dikteta2020
JF-Expert Member
- Aug 14, 2018
- 595
- 3,990
Magufuli akiwa na kampeni wanachapisha picha kubwa ya kampeni zake kwa juu kisha chini wanaweka vipicha vidogo vya wapinzani. Magufuli akipumzika kampeni hawaweki picha ya mgombea anayetoa upinzani mkubwa kwake wala habari zake hazipewi kabisa kipaumbele.
Nyie wahariri, jana na leo Tundu Lissu alikuwa Geita na wote hakuna aliyethubutu kuchapisha habari zake kama habari kubwa wala kuweka picha ya mkutano wake mbele! Aibu kwenu na uhuru wenu. Yani kwa siku mbili mfululizo habari ya Msajili na ACT ndiyo habari kubwa.
Sasa tumeshawagundua kuwa Hassan Abbas amewapa maagizo maalum. Tutaanzisha harakati maalum kwa ajili yenu maana inaonekana dhahiri mumeuza uhuru wenu!
Aibu! Aibu! Aibu!
Hatujawahi kushuhudia ushenzi huu hapo kabla!