Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,999
Ndugu Mwapachu ni mjumbe wa Bodi ya Acacia ambaye kimkakati hutumika kufanya Lobbying katika serikali ya Tanzania pale mambo yanapokuwa magumu na si kuwa labda michango yake kwenye bodi ina 'akili' sana.
Mtakumbuka jinsi alivyoweweseka kipindia cha kampeni,kuanzia kura za maoni ndani ya CCM. na ni mmoja wa wanamikakati wa Ndg.Edward aliyechukizwa hadharani kiasi cha kuondoka CCm kwa mbwembwe za hali ya juu. Naam, alijua kabisa sasa uwezo wake wa ku-lobby sasa umekwisha na upo ukingozi kama si Edward atakuwepo Ikulu ya Magogoni.
Kama mtakumbuka vema muda mfupi baada ya uchaguzi kwisha na swahiba yake Edward kuanguka alirejea CCM kwa 'kuinunua' kadi yake ya uanachama kwa shilingi milioni moja katika tawi la Mikocheni 'A', huku akisema waziwazi ameamua kurejea CCM ili biashara zake na rafiki zake zisikwame.
Naam, sasa yupo ndani ya Acacia, kumbe hawa ndio marafiki zake.