Binti Maria
Senior Member
- Jun 26, 2007
- 158
- 33
Ok, wandugu. Mimi naona hawa CCM tumeshawazodoa vya kutosha na kuna kila dalili kwamba tunayowaambia yanaingilia huku yanatokea kule. Ni wazi pia kwamba kila mwananchi sasa anajua kwamba hawa CCM hawatabadilika hadi watakapobadilishwa. Hata hivyo ukweli ni kwamba wananchi hawataibadili CCM kwa sababu inafanya makosa. Pamoja na makosa haya, lazima patokee wa kuchukuwa nafasi yao.
Kwa upande wangu naona kwamba upinzani tayari wameshakuwa tayari kutawala. Wana sifa zote kuanzia mawazo mazuri-ambayo ndio msingi wa siasa-hadi uadilifu. Yaani, they are both effective and ethical, vitu ambavyo CCM vyote wameshavipoteza. Sasa tatizo la upinzani linakuja nalo ni wao kusambaa huku na huko huku wakijua kwamba wapo wachache. Ni kwa sababu hii naleta hoja kwamba tuanze mapema kuwabana hawa ili wajikusanye wakae pamoja tayari kwa mapambano ya 2010. Katika kufanya hili ni wazi kwamba wapo watakaopoteza na wapo watakaopata. Lakini ni wazi kwamba taifa letu litapona.
Naleta mapendekezo yafuatayo:
i) Wapinzani lazima waikamate Dar. Lazima katika uchaguzi wa 2010 utemi wa CCM Dar ukomeshwe kabisa. Sababu moja ya wapinzani kushindwa kukamata Dar ni ukweli kwamba huwa wanaweka wagombea wachovu. Sasa ili kuondoa hili napendekeza kwamba big shots wote katika uchaguzi wa 2010 wagombee Dar. Napendekeza wajipange kama ifuatavyo:
a) Kawe: asimame Freeman Mbowe
b) Ubungo asimame: Dr Sengodo Mvungi
c) Temeke au Ilala: asimame Profesa Ibrahimu Lipumba
d) Kinondoni: asimame: James Mbatia
e) Kigamboni- watafute
Hii ina maana kwamba lazima wasimamishe mgombea mmoja wa urais ambaye ni, nani tena zaidi ya, Dr Wilbroad Slaa.
Nyie mnasemaje sasa na mawazo haya?