Sasa tujadiri kwa kina swala la ardhi ya arumeru mashariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa tujadiri kwa kina swala la ardhi ya arumeru mashariki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sangarara, Apr 3, 2012.

 1. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Kampeni za ubunge jimbo la Arumeru mashariki lilikugubikwa na swala la Ardhi kuwa mikononi ama mwa wachache ama wageni, swala la kurudisha Ardhi kwa wazawa lilitumiwa karibia na kila mgombea mpaka wa SAU katika kujinadi.

  Nakumbuka kuna mgombea mmoja alikuwa anatoa kauli zinazomaanisha kwamba kuna kamfumo fulani kama kawakati wa ukoloni pale arumeru, kwamba watanzania wanafanya kazi kwenye mashamba ya wageni huku wao binafsi wakiwa hawana ardhi japo ya kulima chakula kwa matumizi ya familia zao.

  Naomba wenye uelewa mzuri na tatizo la Arumeru sasa watujuze vizuri bila mivutano ya itikadi za kisiasa kuhusu Jambo hili, sababu nahisi kama umiliki wa ardhi pande zile uko kinyume na sheria zetu za kumiliki ardhi.

  Maswali ya Msingi
  Arumeru Mashariki ina ukubwa kiasi gani?
  Arumeru mashariki ina wakazi kiasi gani?
  ni asilimia ngapi ni wageni na ngapi ni wazawa?
  Asilimia ngapi ya wakazi wa arumeru wanamiliki ardhi? waliipate ardhi hiyo?
  ardhi ya arumeru inatumikaje?
  Je sheria ya Umiliki ardhi inazingatiwa?
  Je utu wa Mtanzania unazingatiwa?
  n.k


  Swali lingine, ni wageni wangapi wameingia Tanzania na kwenda kujichimbia vijijini? mimi najua hakuna wawekezaji kutoka nje kwenye kilimo? Je Serikali imechukua hatua gani katika kuhakikisha haki za msingi za wazawa hazigandamizwi na maguvu ya kiuchumi ya wageni vijiji? au ndio serikali sio sikivu na haiko kwa ajili ya maslahi ya watanzania?
   
Loading...