kuuwa watu wasio na hatia kisingizio cha dini!!!
Bila shaka wabunge wetu makini kina Mhe Tundu Lisu wamesikia na wanaguswsa na hizi vurugu wachukue hatua!!!!
 
Mkuu unachekesha sana...BUNGE gani la kujadili haya mambo?? la NDUNGAI NA ANNE MAKINDA??
Kama hoja za maji UBUNGO, ELIMU na nyinginezo zinazimwa juu kwa juu hili unategemea litajadiliwa??

Ishu ya Ulimboka ilijadiliwa?? Vipi mgogoro wa MTWARA ulijadiliwa?? Vipi kuchomwa makanisa na vurugu za mbagala zilijadiliwa????

Au mkuu umesahau kuwa unaishi TANZANIA ya CHAMA TUKUFU cha kijani??
 
Kweli Mkuu lakini si unajua hadithi ya mfa maji, haishi kutapatapa??? Tupige kelele labda watajua kuwa tunahitaji hatua zichukuliwe!!!

Safi iko wazi na madai ni ya msingi yamewekwa hapa kama hutaki kuelewa huwezi kuazishwa
Mkuu swala tunalosema si dini yako na madai yake ila usalama wetu wewe mimi na watoto wetu, kwani wewe utaficha watoto na mkeo pangoni, wacha ushabiki usio na msingi, fikiria usalama wa taifa lako!!! Kama kuna madai ya haki peleka kule bungeni ua chama kiweze kudai sio kuuwa watu wasio na hatia, sera hiyo hana tija!!!!

Mkuu kuna kitu ambacho watanzania ama kwa unafiki ama kwa kukepwa mambo yenye ukweli mchungu wanashindwa kuyamudu na haitatokea kuyamudu...
Kiongozi wa dini anaposimama hadharani na kutoa tamko kwa wafuasi wake kuwa wauweni viongozi wa dini nyingine na baada ya muda viongozi wawili wanauwawa na mmoja kukoswa koswa unategemea nini?? Kwamba iundwe tume na timu ya majasusi wa kimataifa(say KGB, CIA labda na MOSSAD) kuja kuchunguza vyanzo na uchochezi wa mauaji?? Ili iwejee kwa kodi ya nani.Kwani hawawajui hawa wachochezi??

Nenda pale MANZESE au UBUNGO utakuta kanda za kukashifu dini za watu wengine na kuchochea chuki zinauzwa shilling BUKU MOJA..Na hili tuliundie tume na kuwaita CIA watusaidiea??

Vipi kuhusu RADIO IMAAN?? Vipi kuhusu JK na MAKAMBA kutumia udini kutafuta kura 2010?? Tunachogopa hapa ni nini??
Kibaya zaidi, yule anayehubiri na kulekeza kuuwaawa viongozi wa dini nyingine hakamatwi na naendelea raha mstarehe. Alafu mtu mwingine anidanganye kuwa serikali haihusiki wala haiwajui wauwaji. Nasikia kuna taasisi inaitwa usalama wa taifa. Hivi ipo? na kama ipo inafanya nini?
 
Nadhani kwa kila mtu mwenye kutafakari haya mambo kwa makini, anajua kabisa kiini cha hili tatizo ni JK na chama chake cha CCM. Tukumbuke kuwa Mnyika alitamka bungeni waziwazi kuwa tumefika hapa tulipo kutokana na udhaifu wa Kikwete! Wengi sana wakati ule, hawakumuelewa anamaanisha nini, hata baadhi ya vigogo wa CCM, akiwemo Lukuvi na Spika Makinda, walienda mbali zaidi na kumuita Mnyika kuwa ni kijana mdogo, aliyekosa adabu!!

Lakini sasa hebu tutafakari mtiririko wa matukio yafuatayo.Mwezi Novemba mwaka jana, Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Soraga, alimwagiwa tindikali kali, kwa kile kilichodaiwa anawasaliti waislamu wenzake na kuwakingia kifua wakristo!! Desemba, mwaka jana, Padri Mkande, alinusurika kifo, baada ya kupigwa risasi nje ya nyumba yake. Wiki iliyopita tumeshuhudia mchungaji wa kanisa, akiuliwa kule Geita, na sasa ndiyo linatokea tukio hili la kuuawa kwa Padri Mushi!!

