Sasa siyo siri serikali ya Kikwete imefulia na inakaribia ku-collapse!

kuna Almashauri juzi tu imepitisha bajeti ya sherehe za kuukaribisha mwaka 2011 wakati mwaka wenyewe umeshazeeka, kwahiyo sishangai serikali kufuria ina matumizi ya hovyo hovyo.

itaje hiyo halmashauri hakuna kumung'unya maneno hapa.
 
suala la serikali kutokuwa na fedha liko wazi, hata ofisini kwetu chai kwa sasa hakuna, na hata mambo mengine yamefutwa, vinafanyika vitu vya lazima tu.

Nyinyi ndiyo munaolalamika serikali inatumia fedha nyingi kwa chai za ofisini. Leo zimekatwa munalalamika hakuna chai, hebu amueni sasa ifanye nini maana kila upande ni lawama.

Na kwa kweli huko serikalini vitu vingi viko inflated bila ya kiasi - gharama za kila kitu ziko juu sana kuliko kawaida ili watu wapate ka percent kao hapo. Leo hivyo vitu vikianza kukatwa basi na maneno yanakuwepo.

Mimi nina hakika serikali ikiweza kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima kwenye taasisi zake basi bajeti itapungua kwa asilimia karibia ya arubaini.
 
Juzi kuna Boss mmoja wa ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kinondoni ameniambia ata Mafuta ya Mashangingi wamepunguziwa liters wanazopewa kwa wiki wanapata Nusu ya wanayotakiwa kupewa kadiri ya Utaratibu.

Na hapo ndiyo serikali itaweza kusave kwa wingi sana. Chukulia mfano, shangingi linapewa mafuta lita 70 kwa wiki, na ikifikia wiki ya pili linaongezewa mafuta bila ya hata kucheki kwamba wiki iliyopita ni mafuta kiasi gani yametumika (kwa kutumia mileage). Akisafiri anapewa fedha za mafuta ya safari na hakuna uhusiano wo wote na mafuta anayopewa ya kila wiki.

Huo ni mfano mmoja lakini iko na mengine kwenye shughuli za usafirishaji ambazo zinazidisha mzigo kwa serikali.
 
Kuna tubilioni kama 200 hivi twa IPTL pale BOT tupo kwenye mchakato wa kuzikwapua.
Kuna hizi za RADAR tunarudishiwa.
Nimeambiwa pia kuna vijibilioni vingine hapo BOT havina mwenyewe(VINAZUBAA) tutavichota.
HATUJAFULIA.
 
Nyinyi ndiyo munaolalamika serikali inatumia fedha nyingi kwa chai za ofisini. Leo zimekatwa munalalamika hakuna chai, hebu amueni sasa ifanye nini maana kila upande ni lawama.

Na kwa kweli huko serikalini vitu vingi viko inflated bila ya kiasi - gharama za kila kitu ziko juu sana kuliko kawaida ili watu wapate ka percent kao hapo. Leo hivyo vitu vikianza kukatwa basi na maneno yanakuwepo.

Mimi nina hakika serikali ikiweza kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima kwenye taasisi zake basi bajeti itapungua kwa asilimia karibia ya arubaini.

kumbuka bajeti ya hivyo vitu ilishapita toka mwaka jana, kama wamekata walitakiwa kusema ili tujue hiyo pesa wanaipeleka wapi? lakini kwa sasa chai ni sehemu ya bajeti na kama haipo ni kufulia mkuu
 
GREAT THINKER!!!! Kutokua na chai maofisini ni dalili za serikali kufulia??? Kazi ipo

Waumini wa uvumi hawaachi kuja na cheap stuff. Mungu wenu Slaa amekuwa akipigia kelele kuwepo kwa chai maofisini. Leo imeondolewa (kama unavyodai wewe) sasa unachomoka na kukimbia kueneza uvumi.
 
Gazeti la MTANZANIA toleo la leo lina habari inatoeleza kuwa Gari la wizara ya maji linashikiliwa katika hoteli ya Landmark, Ubungo baada ya maofisa wa wizara kushindwa kulipa sh.milioni 58!
 
Gazeti la MTANZANIA toleo la leo lina habari inatoeleza kuwa Gari la wizara ya maji linashikiliwa katika hoteli ya Landmark, Ubungo baada ya maofisa wa wizara kushindwa kulipa sh.milioni 58!

Duh! Kindly PM me with some more data on this particular incidence for further action, thanks.
 
plz think twice!! lack of tea in the govt office does not imply that the govt is having shortage of funds, otherwise stated......

True but a colleague of me says that next year no employment (s) within the gvt! If this turns true, then, gvt is in terrible situtation..... Time will tell.
 
Hapa ni kuwa wanamalizia burget ya mwaka,hivyo mara nyingi inavyokuwa wakisubiri buget mpya.Serikali kufilisika kwake sio rahisi kihivyo,maana ina vyanzo vingi vya namna ya kukusanya pesa.Wanaweza leo kubadilisha namba za nyumba na ikatakiwa kila mwenye nyumba alipe 50,000/=itakusanywa shs. ngapi?wanaweza badilisha namba za gari na kila gari wakatoza sh.20,000/=.Hivyo mpaka serikali ifilisike wananchi wake watakuwa wameshaonja joto la tanuru.
 
Ni aibu kweli kweli, Jamaa yangu ananieleza wako katika kukamilisha wizara fulani huko kurasini, na wameambiwa kuwa hakuna kazi mpya kwa mwaka huu, na bajeti imekatwa panga, imeshuka karibu na kiwango walichokuwa wanapata kipindi cha mwinyi. Ni aibu kubwa. Fuatilieni huko kurasini mtajua wizara gani.
 
Nchi hii haina Wachumi au nao wamegeuka kuwa wanasiasa?. Kama Mkulo na wenzake wameshindwa, basi Mchukueni Lipumba, Ndulu na Samwel Wange. Hao ninaamini ni manguli wa uchumi wataisaidia nchi yetu, ila wasiingilwe tu.
Jambo jingine JK hajui kupanga Timu yake ya watendaji. Uswahiba unamponza.
 
Wacheni maneno yenu. Kikwete kasema juzi, Serikali yake inakusanya 5bn a month!!!!!!!!!! kufulia kumetokea wapi? leteni mada ingine siyo hii.

Kazi njemani wajameni. Mie simoooooooooooooooo!!!!!!!!
 
Deni la taifa pia linaongezeka kwa kasi ya ajabu. Huku mfumko wa bei ukitishia hali ya maisha ya watu wenye kipato cha chini. Ukiangalia la maana ambalo serikali inafanyia haya mahela yetu haliönekani. Anayebisha kwb serikali imefilisika lazima ni CCM. Maana wenzetu wanajifanyaga hawaoni adha tunayopata sisi wengine.
 
Hizo ni dua lenu la kuu,swa na fisi kmfuata nyuma binadamu akidhani mkono utandoka.Nyie mlie tu hata 2015 kura mtakazopta zitakuwa pungufu ya 2010.Mmekataa kuheshimu demokrasia na kufanya ubabe wa kufanya kampeniwakati uchaguzi serikali ya CCM ndio iliyoshinda.Sijui mtataoa lawama gani kwa sababu CDM mhehusika kuhujumu uchumi kwa kuwashawishi watu wasifanye kazi ,wachukue sheria mikononi kama vile hii nchi ni lawless.kilichotokea Tarime ni juhudi zenu za kuleta fujo ili nchi iwe ngumu kutawalika.U will pay price for ur evil actions against private sector business like gold mines.Huu ni uhujumu wa uchumi.
 
Back
Top Bottom