Sasa Rais afanye nini - Pinda anamrushia mpira naye hataki kucheza?

Uzuri ni kwamba Kikwete amewafundisha watanzania kufikiria mara mbili kabla ya kupata mpangaji wa magogoni. sio kila mtu anaweza kuwa rais.

Rais anatakiwa kuwa mtu tough mwenye upeo mkubwa wa kuona mambo, mwenye authority na ambaye akisema watu wote wanamsikiliza. Uraisi haitaki ubia kama wa JK, kila maamuzi makubwa lazima ufuate wabia wako.

Kwa manaa hii, hata kama baraza la mawaziri likivunjwa, kuna mpya? atapata wapi watu wapya wa kuleta mabadiliko? Watu kama hao wapo CCM? Na ni wazi kwamba hawezi kuteua mawaziri kutoka upinzani.

Watanzania tuna sifa ya amani na utulivu. Sifa hii ndio imeleta yote haya. Tumekuwa taifa la kuridhika na kila kitu, hatuwezi ku struggle, kupinga serikali na kuonyesha malalamiko na kutoridhika kwetu. Kama huamini, angalia hali ya maisha ilivyo ngumu na watu bado wamekaa kimya. kwa maana hiyo, wananchi hawawezi kuwa na option ya kushinikiza.

The last and viable option ni 2015.

Mkuu,
Very well said. CCM sio option kwa vyovyote vile kulingana changamoto tete zinazokabili nchi hii kwa sasa.

Nimeipenda kwa vile sasa wananchi watakuwa wanatumia akili zao vizuri kufikiri, kuchambua na kuchangua.

Lakini kati ya sasa na Octoba 2015 kuna mwendo! If there's better solution b4 then I will meditate it.
 
The most useless Person in Magogoni at all the time in our country history. Sitegemei mabadiliko kutoka kwake zaidi ya sisi wenyewe wananchi kufanya mabadiliko ya kumtimua kinguvu hata ikibidi kutumia bunduki ili kuweza kulinisuru hili Taifa zidi ya hawa Wapumbavu, tusipofanya hivyo vizazi vijavyo vitatulaumu kwa ujinga na upumbavu wetu. Its time now or never, Muda wa bla bla umekwisha sasa tunahitaji Vitendo vya kulikomboa hili Taifa
 
Mfumo na mawaziri wameoza na dawa ni ku overhaul serikali yote......JK hawezi kuchukua hatua cuz hana nia ya dhati na kinachoonekana nchi ilishamshinda hivyo anavuta muda tuu 2015 ifike but tutafikaje kwa mendo huu?????
 
tatizo ni kwamba rais hana replacement kwa nyazifa za mawaziri.
Hana mpango mbadala
Hana uwezo wa kuamua cha kufanya
.
Hana uoga wa lolote.
Hana chochote cha kupoteza.
Hawezi kuamua.

Mkuu hapo kwenye RED si sahihi hata kidogo
Kama atikitala kuunda Baraza Dogo litakaloperform vizuri, atapata watu wazuri, na atapunguza gharama. Kwa hapa tulipofikia anaweza hata akachukua compitent personel kutoa vyama vyama vya upinzani kama ataona wanamfaa, kwani katiba na sheria nyingine ndogo ndogo hazizuii hilo.

Kumbuka bado rais hajatumia zile nafasi zake 7 za kikatiba. Na kama tatizo ni CCM kwa sasa, bado anaweza akalivunja bunge ili tuanze moja
 
Kimsingi hatuna Rais mwenye hadhi na mamlaka ya Rais, kwa kipindi chake chote kashindwa kutofautisha urafiki na utendaji kazi. Naunga mkono wanaoshauri Pinda ajivue gamba, maana kabaki mtu wa kuumia na kulalamika siku zote.
 
Sasa nimeamini Gazeti la Mtanzania lina uchokozi wa ukweli ukweli. Gazeti lilisema 'UPEPO HUU UTAPITA! Ni kweli si mnaona. CCM ni gari linalokwenda mtoni kwa kasi ya 200km/hr huku dereva amekwenda nyuma kupiga story. Nawasilisha
 
Kama kweli Pinda hana maamuzi ktk baraza la mawaziri wake na kweli hawawajibishi hana maana ya yeye kuendelea kuwepo ktk kiti hicho cha WM kama pambo tu ni bora ajiuzuru ili raisi mwenye uwezo wa kuwawajibisha mawaziri wanaolalamikiwa aweze kufanya kazi au aendelee na ziara ambazo zitasimamishwa na nguvu ya umma. Hii maana yake nini kila kunapokuwa na tatizo kubwa nchini raisi wetu ye ndo anaona ni muda wa kutoka nchini ni kukwepa wajibu wake au ni nini? Pinda kama kweli amebanwa na ajitoe kama posho lake ataendelea nalo.
 
" Lakini katika sakata lile la madaktari mwisho wa siku Waziri Mkuu akampasia Rais Kikwete mpira na safari hii Rais akacheza kama pele kwa kuwapiga mkwara wake madaktari na kuwalazimisha kurudi kazini. Madai yao ya kutaka Waziri na Naibu wake waondoke yakipuuzwa! Wote bado wapo na wanaendelea na kazi. Hakutaka kucheza. "

Naona kuna mgongano wa hoja hapo, kama rais alipasiwa na akacheza kama pele, mwisho unatoa conclusion HAKUTAKA KUCHEZA.

Wewe unajua ushauri pinda liompa rais wake? unakijua walichoongea maDr na Rais magogoni? huwezi kuja na conclusion unless ujue alichoshauriwa JK na pinda na alichozungumza rais na madr.
yet another fabricated story.
 
yes mwanakijiji
This indicate that the ruling part government has failed,has no serous presdent who can analys issues on his government,how can his govn has eighty minister which according to mp are "total corupt minsters",and he ddn't even think about his country, he just pass air to air(Brasil to malawi) with cofindency,
 
Kama kweli Pinda hana maamuzi ktk baraza la mawaziri wake na kweli hawawajibishi hana maana ya yeye kuendelea kuwepo ktk kiti hicho cha WM kama pambo tu ni bora ajiuzuru ili raisi mwenye uwezo wa kuwawajibisha mawaziri wanaolalamikiwa aweze kufanya kazi au aendelee na ziara ambazo zitasimamishwa na nguvu ya umma. Hii maana yake nini kila kunapokuwa na tatizo kubwa nchini raisi wetu ye ndo anaona ni muda wa kutoka nchini ni kukwepa wajibu wake au ni nini? Pinda kama kweli amebanwa na ajitoe kama posho lake ataendelea nalo.

Mie kwa akili zangu za chekechea nilijua kuwa waziri mkuu ndio mtendaji mkuu wa serikali, na alitakiwa kutoa tamko na ONYO kali kwa puuzi zinazoendelea. Lakini jinsi ninavyozidi kukua nagundua kuwa the man is just a ceremonial leader, na pengine yuko plae kwa ajili ya mapitisho ya fisadi zingine, consuming our money. La, sioni umuhimu wa vyeo hivi hapa Tanzania
  1. Waziri Mkuu
  2. Makamu wa Raisi.
Hawana hata uwezo wa kumshauri huy boga aliye huko juu. Inauma kwa kweli kuona tunachezewa shere kiasi hiki. bora tugawane majibo na kila jimbo liwe na Raisi wake, ili tutiane adabu "KIMILA" huko.
 
Mie kwa akili zangu za chekechea nilijua kuwa waziri mkuu ndio mtendaji mkuu wa serikali, na alitakiwa kutoa tamko na ONYO kali kwa puuzi zinazoendelea. Lakini jinsi ninavyozidi kukua nagundua kuwa the man is just a ceremonial leader, na pengine yuko plae kwa ajili ya mapitisho ya fisadi zingine, consuming our money. La, sioni umuhimu wa vyeo hivi hapa Tanzania
  1. Waziri Mkuu
  2. Makamu wa Raisi.
Hawana hata uwezo wa kumshauri huy boga aliye huko juu. Inauma kwa kweli kuona tunachezewa shere kiasi hiki. bora tugawane majibo na kila jimbo liwe na Raisi wake, ili tutiane adabu "KIMILA" huko.

Pinda hawezi kuwa na maamuzi kwa walio chini yake kwani wote wako pale kwa ajili ya mkulu ili WM huyu ajilindie heshima yake ambayo imepotea kkwa kukosa confidence / power of command. Tusubiri siku akiwa na kimavi ndo utasikia akilalama kuwa mi nilikuwa tu kondoo wa kafara, na achukuwe hatua sasa.
 
Wasubirie nguvu ya umma ndo itawaadhibu

We are tired of them already, wanatutoa povu hapa, usikute wao sasa hivi wako kwenye majacuzzi wanafurahia posho walizokusanya for the two weeks or so, za vikao vilivyokwisha. Haki ya MUNGU vile tutawafunga mawe shingoni mwao tuwatpe BAHARINI, they don't deserve this LAND
 
waacheni waliochaguliwa na wananchi wamalizie muda wa miaka 5 waliopewa na wananchi wa majimbo wao (mawaziri), na rais chaguo la Mungu aliyechaguliwa na waTanzania (kumbuka repoti za baada ya uchaguzi mpaka za viongozi wa dini)
Tuombe uchaguzi ujao waTanzania tujue kuchagua makapi then kulalamika ndio kansa ya Utanzania,......Gabbage in Gabbage Out coz mawaziro wote wanaotakiwa kujiuzulu walichaguliwa na watanzania tena kwenye majimbo ambayo wanaishi maisha duni (chini ya 1US $)
 
hatuna serikali ikiwa inashindwa kutekeleza majukumu yake.
ila kuna kikundi cha watu wanaofanya biashara yao na kujiwekea namna rahisi ya kufaika kupitia wengi.na huu ni unyonyaji ama wizi.
 
Kwa karibu mara tatu sasa ndani ya miezi hii minne tumeshuhudia mchezo fulani ambao kidogo umeanza kukera. Pinda anacheza peke yake na kila akimpatia Rais afunge goli, rais siyo tu hafungi goli hataki kucheza! Kwenye sakata la Jairo Pinda alifanya alichoweza kufanya lakini mwisho wa siku akatuambia kuwa Rais ndiye aliyekuwa na uwezo wa kuchukua hatua mara moja na kweli hata Rais aliporudi toka Afrika ya Kusini hakuna lililofanywa zaidi ya Jairo kusimamishwa na Katibu Mkuu Luhanjo.

Lilipokuja suala la mgomo wa madaktari Rais Kikwete aliondoka na kusafiri kwenda nje tena na akiwa huko mgomo uliiva huku Pinda akiachiwa jukumu la kutengeneza jambo hilo. Alijitahidi Pinda hadi ukomo wa madaraka yake - hakuwa na uwezo wa kumwajibisha Waziri yeyote na kwa kweli hakuwa na uwezo wa kuwawajibisha madaktari wote - kama alikuwa nayo basi hayakuwa wazi baada ya kuwafukuza madaktari kazi lakini hawakufukuzika! Lakini katika sakata lile la madaktari mwisho wa siku Waziri Mkuu akampasia Rais Kikwete mpira na safari hii Rais akacheza kama pele kwa kuwapiga mkwara wake madaktari na kuwalazimisha kurudi kazini. Madai yao ya kutaka Waziri na Naibu wake waondoke yakipuuzwa! Wote bado wapo na wanaendelea na kazi. Hakutaka kucheza.

Sasa suala la ripoti za CAG kwa mara nyingine limefunua yale yale tunayoyajua - hakukuwa na jipya. Lakini wabunge na wananchi walianza kupiga kelele sana. Siku ya Jumamosi kelele hizo zilizidi kiasi cha baadhi ya watu kuripotiu kuwa mawaziri kadhaa walikuwa wanajiuzulu na wengine wakisema pia kwa uhakika kuwa tayari wameshajiuzulu. Hili pia lilitokea wakati Kikwete akiwa nje ya nchi na huku nyuma ni Waziri Mkuu PInda akiachwa kukiona cha moto. Nina uhakika wa asilimia 100 kuwa kama Rais angekubali mapendekezo ya wabunge wa CCM kuwa mawaziri watoke wangetoka lakini pamoja na Pinda kuwa matatani Rais hakutaka kucheza.

Rais sasa yuko pagumu kwani ni wazi kuna njia mbili tu za kutokea (ya tatu ni ile niliyoileza kwenye mada ya 'no half revolutions'). Kwanza ni kuvunja baraza la mawaziri na kupata waziri mkuu mpya hili litaturudisha kwenye 2008. Bahati mbaya utaona kuwa tukio la 2008 lilitokea karibu miaka miwili na miezi kadhaa baada ya ushindi wake. Hili la mwaka huu kama likitokea litakuwa nalo limekuja karibu muda ule ule tena kiasi cha kutuaminisha kuwa miaka miwili ya miezi kadhaa ndio maisha tu ya baraza lake kabla halijaanza kuboronga! Ndugu yangu Mchambuzi anaita hiki ni "instability" ya serikali. Njia ya pili ni kufanya "mabadiliko makubwa" yaani kuwaondoa baadhi ya mawaziri bila kumuondoa Waziri Mkuu. Sasa akimuondoa Waziri Mkuu atajipa kazi ngumu zaidi kwani wakati Lowassa aliondolewa kwa kuhusishwa na kashfa ya Richmond, Pinda aweza kuondolewa kwa kutokuhishwa na kashfa yoyote yeye mwenyewe bali kuwa alama ya serikali iliyoshindwa.

Kuendelea hivi hivi kama ilivyo sasa inawezekana ndio option yenyewe kwa sababu maneno aliyoyasema Makinda leo yanaweza kuwa ndio sentiment ya Rais pia - kusemwa wanakosemana hakujalishi kama ni ukweli au ni uzito mawaziri na watendaji wa serikali wasijali sana kwani ni sehemu tu ya majukumu yao. Lakini kujaribu kubadilisha kwa namna yoyote ile kutathibitisha tu kuwa bado Rais Kikwete hajapata dawa ya matatizo katika uongozi wake na sasa ameamua kubadilsiha chupa tu na label tu lakini kilichomo ni kile kile.

sasa afanye nini?

ang'a'tuke
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom