Sasa nimehakikisha bila chembe ya wasi wasi wowote kwamba CCM ni chama cha mafisadi.

Kwamhuzi

JF-Expert Member
Nov 15, 2014
1,762
400
Tumeaminishwa kwa muda mrefu kwamba CCM ni chama kinachotetea maslahi ya watanzania.Jambo hili limeonekana katika majukwa ya siasa likitetewa kwa nguvu zote.Hata hivyo watu makini waliona kwamba yaliyozungumzwa kwenye majukwa ya siasa na CCM yalikuwa mbali na ukweli.Ukwasi ambao CCM na watendaji wake hata wale wa ngazi za chini walikuwa nao ulikuwa na maswali mengi ya kujiuliza.Kusema kweli haikueleweka kirahisi ukwasi huu unatoka wapi.Hata hivyo baada ya kuonja joto ya jiwe,wanachama wa CCM wamefunguka.Sasa wanasema wazi kwamba Magufuli amefunga bomba.Kwamba sasa pesa ambayo CCM ilikuwa inapata kwa kuweka viongozi wake wa juu serikalini sasa haipo tena.Inaeleweka sasa kwa nini Mwigulu alikuwa kiongozi wa juu kwenye chama na pia Naibu waziri hazina.Nia ilikuwa kuhamisha hela ya watanzania kutoka hazina na sehemu zingine kwenda CCM, ili itumike kwa ajili ya kuwafanya wanachama wake kwa nguvu zote kuipigia debe CCM.Wana CCM sasa wanasema wazi, bila kupewa fedha nzuri kama zamani mambo yatakuwa magumu

Wanakwenda mbali zaidi.Wanasema Magufuli anavyofanya ni vibaya.Hakupaswa kufika huko.Wafanyibiashara wakubwa na mafisadi ndio waliokuwa wanainemesha CCM na watendaji wake.Kuwasakama kama anavyofanya sasa na hatimaye labda kuwafirisi kabisa, kutainyonga CCM kwa kuikosesha mapato na kuwakosesha wanachama na viongozi mbali mbali wa CCM ukwasi ambao walikuwa wameuzoea.Hali si shwari CCM,hali ni tete,hali ni mbaya.Wanachama wa CCM wanamchukia Rais wetu sana.

Nini kinacho dhihirika hapa.CCM si chama kinachotetea maslahi ya watanzania.CCM ni chama kinachotetea maslahi ya wale wanaokiwezesha kubaki madarakani:mafisadi na makada wake wanaokipigia debe ili kiweze kukubalika kwa watanzania wasio jitambua.

Ushauri wangu kwa Rais wetu kipenzi ni kwamba ai-strangle kabisa CCM ipotelee mbali.Kwa mahali CCM ilipofikia sasa,it can't reform it has to go.
 
Back
Top Bottom