Inajulikana wazi kuwa Rais amepewa madaraka makubwa sana kwenye Katiba ya sasa, akiwa Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote nchini kwa nia njema sana, ili avitumie vyombo vya ulinzi na usalama kwa usalama wa raia na mali zao, wakati nchi yetu inakabiliwa na tishio la kuvurugika kwa amani. Inajulikana wazi na kila mtu kuwa chokochoko hizi za udini, kwa kutumia vipeperushi na kanda za kukashifu dini nyingine hazikuanza jana wala juzi, bali zimekuwepo kwa muda mrefu. Sasa wakati hivyo vipeperushi vya akina Uamsho vinapeperushwa na kanda za kukashifu dini nyingine za akina ustaadh Ilunga, zinauzwa mitaani, ina maana intelejensia ya Jeshi la Polisi na umahiri wa usalama wa Taifa, ulikwenda likizo?! Au ndiyo tuseme Intelejensia ya Polisi wetu inaishia katika kuwasaka watu waliomwandikia Spika Anna Makinda, wakimshinikiza ajiuzulu wadhifa huo kwa kuonyesha upendeleo wa wazi kwa CCM wakati anaongoza vikao vya Bunge?!

Ndiyo maana nimetangulia kusema, wakati Mnyika aliposema nchi yetu imefika hapa kwa ajili ya udhaifu wa JK, wakati ule ni watu wachache sana walimuelewa anamaanisha nini, lakini naamini kwa sasa mamilioni ya watanzania watakuwa weshafahamu Mnyika alichokuwa akikisema kilikuwa ni nini na kwamba kina ukweli wa asilimia 100!!

Hebu tujiulize kwa upande mwingine, gazeti la Mwanahalisi ambalo lilikuwa mstari wa mbele kuandika habari za uchunguzi na kufichua maovu mbalimbali nchini, ukiwemo mkasa wa kutekwa na kuteswa kwa Dr Ulimboka. Gazeti hilo limefungiwa kwa muda usiojulikana, na Rais amenukuliwa na waandishi wa habari kuwa kamwe gazeti hilo hatalifungulia! Jambo linalothibitisha bila shaka yoyote kuwa ufungiaji wa gazeti hilo ulikuwa na mkono wake JK mwenyewe, kwa kuwa lilimtaja kwa jina mtumishi wa Ikulu, Ramadhan Ighondu kuwa ni mtuhumiwa na.1 wa kadhia ya kutekwa nyara kwa Dr Ulimboka!

Tumemsikia Salva Rweyemamu akiongea na waandishi wa habari akieleza kuwa Rais amesikitishwa sana na mauaji ya Padri kule Zanzibar. Lakini watanzania tunapaswa tutofautishe kauli ya mtu ya kusema na vitendo vyake. Mimi naweza kudiriki kusema kuwa kauli za JK mara nyingi zimejaa usanii na uigizaji wa hali ya juu, kwa kuwa yeye kama mkuu wa nchi ambaye taarifa zozote zinazohusu hatari ya uvunjifu wa amani, vyombo vyake vya ulinzi na usalama vinamfikishia yeye taarifa kabla ya mtu mwingine yeyote. Ni kwa nini wakati wote ameshindwa kuchukua hatua? Hivi wananchi tukiamini kuwa machafuko haya ya kidini yanashabikiwa na CCM ili watangaze hali ya hatari, ili waufute uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ambao vyombo vyao vya dola vya ulinzi na usalama, vimeshawaambia kuwa kutokana na wananchi wengi kukosa imani na CCM, uwezezekano wa CCM kushinda kwenye uchaguzi 2015 ni sawa na uwezekano wa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano!na kwa kuwa JK alishawahakikishia kuwa ni lazima nchi ataikabidhi kwa CCM mwaka 2015, anachotafuta sasa ni kutangaza State of Emergency, ambapo nchi itaendelea kutawaliwa na CCM bila kufanyika uchaguzi wowote kwa miaka mingi ijayo ili wanaCCM wasimuone kuwa aliwafanyia usanii!! Wananchi tunalazimika kumwomba sana Mungu ili atuepushe na haya majanga wanayotaka kuyaleta wanamagamba ndani ya nchi yetu!!
 
