Sasa tutegemee rushwa ya kutisha kwenye uchaguzi mkuu wa 2015

Easyway

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
2,606
3,702
Utoaji mkubwa wa rushwa kwenye uchaguzi wa CCM kuanzia wilayani,mikoani na sasa kwenye ngazi ya taifa hususani kwenye UWT na UVCCM si jambo la kificho na bahati mbaya hakuna wa kudhibiti rushwa hapa nchini,taasisi ambayo inatakiwa kudhibiti rushwa ilishakufa siku nyingi,makamu wa rais analalamika,rais naye analalamika,rais anakemea rushwa hachukui hatua yoyote.

Rushwa ambayo imebakia ni kwenye uchaguzi wa jumuiya ya wazazi ya CCM, nafikiri nayo wajumbe wanaisubiri kwa hamu!,na tutegemee kiongozi atakayefungua mkutano wao naye kukemea rushwa ni mwendo wa kukemea tu hakuna kuchukua hatua.

Anayetoa hizo fedha anafahamika na mawaziri wa Kikwete sasa wamekuwa mawakala wa kugawa fedha za rushwa , hakuna wa kuchunguza tuhuma hizi wala wa kuchukua hatua, ni upepo tu utapita.

Kwa jinsi rushwa ilivyo tawala na hakuna wa kuidhibiti basi uchaguzi mkuu wa 2015 utavunja rekodi ya matumizi makubwa ya rushwa kwa sababu CCM imeacha watoa rushwa watambe na washinde kwenye chaguzi zake.

Sasa tumekuwa taifa la rushwa la Afrika mashariki.
 
:target:SHAME UP ON CCM. KAMANDA MNYIKA NA WENZAKO HARAKA ANDIKEN HOJA BINAFSI YA KUIFUTILIA MBALI TAKUKURU aka TAKOKURU kwan sasa ni dhahili kuwa taasis hiyo ambayo inatumia bure kodi za wananchi ipo kwa ajili kuilinda ccm ambayo kwa sasa hailindiki tena. pumbavu zao.
 
Kuna yule mtu aliwaambia Watanzania kua Kikwete ni chaguo kutoka kwa Mungu! Huyu bwana anatakiwa ashikwe na awekwe pale Mnazi mmoja na apigwe Mawe mpaka afe!
 
Inawezekana alikuwa sahihi pia, wewe unadhani alimaanisha MUNGU yupi,inawezekana MUNGU wake yeye ni tofauti na wako
 
ni kweli,dalili ya mvua ni mawingu,kama viongozi wa chama wote mpaka wajumbe wamepita kwa rushwa,mipango yao yote itakuwa ni kujiandaa kwa aajili ya rushwa za kuwahadaa wananchi.
uchaguzi uliopita jimbo ninalotoka mie mbunge aliyeshinda alikuwa aknunua wapiga kura kwa 2000 au kiloba.sijui uchaguzi ujao itakuwaje.
 
Mwenyekiti wao ni sawa na sikio lisilosikia dawa! anakumbuka shuka huku kumeshakucha eti anakemea rushwa ndani ya chama chake huku mtoto wake ndio kinara wa mchezo mchafu pale Dodoma nani asiyejua?
 
:target:SHAME UP ON CCM. KAMANDA MNYIKA NA WENZAKO HARAKA ANDIKEN HOJA BINAFSI YA KUIFUTILIA MBALI TAKUKURU aka TAKOKURU kwan sasa ni dhahili kuwa taasis hiyo ambayo inatumia bure kodi za wananchi ipo kwa ajili kuilinda ccm ambayo kwa sasa hailindiki tena. pumbavu zao.
Hii na ile FIU zinatakiwa kuwa idara tu ndani ya TISS. Sasa hivi ni uhuni mtupu.
 
Unanikumbusha kitu kinaitwa derivative, vijana wa CCM ni derivative ya wazee wao, usitegemee juice ya chungwa iwe na harufu tofauti na chungwa lenyewe. Baba zao wameingia madrakani kwa kuiba pesa, kuhonga, kofia na khanga na wanajisifia wakiwa kwenye dining table, kwa hiyo watoto wao wanaona kumbe hii ndo style yenyewe. Bahati mbaya siku hizi vijana wanaochipukia they don't know the right and wrong as a result na wenyewe wamekuwa kama baba zao.
 
Nahisi watafilisika kabla ya 2015.

Mkuu kumbuka hao jamaa (CCM) ndio wenye Hazina ya nchi hivyo endapo watafilisika kama "unavyohisi" maanake automatically nchi itakuwa imefilisika. Hilo ni janga la kitaifa tusiombee litokee.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Unanikumbusha kitu kinaitwa derivative, vijana wa CCM ni derivative ya wazee wao, usitegemee juice ya chungwa iwe na harufu tofauti na chungwa lenyewe. Baba zao wameingia madrakani kwa kuiba pesa, kuhonga, kofia na khanga na wanajisifia wakiwa kwenye dining table, kwa hiyo watoto wao wanaona kumbe hii ndo style yenyewe. Bahati mbaya siku hizi vijana wanaochipukia they don't know the right and wrong as a result na wenyewe wamekuwa kama baba zao.
serpent

Hapo kwenye red; inaweza pia kuwa offspring kama hivi: serpent's offspring is also a serpent; yaani, kilichozaliwa na nyoka ni nyoka.
 
Kuna yule mtu aliwaambia Watanzania kua Kikwete ni chaguo kutoka kwa Mungu! Huyu bwana anatakiwa ashikwe na awekwe pale Mnazi mmoja na apigwe Mawe mpaka afe!
Kwa jinsi alivyoachia chama chake kisambaratike, nashiwishika kuamini kuwa huyu kweli tuliletewa na Mungu ili 2015 hawa wezi wenzake wasipate nafasi ya kututawala tena.
 
Nahisi watafilisika kabla ya 2015.

Watafilisikaje wakati wewe unaendelea kutoa kodi? Kwani hizo rushwa zinatoka wapi mkuu? Ni pesa zako za kodi....Gone is my beutiful country but I am in a fight to claim it back....
 
Soon wataanzisha "wakala wa kuratibu na kusimamia Rushwa CCM"
 
Kukemea maovu style ya Kikwete hauwezi badilisha chochote. Tatizo ni kuzoea kusoma kila uapotaka kuhutubia au kuelekeza. Hutuba ni kusoma tu, wala huwezi kuonyesha msisitizo wa zati ktk kusoma ujumbe. Anakemea rushwa kama vile mchunganji anawaasa watu waache kuvunja amri ya sita! Wee acha tu.
 
Kuna yule mtu aliwaambia Watanzania kua Kikwete ni chaguo kutoka kwa Mungu! Huyu bwana anatakiwa ashikwe na awekwe pale Mnazi mmoja na apigwe Mawe mpaka afe!

Sasa usichiamini km JK ni chaguo la Mungu ni kipi ? Maandiko yanasema kila mamlaka yanatoka kwa Mungu

Ndio najua kila mamlaka yanatoka kwa Mungu! Unataka kuniambia kua hili la Raisi wako anakotupeleka ni mamlaka kutoka kwa Mungu??
 
Back
Top Bottom