sasa umefika wakati muafaka wa kuunda serkali moja tz! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

sasa umefika wakati muafaka wa kuunda serkali moja tz!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mgen, Dec 24, 2010.

 1. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,192
  Likes Received: 1,914
  Trophy Points: 280
  Kila mwenye imani aombe Dua kwa imani yake ili MWENYEZI MUNGU ATUANGAZIE BAYANA TUONE HILI BILA UNAFIKI WALA UBINAFSI AU UMASLAHI WA PANDE MOJA YA MUUNGANO; Tulikubaliana tuue mama zetu ili wote tuwe wakiwa Mimi nikamuua mama yangu (TANGANYIKA); Nikaja gundua mama yake hakumuua! Bali kamficha (Zanzibar); Nilipoliona hilo nikampa ushauri mwenzangu Kwamba nimfufue mama yangu au nawe umuue mama yako Ili wote tuwe sawa. Jibu nililo pata ni la uchungu sana ambalo halivumiliki kibinadamu. Kwamba aliye kufa kafa hakuna kumfufua; Wala Usimkumbuke marufuku Hata kwa jina Na Mama yangu aliye hai Yuko hai hafi mtu Hapa. Kweli inasikitisha sana KILICHO baki leo Kama NI UCHUMBA tumechunguzana muda mrefu kama dosari tumeziona kilicho baki ni KUFUNGA NDOA AU KUACHANA KWISHA. ZAIDI YA HAYO MAWILI NI LONGOLONGO Watanganyika TUJITAMBUE!
   
 2. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,198
  Trophy Points: 280
  Katiba mpya itakuja na serikali moja.
   
 3. AIZAK

  AIZAK Member

  #3
  Dec 24, 2010
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  1 Corinthians 1:10

  10 I appeal to you, brothers, in the name of our Lord Jesus Christ, that all of you agree with one another so that there may be no divisions among you and that you may be perfectly united in mind and thought. mungu na atutangulie.
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Uyo 1 Corinthians 1:10 ni nani au nini ?
   
 5. AIZAK

  AIZAK Member

  #5
  Dec 24, 2010
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hii ni barua ya paul kwa wakorintho.
   
 6. N

  Nonda JF-Expert Member

  #6
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Kitu gani au jambo gani linalofanya kuwa sasa ni wakati muafaka wa kuwa na serikali moja?

  Mimi nafikiri ni wakati muafaka kuitisha kura ya maoni juu ya muungano na muundo wake.

  Katika Tanzania hii, suala la muungano wa Tanzania limekuwa la kichama.

  CCM walikuwa na sera ya serikali mbili, sasa hivi imebadilika kuwa serikali mbili kuelekea moja.

  CHADEMA wana sera ya serikali tatu.

  CUF nao wana sera ya serikali tatu

  Mgen ana sera ya serikali moja.

  Buchanan ana sera ya serikali tatu

  Rev. Mtikila na G55 walitaka serikali ya Tanganyika ndani ya muungano.

  Ili kutegua kitendawili hiki ni bora kuitishwa kura ya maoni itakayowashirikisha wananchi moja kwa moja kuamua juu ya muungano kama uwepo au uvunjwe, kama utakuwepo, pia wapige kura aina ya mfumo,muundo wa muungano huo. Aidha uendelee huu wa serikali mbili, serikali moja au tatu.

  Ikitokea theluthi mbili ya kila upande wataamua katika hayo mapendekezo basi hapo iamuliwe hilo lililochaguliwa litendeke.

  Vyenginevyo tunayachelewesha tu matatizo na migongano ambayo lazima yatatokea siku za mbele.

  Sijui ni kwa sababu gani CCM na serikali zake kusita kuendeleza ujasiri wake wa azimio la musoma la kura ya maoni kwa Zanzibar kama wanataka GNU.
  Kwa nini hawataki kufanya kura ya maoni kwa watanzania kwa Muungano na muundo wake?
   
Loading...