Sasa ukionyesha udhaifu katika utendaji kazi unabadilishiwa kituo kingine, ndio kujivua Gamba.ARUSHA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa ukionyesha udhaifu katika utendaji kazi unabadilishiwa kituo kingine, ndio kujivua Gamba.ARUSHA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fasta fasta, May 17, 2011.

 1. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Mwanasheria ahamishwa kimya kimya Send to a friend
  Arusha
  UTAFITI umebaini kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Arusha, mkoani hapa imemuhamisha kimya kimya aliyekuwa
  Mwanasheria Mkuu wa Manispaa hiyo,Paul Mugasha.Kuhamishwa kwa Mugasha ambaye pia anadaiwa kuhusika katika usimamizi mbovu wa mikataba ndani ya manispaa hiyo hususani ile ya kutoa zabuni kwa kampuni mbalimbali tayari kumezua minong’ono kwa baadhi ya wakazi wa Arusha, wakiwemo wanasiasa.

  Vyanzo vya habari vimeeleza kuwa Mugasha amehamishiwa katika Halmashauri ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro huku nafasi yake ikichukuliwa na Allen Ndomba aliyetokea mkoani Mbeya.

  Vyanzo hivyo vya habari vimedai kuwa uhamisho wa mwanasheria huyo ni moja ya mikakati iliyowekwa na
  uongozi wa manispaa hiyo kama njia ya kuzima tuhuma za ufisadi zinazoikabili manispaa hiyo.

  Taarifa hizo zimeenda mbali zaidi na kudai kwamba uhamisho wa Mugasha umekuja wakati kamati ya hesabu za
  serikali za mitaa iliyopo chini ya mwenyekiti wake, Augustino Mrema ikitarajiwa kwenda katika
  Manispaa ya Arusha hivi karibuni kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa mahesabu mbalimbali.

  Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Estomi Chang’a alipotafutwa kwa njia ya simu juzi kwa lengo la kuthibitisha madai hayo alipokea simu na kujibu kwa mbwa yupo kwenye kikao na kusema kwamba Mugasha amehamishiwa wilayani Mwanga .

  Chang’a alipopigiwa simu kwa mara ya pili kwa ajili ya kutoa ufafanuzi kuhusu mwanasheria huyo kuhusika na usimamizi mbuvu wa mikataba, alisema uhamisho wa Mugasha ni wa kawaida, lakini hakutaka kuzungumzia suala la usimamizi mbovu wa mikataba ya manispaa hiyo.

  Mugasha alisema tayari ameripoti wilayani humo tangu Aprili 27, mwaka huu, lakini alikataa kuzungumzia
  suala la usimamizi mbovu wa mikataba na baadaye alipopigiwa tena alikata simu.
   
 2. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Sasa mtu kama huyu serikali inamlinda ili aendelee kufilisi taifa letu.
   
 3. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,079
  Likes Received: 877
  Trophy Points: 280
  kama vile mabailiko ya mawaziri eg mh wasira............
   
 4. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Sasa kama sera ya kujivua gamba haijaweza kufanikiwa nani atakayeweza kuwashughulikia watendaji hawa fisadi wa halmashauri na manispaa zetu? Hivi tuwafanyaje hawa wanaofanya maisha ya watanzania yawe magumu? Kwa nini CAG anapokagua halmashauri na manispaa zetu halafu zinaqualify wahusika wasichukuliwe hatua kali? Mi Namlaumu huyu mkuu Pinda, yeye ndiyo anatakiwa kumshughulikia huyu waziri wa TAMISEMI, NAE awashughulikie watendaji wake. ACHA UPOLE MZEE WETU PINDA MTOTO WA MKULIMA. FUKUZA MAFISADI, USHAIDI CAG ANAO
   
 5. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Kama serikali imeona njia hii ya kujivua gamba ndio mbadala, inabidi madiwani watusaidie kushinikiza hawa watu wapunguziwe madaraka au waondolewe sio kuhamishwa kwa sababu ni kuendeleza uozo wao na utaendelea kuambukiza kwa wengine. Madiwani ndio wenye meno ya kuondoa hivi visiki vinavyofichwa fichwa tumechoka.
   
 6. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #6
  May 17, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Mungai alipoharibu wizara ya Elimu....
  Na Mchapa kazi alipofanya Vizuri wizara ya ujenzi/Miundombinu.......akahamishiwa wizara ya Vitoweo!
  Huo ndo Mtindo
   
 7. d

  dotto JF-Expert Member

  #7
  May 17, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Like Mrindoko!!! style.
   
Loading...