Sasa nimeelewa mwongozo ( blue print) ya Tanzania ya viwanda ya Rais Magufuli, watanzania tumuunge mkono

Ayubu Massau

Member
Apr 24, 2015
16
43
SASA NIMEELEWA MWONGOZO ( BLUE PRINT) YA TANZANIA YA VIWANDA YA RAIS MAGUFULI ,WATANZANIA TUMUUNGE MKONO.

Ndugu ,

Watanzania Na Wanabodi

Huu ni mwaka mpya wa 2018, ambao sasa ndio mwezi wa nne umeanza ukiwa mbichi kabisa , lakini mwaka huu unasogeza mbele na kutuelekeza tukiwa tumebakiwa na miaka takribani 7, kukamilisha dira ya maendeleo ya taifa mwaka 2000-2025.

Katika dira hii inatuelekeza tanzania kufikia uchumi wa kati na kutoka kundi la nchi maskini duniani ifikiapo 2025.

Sasa naweza sema nimeelewa mwongozo(blue print) ya Tanzania ya viwanda ya rais Magufuli na kama watanzania wengi tukimuelewa tutaenda sawa ,

Blue print ya Tanzania ya viwanda iko tofauti kidogo na nchi zilizofanikiwa kiviwanda , na huu ni mtizamo wangu kwa nilivyoanza kuifatilia toka 2015,rais Magufuli aingie madarakani

Nchi nyingi kama sio zote zilifanikiwa kiviwanda kwa kufuata njia zifuatazo;

1. Proto-industrialization- Hii ni awamu inayoendeleza viwanda vya maeneo ya vijiji kwa kufanya biashara na wafanyabiashara wanaotoka maeneo ya mbali ili kukuza soko.

2. First industrial revolution –Hii awamu ilibeba dhana ya kuzalishwa bidhaa nyingi kwa ajili ya soko kubwa.

3. Industrial trinity boom- Hii awamu ilibeba dhana kuu tatu ambazo ni kusambaza nishati, usafirishaji na miundominu itakayotumika kufikisha bidhaa katika masoko.

4. Second industrial revolution- hii awamu ilihusisha muunganiko wa uzalishaji wa kiwango kikubwa wa bidhaa ukienda sambamba na uzalishaji wa kiwango kikubwa wa zana za kilimo.

5. Welfare stage-Hii awamu ilihusisha masuala kama vile , bima ya kukosa ajira, usawa katika upatikanaji huduma za afya na elimu, upatikanaji wa vyandarua kutunza afya za wananchi na magonjwa kama malaria , demokrasia ,haki za binadamu, haki ya kupiga kura,haki za msingi mfanyakazi anapofia kazini na kutambua ndoa za jinsia moja n.k.


hizo ndizo njia kuu tano ambazo nchi hasa za Ulaya ,Japan, Korea Kusini Na Marekani zimepitia katika , kukuza uchumi wa viwanda na zilienda kwa kipindi flani ndio hatua inayofuatwa inaanza kutekelezwa.

turudi tanzania kwa nchi yetu, rais magufuli ukimfatilia utakubaliana na mimi kawekeza nguvu kwenye njia inayoitwa “INDUSTRIAL TRINITY BOOM” njia hii katika ukuaji wa viwanda imejikita katika kutengeneza miundombinu mbalilmbali ambayo ni;

1.Nishati(energy)- Umeme wa maporomoko ya maji ,mfano stiglers gorge(2100mw), gesi asilia n.k ,

2. Usafirishaji(transportation) -Barabara za lami, meli na vivuko katika maziwa makubwa yote, ndege za abiria na mizigo(atcl).

3. Reli (locomotive)- Ujenzi wa reli ya kisasa sgr(standard gauge railway), ukarabati wa reli za mgr (metre gauge railway) hizi mgr ni kama kukarabati reli ya Arusha ,Tanga ,Musoma

Ukitazama kwa makini , hii industrial trinity boom , ni njia pekee ambayo itasaidia kufanikishwa kwa kiasi kikubwa njia nyingine zote zinazobaki katika kufika Tanzania ya viwanda na hii njia inatekelezwa na serikali kwa asilimia 100% ,

njia nyingine zilizobaki kama , Proto-industrialization, First industrial revolution, na Second industrial revolution hizi zinatekelezwa kwa pamoja kwa ushirikishaji wa sekta binafsi, wakulima na serikali kutoa msaada wa mazingira wezeshi, mfano kwa wakulima ni kuwapatia mbegu na mbolea za ruzuku katika kutimiza malengo, leo hii serikali imeweka mazao ya mkakati naweza sema mazao ya kitaifa , mazao haya ni kama pamba , korosho,alizeti n.k jumla yapo matano , ukiangalia mfano zao la pamba sasa linalimwa karibia nchi nzima lengo ni kuzalishwa pamba ya kutosha ili sekta binafsi zinapoanzisha viwanda vya textiles (nguo) zipate malighafi za kutosha na hii itapeleka 2019 kusitisha kabisa mkataba wa AGOA( African Growth and Opportunity Act) ambao ni mkataba unaoruhusu mitumba kuja kwetu sababu hatuna uwezo wa kuzalishwa nguo zetu ,viatu n.k.

Hii itasaidia kukuza uchumi kuanzia kwa wakulima ,kutengeneza ajira viwandani, ginnery n.k na kuongeza kipato kwa serikali na kupunguza umaskini ,pia kwenda na ongezeko la watu jumuiya ya Afrika Mashariki,nchi za SADC na sasa soko la pamoja na huria la Afrika ambapo makubaliano yamesainiwa Rwanda hivi karibuni.

Upande wa zao la korosho ni kuongeza pesa za kigeni na kufanya nchi ijiendeshe na ikiwezekana turudi kwenye namba yetu ya awali miaka ya nyuma kama nchi mzalishaji wa korosho kwa wingi duniani na kuwapita vietnam wanaoongoza duniani kwa sasa ambao miaka ya 1970s walikuja kujifunza kwetu kuhusu zao la korosho kule naliendele Mtwara.

Vilevile bomba la gesi linatufanya kuwa katika hali nzuri zaidi kwani likikamilika toka Uganda kuja Tanzania , kuna nchi zinaweza kuunganishwa na kuchochea ukuaji uchumi zaidi ,mfano Sudan Kusini, Rwanda hadi Kongo(kinshasa), hapo vilivile tukumbuke nchi ambazo ni landlocked kama Malawi sasa wanataka kuunganisha bomba la gesi toka mtwara hadi Malawi ili wapate umeme wa uhakika.

Welfare stage , hii hadi sasa inatekelezwa cha msingi ni kuoboresha na kuendelea kutoa huduma bora zaidi , lakini kukua na kuiamarika kwake inategemeza zaidi kuimarika kwa njia hizo nilizozitaja hapo juu mfano sasa upatikanaji wa madawa hospitalini ni wa kiwango kikubwa n.k.

Hivyo naweza kusema hadi kufikia 2025 , naamini tutakuwa tunaongoza kama nchi yenye uchumi mkubwa afrika mashariki na hizi dalili zimeshaanza onekana kwa nchi jirani , hadi wachumi wakubwa kama Dr David Ndii wa Kenya wameshaliona , na kufikia 2025 tutakuwa tumeshatoka rasmi kwenye kundi la nchi masikini, kwa mujibu wa makabrasha ya uchumi inaonesha miaka ya 1990 , uchumi wa kenya ambao ndio unaongoza Afrika Mashariki ulikuwa mbele ya Tanzania kwa asilimia 30(30%) , lakini leo kwa kutumia mlinganisho wa PPP uchumi wa Tanzania na Kenya uko sawa na miaka ijayo tutakuwa tumewazidi.

Kijiografia na Kihistoria Tanzania tupo kwenye nafasi kubwa sana ya kufanya maajabu kama china ilivyofanya maajabu na hadi kufikia 2030 naamini zile 17 SDGs( 17 sustainable Development Goals) kama nchi tutakuwa tumezifanikisha na inaweza kuishangaza zaidi dunia kama China ilivyoshangaza dunia kukua kwa kasi katika uchumi.

Nimalizie kwa kusema kuna haja ya kutambua sasa tuko katika nafasi gani kama nchi , kwani welfare stage ambayo ni njia ya mwisho katika mapinduzi ya viwanda sisi tuliamua/kulazimishwa kuichukua bila kupita hatua za awali kwani katika hii awamu kuna mambo mengi yanayozuia kwa makusudi mapinduzi ya viwanda lakini ilikuwa haina jinsi , japo tumeishaichukua na tunaifanyia kazi lakini njia “Industrial Trinity Boom” ambayo sasa awamu ya tano imeichukua ni nzuri sana kwani unaua ndege wengi kwa jiwe moja.

Kipindi cha mtawala wa kifaransa ajulikanaye napeleon bonaparte aliwahi kunukuliwa akisema hivi kuhusu china , nanukuu “Let China sleep for a while, when the dragon awakes, she will shake the world” mwisho wa kunukuu , sasa tunajua yaliyotokea china kwa sasa ni historia na anasumbua dunia

Hivyo na Tanzania kwa kuwa imeshaamka ni suala la Muda tu kuisumbua Afrika na dunia kiuchumi kama tulivyosumbua wakati wa harakati za ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika.

Mungu ibariki Tanzania
 
Unaijua sera ya viwanda Tanzania?

Wakati wenzetu wamekimbilia “Information and Technology Industrialization” Sisi ndio tunaamka na viwanda uchwara. Hongera kwa kumwelewa mkuu.
 
Back
Top Bottom