Mkuu yote uliyo andika ni sawa kabisa hatua ya kuchukua ni hoja ya kuilazimisha serikali kuchukulia hatua woote wenye kuchochea vurugu na mauwaji nchi!!!Tena tunahitaji external support maana financiers wako nje ya nchi, wanajulikana!There is a price tag for every christian leader killed! Kama hawataki kuchukua hatua basi ni bora watu wapenda amani bila kujali dini zetu tukaandamana woote ili wajue tuko serious na usalama wa nchi yetu!!!

Kibaya zaidi, yule anayehubiri na kulekeza kuuwaawa viongozi wa dini nyingine hakamatwi na naendelea raha mstarehe. Alafu mtu mwingine anidanganye kuwa serikali haihusiki wala haiwajui wauwaji. Nasikia kuna taasisi inaitwa usalama wa taifa. Hivi ipo? na kama ipo inafanya nini?
Mkuu kuna vikundi na taasisi zinajulikana kabisa zinatoa msaada ili kusababisha vurugu, ujue hawa watu wanapouwa wakuu wa dini sio bure wanalipwa!!Hebu angalia hii post ya jamii intelligence iliyorushwa na mdau mmoja wapo:-
(Samahani nime quote post ya mdau kukazia ukweli wa yanayotokea nchini kwetu)
[h=2] Exremism on the rise in Zanzibar-funded from Saudia and Dubai! [/h]
Wakuu tumekuwa tukujiuliza haya matukio yasiyo ya Kitanzania yatoka wapi?
Tunajua vyombo vetu vya usalama vinaweza kuwa na habari hizi(ambazo hata kwenye mtandao zipo), lakini kwa nini hatua za wazi wazi hazichukuliwi ndio swali kubwa.

Watu wanaoua na kuchoma moto nyumba za ibada wanafadhiliwa toka Saudi Arabia na Dubai, hilo ni wazi. Hebu cheki hii makala toka website ya Sharia Finance Watch:

“Extremism” on the Rise in Zanzibar–Thanks to Saudi Money and Islamic Charities

On December 31, 2012 · In Abu Dhabi, Al Qaeda, Dubai, Islam, Islamic charities, Islamic Law, Islamic schools, Islamization, Jihad, Jihadist Groups/Individuals, madrassas, Salafism, Saudi Arabia, Shariah Law, Sudan, Tanzania, Wahhabism, Zakat, Zanzibar

The Financial Times has an important article about the influx of Salafi Islam in the island region of Tanzania known as Zanzibar.
The article doesn’t draw any of the correct conclusions about what is happening there, but it contains enough clues to build a picture.
For folks who don’t remember, Tanzania is one of the East African nations where the US embassy was bombed by Al Qaeda in August of 1998.
Zanzibar is an island off Tanzania’s coast in the Indian Ocean. It has been somewhat of a tourist destination–at least up to now. Up to now because Salafi Islam is making its presence felt in Zanzibar.
That manifests itself in several ways, but here’s one from the opening of the FT.com article that is particularly intriguing:
Under the peach arches of Al-Noor charitable agency for the needy just outside Stone Town in Zanzibar, a 24-hour Islamic radio station broadcasts religious guidance.
Female tourists should wear headscarves and cover their knees, says Mohamed Suleiman Ali, director of Radio Al-Noor, echoing the opinions voiced on radio. “It’s too early to fight for an Islamic state because there are several stages to that, but a lot of things are being done contrary to the teachings of Islam,” he says. “There’s no social responsibility; the government keeps producing more [social] freedom.”
This is remarkable in that it illustrates vividly how “charities” in the Islamic world aren’t like charities elsewhere. They get involved in all sorts of activities that have nothing to do with charity at all. Al Noor is no exception:

Al Noor Charity Agency - Coming Soon!Here are some highlights from Al Noor’s own web site:

Over the years our organisation has built numerous islamic centres, masjids, madrasas (Qur’an schools), and waterwells.
Keep in mind that madrasas are notorious in other places, particularly Pakistan, for being incubators of Jihad.

We also distribute Zakat…
Once again, zakat is a major concern for Western Civilization because it can be and is in fact used to fund Jihad. We don’t know that Al Noor is distributing zakat for Jihad in Zanzibar, but other Islamic charities have and Jihad is definitely becoming a problem in Zanzibar.

Al Noor operates with a vision to promote the islamic way of life…
This of course explains the statement above admonishing tourists to dress in a modest fashion in compliance with Shariah.

Al Noor is simply a tool of Islamic imperialism. They claim they are just helping the needy but promoting Shariah has nothing to do with helping the needy.

How did Al Noor come to be in Zanzibar? Money from Saudi Arabia and Dubai started showing up and the effect has been predictable. From FT.com:

Al-Noor charity, set up four years ago with money from private donors in Dubai and Saudi Arabia, is among a clutch of new foreign-funded religious institutions to increase its investment on the island. As well as the radio, it has established a mosque, internet rooms and a nationwide network of madrassas. It plans to build more, and every year pays for students and teachers alike to study in Sudan, Abu Dhabi and Saudi Arabia.
Academics estimate that Saudi Arabia – where Wahhabi Islam is practised – alone spends $1m a year on Islamic institutions in Zanzibar.
Sending students from Zanzibar to study in Saudi Arabia, genocidal, terrorist-sponsoring Sudan and Abu Dhabi is essentially a means of entrenching Wahhabi Islam in Zanzibar.
And even Muslims in Zanzibar know it:
“Wahhabi madrasas are just starting – they are now many and Saudi funds are spreading their work – they have nice buildings, they are well off and well organised; they preach and convince the parents to come there, so the effect of the madrassa is very powerful,” says Idrissa Ahmad Khamis, a teacher who is from the Sufi tradition, a mystical form of Islam opposed by more literalist Wahhabis or Salafists.
Al-Qaeda and other terrorist organisations draw their thinking from Wahhabism. “We’re not happy with other sects like [Sunni hardline] Wahhabi – people who go to countries like Saudi Arabia; when they come back they want to change everything,” he says.
None of this is new or surprising. In fact, this system was detailed in the 9/11 Commission Report years ago. Yet it continues and no one is lifting a finger to stop it.Saudi Arabia is our “ally” so military action is out of the question. Don’t expect the State Department to even mention it however. The list of former and retired State Department diplomats who are now on retainer with the Kingdom of Saudi Arabia is long.
If this is what is happening in Zanzibar…where else is it happening?
Extremism on the rise in Zanzibar - FT.com"

Wakuu nimeweka highlights za red kama msisitizo, na narudia tena:

None of this is new or surprising. In fact, this system was detailed in the 9/11 Commission Report years ago. Yet it continues and no one is lifting a finger to stop it.Na sasa viongozi wa dini ya Kikristo wanauwawa makanisa yanachomwa, tuchukue hatua madhubuti kabla hali haijawa mbaya zaidi.

You and Nyenyere like this.

Inatisha. Serikali inaunga mkono vikundi hivi bila shaka! Kama sivyo, wangelichukua hatua!
 
Kauli iyo imeshasemwa sana na hakuna kinachofanyika.
Wananchi ndio tumeipaserikali ridhaa ya kutuongoza, sasa kama serikali hii ya ccm imeshindwa tena kwa maksudi hatuna budi kuitupilia mbali na kuipa ridhaa serikali mpya yenye tija ya kusimamia usalama wetu pamoja na uhuru wa kuabudu.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom