Sasa tunataka Tuone Maendeleo Fungate limeisha. Rais umeshaongea sana anza kutenda. Haya tumeshayasikia sana

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
1,694
3,982
Magufuli alishafariki na mabaya yake na mazuri yake. Sasa tupige kazi. Kazi ipi hiyo? Kazi iendelee ipi? Ya kuibia wananchi? Ipi? Ya kupeana vyeo kwa kujuana?ipi?

Mi sijui. Ila kazi iendelee vijembe havitatusaidia kitu. Marehemu hayupo tena nasi. Hana la kujitetea. Na hatuwezi pata umaarufu kwa kuendelea kutembelea nyota yake.

Nlikuwa napingana na Magufuli kwenye mambo mengi. Alipokuwa niliyazika naye ....sasa nasonga mbele. Serikali ya sasa ikosoe yale mambo mabaya kwa kutenda mema hii style ya kichovu ya kila siku tunaibua la kujisema awamu yetu iliyopita haitusaidii.

Maana ni kama tumeanza kukosa content kwenye hotuba. Ndo maana wengine tulipendekeza yawepo maridhiano ya dhati kabisa. Watu wakusanyike waombane na kuombwa msamaha kisha tuanze upya kwa miguu misafi.

Huwezi jikosha kwa kuchagua yake ya kunawa na yapi ya kumwagia wenzio. Watu waridhiane na wakubali kubadilika kwa kuunda Katiba ambayo haitarudisha tawala zote zilizopita. Italeta tawala mpya kwa misingi mipya. Otherwise tutakuwa tunapiga porojo na kujikosha baada ya kuona tumeshapoteza mvuto.

NITASEMA KWELI DAIMA. FITNA KWANGU MWIKO.
 
Halafu wanaoinanga awamu iliyopita nao walikuwa sehemu ya awamu hiyo tena kwa nafasi za juu kabisa.

Sasa sijui wanatuona kama hatuna kumbukumbu hiyo??
 
Halafu wanaoinanga awamu iliyopita nao walikuwa sehemu ya awamu hiyo tena kwa nafasi za juu kabisa.

Sasa sijui wanatuona kama hatuna kumbukumbu hiyo??
Wanafiki sana,alafu bado kuna watu wanawaona wa maana.
kama wangeshindwa kumkosoa basi wangejiuzuru angalau kuonyesha kutoridhishwa na uongozi wa serikali iliyopita.
 
Viatu vimewazidi..wanaona wivu..hawawezi kazi..wamebakiza chuki.

Legacy inawatesa sana..

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom