Sasa Rais afanye nini - Pinda anamrushia mpira naye hataki kucheza? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa Rais afanye nini - Pinda anamrushia mpira naye hataki kucheza?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 24, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwa karibu mara tatu sasa ndani ya miezi hii minne tumeshuhudia mchezo fulani ambao kidogo umeanza kukera. Pinda anacheza peke yake na kila akimpatia Rais afunge goli, rais siyo tu hafungi goli hataki kucheza! Kwenye sakata la Jairo Pinda alifanya alichoweza kufanya lakini mwisho wa siku akatuambia kuwa Rais ndiye aliyekuwa na uwezo wa kuchukua hatua mara moja na kweli hata Rais aliporudi toka Afrika ya Kusini hakuna lililofanywa zaidi ya Jairo kusimamishwa na Katibu Mkuu Luhanjo.

  Lilipokuja suala la mgomo wa madaktari Rais Kikwete aliondoka na kusafiri kwenda nje tena na akiwa huko mgomo uliiva huku Pinda akiachiwa jukumu la kutengeneza jambo hilo. Alijitahidi Pinda hadi ukomo wa madaraka yake - hakuwa na uwezo wa kumwajibisha Waziri yeyote na kwa kweli hakuwa na uwezo wa kuwawajibisha madaktari wote - kama alikuwa nayo basi hayakuwa wazi baada ya kuwafukuza madaktari kazi lakini hawakufukuzika! Lakini katika sakata lile la madaktari mwisho wa siku Waziri Mkuu akampasia Rais Kikwete mpira na safari hii Rais akacheza kama pele kwa kuwapiga mkwara wake madaktari na kuwalazimisha kurudi kazini. Madai yao ya kutaka Waziri na Naibu wake waondoke yakipuuzwa! Wote bado wapo na wanaendelea na kazi. Hakutaka kucheza.

  Sasa suala la ripoti za CAG kwa mara nyingine limefunua yale yale tunayoyajua - hakukuwa na jipya. Lakini wabunge na wananchi walianza kupiga kelele sana. Siku ya Jumamosi kelele hizo zilizidi kiasi cha baadhi ya watu kuripotiu kuwa mawaziri kadhaa walikuwa wanajiuzulu na wengine wakisema pia kwa uhakika kuwa tayari wameshajiuzulu. Hili pia lilitokea wakati Kikwete akiwa nje ya nchi na huku nyuma ni Waziri Mkuu PInda akiachwa kukiona cha moto. Nina uhakika wa asilimia 100 kuwa kama Rais angekubali mapendekezo ya wabunge wa CCM kuwa mawaziri watoke wangetoka lakini pamoja na Pinda kuwa matatani Rais hakutaka kucheza.

  Rais sasa yuko pagumu kwani ni wazi kuna njia mbili tu za kutokea (ya tatu ni ile niliyoileza kwenye mada ya 'no half revolutions'). Kwanza ni kuvunja baraza la mawaziri na kupata waziri mkuu mpya hili litaturudisha kwenye 2008. Bahati mbaya utaona kuwa tukio la 2008 lilitokea karibu miaka miwili na miezi kadhaa baada ya ushindi wake. Hili la mwaka huu kama likitokea litakuwa nalo limekuja karibu muda ule ule tena kiasi cha kutuaminisha kuwa miaka miwili ya miezi kadhaa ndio maisha tu ya baraza lake kabla halijaanza kuboronga! Ndugu yangu Mchambuzi anaita hiki ni "instability" ya serikali. Njia ya pili ni kufanya "mabadiliko makubwa" yaani kuwaondoa baadhi ya mawaziri bila kumuondoa Waziri Mkuu. Sasa akimuondoa Waziri Mkuu atajipa kazi ngumu zaidi kwani wakati Lowassa aliondolewa kwa kuhusishwa na kashfa ya Richmond, Pinda aweza kuondolewa kwa kutokuhishwa na kashfa yoyote yeye mwenyewe bali kuwa alama ya serikali iliyoshindwa.

  Kuendelea hivi hivi kama ilivyo sasa inawezekana ndio option yenyewe kwa sababu maneno aliyoyasema Makinda leo yanaweza kuwa ndio sentiment ya Rais pia - kusemwa wanakosemana hakujalishi kama ni ukweli au ni uzito mawaziri na watendaji wa serikali wasijali sana kwani ni sehemu tu ya majukumu yao. Lakini kujaribu kubadilisha kwa namna yoyote ile kutathibitisha tu kuwa bado Rais Kikwete hajapata dawa ya matatizo katika uongozi wake na sasa ameamua kubadilsiha chupa tu na label tu lakini kilichomo ni kile kile.

  sasa afanye nini?
   
 2. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Kikwete anamalizia Muhula wake wa Mwisho hana cha kupoteza, na hii ni picha harisi ya Kikwete angetoa ushirikiano tu iwapo wabunge wangeonyesha wanataka kutoa hoja ya kutokuwa na imani naye, maana hii ingehatarisha uwezekano wa Kumalizia muhula wake.
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,275
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji hapa hakuna haja ya kujaza maandishi, kama JK angekuwa ni mtu wa maana kama wengi wanavyotaka tuamini ukweli option ni 2 tu:

  1. Avunje Bunge turudi kwenye uchaguzi
  2. Au yeye mwenyewe aachie ngazi

  JK nchi imemshinda hakuna option nyingine yeyote itakayoisaidia nchi hii zaidi ya hizo option mbili hapo juu.
   
 4. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ninaamini kwamba hawa Wataalam wa Afya kupitia uwezo wa Viongozi wetu kufikiri, soon watakuja na finding mpya. Tegemeeni ugunduzi wa kisayansi kwamba kuna MENOPAULSE ya akili.
   
 5. w

  wikolo JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mwanakijiji, bado nakumbuka ile post yako ya siku chache zilizopita kwamba haya yote ni mazingaombwe. Kwa watu hawa wa mazingaombwe, siku zote huwa ni ujanja ujanja tu na kufikiria ni jinsi gani wataghiribu akili za watu zaidi. Hapa tutarajie mazingaombwe zaidi na si kingine chochote!
   
 6. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2012
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji,

  Watanzania na Upinzani tumshukuru Mungu kwa haya yote yanatotokea. This is just another very open indication kwamba CCM na serikali yake na Sera zake vyote vimeshindwa.

  Ni somo la pekee na ni kama mwalimu anaandika ubaoni akiwafundisha wanafunzi kuwa "CCM na Serikali yake vimeshindwa".

  Kazi ni moja tu, Upinzani wayachukue yote haya na kuhakikisha kuwa Wananchi wote wanaujua uozo huu. CCM na Serikali hawatakuwa na guts za kwenda kujitetea kwa maana CCM wenyewe wamegawanyika na mbaya zaidi sasa "Hata Serikali nayo imegawanyika". Wote tumeshuhudia Mawaziri wakisigana"

  Mungu Ibariki Tanzania!
   
 7. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Comrade kama ungekuwa wewe kila ukimpasia team met wako afunge nae hafungi nawe uwezo wa kufunga huna kwa nini uendelee kucheza hiyo mechi ambayo malengo yake sio ushindi? kwani ukitoka ndani ya kiwanja na kukaa jukwaani na kumuacha acheze mwenyewe huoni kama itakuwa ndio suruhisho?
   
 8. MANI

  MANI Platinum Member

  #8
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  You are right Mkuu this guy has nothing to lose and he don't want to keep good paltform for his party to win in 2015.
   
 9. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #9
  Apr 24, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  mimi nafikiri J.K amedhamiria kuiacha nchi hii mikononi mwa wapinzani, yeye mwenyewe anaona kwamba CCM imeshindwa na soon itakufa kabisa hivyo anatayarisha mazingira mazuri kwa wapinzani kuchukua nchi, hongera J.K kwa kuwa mzalendo wa kweli, shikilia hapo hapo, kimya kimya usisikilize la mtu.
   
 10. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #10
  Apr 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa Matola. Hapo tuko pamoja sana.
   
 11. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #11
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Dhambi inayomsumbua Kikwete na ambayo inalimaliza Taifa letu ni juu ya Rais wetu kushindwa kutenganisha MADARAKA aliyopewa na MARAFIKI wanaomzunguka.

  Kikwete amekuwa akigawa nafasi nyingi na nyeti katika nchi yetu kwa kuangalia marafiki alionao badala kuangalia uwezo na uadilifu wa mtu anayempa madaraka ama nafasi husika.

  Kinachomsumbua Kikwete kwa sasa hana uwezo na uthubutu wa kuwakemea hao aliowapa madaraka na kwake anaamini kila kelele itakayopigwa ina ukomo wake na mambo mengine yataibuka hivyo wananchi watasahau.

  Kwa kujiaminisha hivyo nafikiri atakumbana na mengi na pale wananchi watakapoamua kupiga kelele kwa pamoja sijui nani ataweza kuwanyamazisha.
   
 12. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #12
  Apr 24, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tatizo si la hao wachezaji, tatizo ni letu sisi (kocha).
  Yaan kweli kocha unaona mchezaji wako anaboronga na kukupotezea point tatu za muhim halafu bado unamuanagilia??
  Ni ama kocha haujui mchezo wa mpira au anamuogopa mchezaji husika, lakin jukumu kubwa ni la kocha kufanya sub.
  Ni aibu gani hii kwa watanzania, kuiona nchi yao inaelekea inapoelekea hata baada ya kuujua ukweli!!!
  Tuchukue hatua
   
 13. bombu

  bombu JF-Expert Member

  #13
  Apr 24, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,134
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Pinda alitakiwa awe mkweli kwa nafsi yake, ajitendee haki na kuwatendea haki watanzania, kama kweli ana dhamira safi. Ajitoe kwenye msururu huo kama kweli ana nia ya dhati ya kufanya maamuzi, kwa nini kuwepo mahali ambapo mchango wake hauna thamani na wala hauonekani? Ajitoe ili kuuthibitishia umma kuwa mambo yanayoendelea haafikiani nayo, if at all he has guts.

  Hapa tumlaumu Pinda na wala si JK, yeye alitakiwa aanze kuchukua hatua, kama mzalendo wa kweli ili kumthibitishia JK kuwa he is a man enough to stand for his own people. My take
   
 14. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #14
  Apr 24, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  JK akae asiongee lolote ni upepo utapita tuu!
   
 15. D

  Deofm JF-Expert Member

  #15
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hiyo kazi tulishamaliza kitambo, ndiyo maana kukawepo umri wa kustaafu kwa lazima. Kwa taarifa yako angalia wanaosinzia bungeni ni watu wa umri gani utapata jibu. Rejea Hooks' law. ni ya kiengineer, lakini inahold " Provided the elasticity limit is not exceed the deformation of material is proportion to the force applied.
   
 16. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #16
  Apr 24, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  tatizo ni kwamba rais hana replacement kwa nyazifa za mawaziri.
  Hana mpango mbadala
  Hana uwezo wa kuamua cha kufanya.
  Hana uoga wa lolote.
  Hana chochote cha kupoteza.
  Hawezi kuamua.
   
 17. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #17
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,000
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  JK ndio chanzo cha matatizo yote hayo,
  Hatufai kabisa huyo mtu angejiuzuru tu ili tuchague kiongozi mzarendo.
   
 18. m

  mweleka Member

  #18
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mie naamini mahali tulipofika sio tena kuangaikia mawaziri maana aliye wachagua anawalinda. Hii inaonyesha wazi kuwa raisi ni mtu wao na madudu wanayoyafanya ni kwa faida yake na familia yake. Raisi hana maslahi na nchi yetu wala na chama chake, sasa huyu ni kiongozi wa aina gaini. Hii inasikitisha sana kuona nchi inayumba kama inaendeshwa na mlevi wa gongo.
   
 19. D

  Deofm JF-Expert Member

  #19
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Rais wetu ni msikivu
   
 20. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #20
  Apr 24, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dawa ni MAANDAMANO mpaka IKULU, tukamtoe huyu mtu ktk NYUMBA ile TAKATIFU, KIKWETE ndiyo GAMBA tena GUMU, tofauti na hapo tuendelee kulalamika na kama WABUNGE WA CCM.

  Sidhani kama MUNGU anapenda wananchi wanaolalamika tu kila siku bila ya kuchukua hatua wakati yeye katupatia akiri, nguvu na maharifa.

  Muda wa maamuzi ndio huu. Wake up Tz
   
Loading...