Nilijiunga na chama cha mapinduzi baada ya kumaliza shule nikiwa na matumaini makubwa na chama changu, nimeendelea kuishi kwa matumaini nikijua kuwa matatizo yaliyoko hapa nchini yanatokana na mfumo mbaya wa dunia. Nilikuwa naviogopa vyama vya upinzani kama ukoma nikjua kuwa ni wababaishaji na watu wanaotafuta ulaji na umaarufu tu.
Sasa nimebaini kuwa wana CCM wengi tunaishi katika dunia ya uoga, hatuwezi kuzungumza mawazo yetu na tunamuogopa sana mwenyekiti wetu kama vile yeye ni mungu mdogo. tunaishi katika kivuli cha kugandamizwa na wala hakuna mahala tunapoweza kusikilizwa au kuwasikiliza viongozi wetu.
Kwa jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa na kwa jinsi ambavyo CHADEMA wameonyesha kwa kumsusa Mwenyekiti wetu bila woga wala kumtusi mtu, nimeamini kuwa lolote lawezekana hata mimi naweza kuondoka ktk hiki chama na maisha yangu yakaendelea kama kawaida!
Nawaomba CHADEMA mnikaribishe kwenye chama chenu, mnipatie maelekezo namna ya kupata kadi ya chama chenu ili niwakabidhi hii niliyo nayo ya CCM. Mimi naishi Tabata nafanya kazi kwenye taasisi ya umma hapa Dar.