Sasa RASMI gazeti la Mwananchi na TanzaniaDaima ni mali ya Chadema.

Hakika sio siri tena kuwa gazeti la Mwananchi na TanzaniaDaima ni magezeti ya Chadema waziwazi na jana wamepata tabu sana kupata stori ya kuenda nayo leo.WameshIndwa kabisa kusema ukweli juu mkutano wa CCM jana jangwani....kwa gazeti kubwa kama Mwananchi hii ni aibu kubwa....
Nasikia harufu ya uvundo, ptuuuu!!
 
Gizakuu,
Magazeti ya leo 11/06/2012

1. Uhuru
- CHADEMA yapasuka; Mbowe, Dk. Slaa wazodoana Kikaoni; Wazee, hatutaki sera za ukabila, fujo; Mikutano yake yasuwiwa na wannchi
- Alhaji Mwinyi Awaonya Waislamu,
- Mgombea Urais Kenya Afariki
- Kikwete amlilia Makani

2. Mtanzania
- CHADEMA: Tumepoteza Jembe; Chasema ni Pigo kubwa kwa Taifa, kuagwa viwanja vya Karimjee Hall leo, Rais Jakaa Kikwete amlilia, atuma salamu
- Maliasili kwatibuka
- Ajali ya helikopta yaua mawaziri, marubani Kenya

3. Habari Leo
- Waziri, Naibu wafa ajalini,
- Dk Mwinyi kukutana na Madaktari
- Makani kuagwa leo Karimjee

4. Mwananchi
- Mawaziri wafariki ajali ya helikopta
- CHADEMA yarudisha makombora CCM Jangwani
- Bob Makani kuzikwa Shinyanga

5. TANZANIA DAIMA
- Mawaziri wateketea kwenye helikopta
- CHADEMA Wamlilia Bob Makani

6. Majira
- Malasusa awavaa viongozi wa siasa
- Waislamu Ausha Wamshukia Askofu Laizer
- Radi yaua sita wa familia Moja
 
Hakika sio siri tena kuwa gazeti la Mwananchi na TanzaniaDaima ni magezeti ya Chadema waziwazi na jana wamepata tabu sana kupata stori ya kuenda nayo leo.WameshIndwa kabisa kusema ukweli juu mkutano wa CCM jana jangwani....kwa gazeti kubwa kama Mwananchi hii ni aibu kubwa....
Wewe kweli ni mbumbumbu: yani unaongea bila facts zozote, somahili gazeti la Tanzania Daima hapa, halafu kama unabisha utafute toleo la jana. CCM yataabika Yakusanya watu kwa maroli mkutanoni na Chalila Kibuda VIGOGO na makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana walilazimika kutumia jitihada za ziada kuhakikisha mkutano wake unaufunika ule uliofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wiki mbili zilizopita. Miongoni mwa jitihada hizo, ni kuwapa fursa Waziri wa Ujenzi, Dk. Harisson Mwakyembe, Waziri wa Miundombinu, Dk. John Magufuli, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na wengine kuzungumzia mazuri yaliyofanywa na chama hicho ambayo yanadhihakiwa na wapinzani. Mwakyembe alitumia mkutano huo kuelezea madudu aliyoyakuta kwenye wizara anayoiongoza, ambayo kwa kiasi kikubwa yamesababishwa na udhaifu wa serikali ya chama chake ambayo kwa muda mrefu imekuwa na utaratibu wa kulindana, kubebana na kufumbia maovu. Alisema tayari ameanza kazi kwa kasi na ameomba apewe miezi mitatu kuishughulikia Mamlaka ya Bandari kwani amepata taarifa kuna madudu mengi ambayo yanasababisha serikali kukosa mapato kwa uzembe wa watu wachache. Waziri huyo alisema matatizo mengine yanatokana na watu kulindana katika kufanya uzembe ambao unagharimu serikali kupata hasara pamoja na kuyafanya mashirika kushindwa kujiendesha yenyewe kwa ufanisi, huku watumishi wakifanya kazi kwa mazoea. “Bandarini kuna madudu makubwa, suala la bandari kugeuzwa 'supermarket' ya vifaa vya magari ni suala ambalo nitalishughulikia kwa nguvu zote, biashara hii itawang'oa ambao wameota mizizi kama mbuyu kwa kuifanya bandari sehemu ya kufanya madudu, “Nitawafukuza kazi wote ambao wanafanya kazi kwa mazoea wizarani pamoja na taasisi ambazo ziko chini ya wizara yangu. Katika mkutano huo mawaziri hao walitaabika kukitetea chama na serikali yao kwani walidiriki kutofautiana juu ya upandaji wa nauli kulikosababishwa na kupaa kwa gharama za mafuta. Wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu, Steven Wassira akisema ugumu wa maisha, kupanda kwa nauli, bei za bidhaa, na huduma muhimu unaowakabili wananchi ni kwa sababu ya kupanda kwa gharama za mafuta huko Uarabuni, Dk. Mwakyembe amepingana naye kwa kusema wanaopandisha nauli za daladala wana matatizo, na serikali haitowavumilia waendelee na utaratibu huo unaokiuka utaratibu wa kisheria wa kupandisha nauli. “Juzi nilipanda daladala kutoka Mwenge kwenda Tegeta nikalipishwa sh 500 badala ya sh 400, nikapanda tena daladala hadi Bunju nikalipishwa tena sh 500, nikapanda tena... ukienda Ubungo hadi Kimara hali ni hiyo hiyo, kwa hiyo nikajikuta safari ndogo natumia sh 1500, pesa ambayo kwa Mtanzania wa kawaida hawezi kuimudu kila siku,” alisema Mwakyembe. Kwa upande wake, Magufuli aliwahakikishia wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa na suluhisho na kudumu la barabara na kwamba tayari miradi kadhaa inatekelezwa. “CHADEMA wanasema tu, lakini wao sasa hivi wanafanya maandamano katika lami… nawapongeza sana na ninaamini wataendelea kuandamana katika lami huku wakiendelea kuisema serikali ya CCM vibaya," alisema Dk. Magufuli. Dk. Magufuli aliyetumia muda wake mwingi kuelezea mafanikio ya barabara katika Mkoa wa Dar es Salaam na nchi nzima huku akitumia lugha za mikoa mbalimbali, alisema CHADEMA ni chama kilichokosa shukrani. Alisema CHADEMA wanapiga kelele bure wakati huo huo wakiendelea kuandamana katika barabara za lami. Magufuli na Mwakyembe wote wamekiri kuwa kuna tatizo la foleni kubwa jijini Dar es Salaam na kutoa mikakati ya kutatua, lakini jambo kubwa linaloonekana kuwatesa ni utekelezaji wa ahadi hizo. Nae Waziri Wassira alitoa takwimu za kuongezeka na kuboreka kwa shule, wanafunzi, zahanati, vituo vya afya, lakini akakwepa kuzungumzia uduni wa huduma zinazotolewa sehemu husika. Nape na Jumuiya ya Uamsho Katibu wa Uenezi na Itikadi CCM, Nape Nnauye, akihutunia mkutano huo, alikemea vurugu zinazodaiwa kuchochewa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) inayohamasisha Wazanzibari kuupinga Muungano. Nape alisema Jumuiya ya Uamsho ni majambazi na akaitaka serikali iwashughulikie. Kinana aishambulia CHADEMA Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Abdulrahman Kinana, alitumia fursa hiyo kuwataka Watanzania wawapuuze wapinzani, kwamba wamekuwa hawana ajenda ya kulikomboa taifa zaidi ya kuwatukana viongozi wa serikali. Alisema CCM, haitaacha kueleza mafanikio mbele ya Watanzania kutokana na chama hicho kupewa dhamana ya kuiongoza nchi. Watu kusombwa na maroli Tanzania Daima Jumapili, lilishuhudia idadi kubwa ya magari yakiwa na makada wa CCM wa ndani na nje ya Jiji la Dar es Salaam yakiwasili kwenye viwanja vya Jangwani kuhudhuria mkutano huo ulioitishwa na viongozi wa mkoa huo. Viwanja hivyo vilifunikwa na magari yaliyokodiwa na matawi ya chama hicho kwa ajili ya kuwapeleka wananchi kushiriki mkutano pamoja na kuwapa sare za chama zikiwemo kanga, miamvuli, kofia, mashati na vilemba. Makada wa chama hicho tawi la Mabwepande, walikuwa na mabango ya kumshukuru Rais Kikwete kwa kuweka mji mpya wenye makazi bora. Hata hivyo, walionesha kushtushwa na matumizi ya fedha juu ya mkutano huo, huku wakiweka wazi kuwa fedha hizo zingewasaidia kuboresha huduma ya maji kwenye maeneo wanayoishi. Kada wa chama hicho, Magdalena John alisema kuwa CCM imekuwa kimya kushughulikia matatizo ya wananchi, hali ambayo wapinzani wanatumia udhaifu wao kujipatia umaarufu. Alipoulizwa kama alihudhuria mkutano huo kwa ushawishi wa fedha, alisema: “Mimi sijapatiwa fedha ili nihudhurie, lakini ni utashi wa mtu wa kuchukua au kutochukua, kama kuna watu wamepata basi ni wao.” Viwanja vya Jangwani vyajaa Katika mkutano huo, maelfu ya wanachama wa CCM, wakazi wa jiji la Dar es Salaam na maeneo jirani walijazana kwenye viwanja vya Jangwani, huku vibwagizo cha wasanii mbalimbali vikionekana kukonga nyoyo za waliohudhuria. Miongoni mwa wasanii na makundi yaliyokuwapo ni TOT, Twanga Pepeta, Chege Chigunda na Malkia wa Mipasho nchini, Khadija Kopa.
 
Wameacha kuandika maana kama wange andika jinsi mlivyo beba watu kwenye mafuso ungelalamika.
 
Kwani kuna kosa gani Mwananchi na Tanzania Daima kuwa ya CCM, kama Uhuru na Habari leo, Mtanzania yote ni ya Magamba. Acha ushamba
 
Ukweli ni kwamba CCM kimepoteza mvuto kwa watu makini ambao hasa ndiyo wenye udadisi na uwezo wa kununua magazeti. CCM kimebaki ni cha kupigiwa chapua na wacheza segere, wapwani na watu walioishiwa uwezo wa kuwa na mawazo huru zaidi kusoma alama za nyakati.

Sasa media zinakuwa kwenye dilema.Ukizipa uzito habari za CCM gazeti haliuziki maana wafuasi wake ni wacheza segere, wazee na watu walioishiwa uwezo wa kudadisi, kufikiri na kutaka mawazo mapya.

Gazeti likitoka na habario kubwa Front page ya CDM tena yenye picha ya nyomi kwenye mkutano mauzo ya magazeti yanakuwa juu na ukichelewa kuamka kuwahu gazeti unakuta yameisha.

Sasa katika hali kama hii nani yuko tayari kuzipa uzito habari za CCM ili gazeti alke life?No haiwezekani.
 
Yawezekana unachokisema kikawa na chembe chembe za ukweli ila nakuuliza swali moja....Wewe na wenye hilo gazeti nani mwenye akili zaidi.....Bila shaka jibu liko wazi hata kama utataka kulipindisha.....
ni Kwamba watakuwa wamesoma alama za nyakati kwakuwa wana akili kuliko wewe....ndugu yangu giza kuu Vua giza Kuu uvae Mwanga mkuu....
 
tanzania leading newspapers are:

1.mwananchi
2.tanzania daima
3.nipashe
4.mtanzani

hayo mengine yote yaliobaki ni ya udaku na porojo nyingi tu.
 
Hakika sio siri tena kuwa gazeti la Mwananchi na TanzaniaDaima ni magezeti ya Chadema waziwazi na jana wamepata tabu sana kupata stori ya kuenda nayo leo.WameshIndwa kabisa kusema ukweli juu mkutano wa CCM jana jangwani....kwa gazeti kubwa kama Mwananchi hii ni aibu kubwa....

Ni ujinga kujadili vitu vila utafiti. Watu wanakurupuka huko, hata gazeti hawajalitafuta wala kuliona, wanazomoka na kudanganya umma; na wachangiaji wengine tunaunga wagon bila kufikiri mara mbili. Gazeti la Mwananchi jana liliandika habari hii kuhusu mkutano wa Jangwani CCM yaijibu Mapigo ya Chadema Dar, ilikuwa ya pili kwa uzito baada ya ile ya kifo cha Makani. Habari hii ina matatizo gani? Ila tu kwenye website ilichelewa kuingia maana ilikupatikana late, ilikuwa breaking news, Exlusive and Stop Press.
 
A photo can speak a thousands words, wacha kupiga mayowe wacha watu waone wenyewe.
Serikali ya Kenya ikitimiza ahadi zake ya kujenga Flyovers Nairobi kwa vitendo.

View attachment 56037

Matola,

Haya ndio matatizo ya kuchanganyikiwa; hatujamaliza ya Jangwani umerukia ya flyover; hata Kikwete amaeanza kutimiza ahadi zake si unaona mradi wa Rapid Trans ulivyoshika kasi? Lengo ni kuondoa masongamano hilo linafanyiwa kazi tumalize ya Jangwani.

Chama
Gongo la Mboto DSM.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom