Sasa nimeelewa kwanini Waarabu walituchukua kirahisi kwenda utumwani. Mke kupigwa na kukubaliana na mume anapoambiwa unaona umenifanya nikupige!

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Ulishawahi kusikia hadithi kwamba kuna wakati Waarabu walipata watumwa kirahisi kwa kutoa shanga na vioo kwa machifu wetu? Na pia kuna habari kwamba walitumia tende, wakawaonjesha watu tende, waliponogewa wakawaalika kwenda kweye merikebu zao za utumwa na kuwafungia huko, na kuishia kuwa watumwa na hata kuhasiwa! Kinachosikitisha zaidi ni kwamba watu hawakujifunza kutokana na wenzao kuchukuliwa utumwani huko nyuma - waarabu walirudi na bado wakabeba watumwa wengine kwa mbinu zile zile!

Hivi ndivyo nilivyoona Watanzania wengi wakichotwa akili na wagombeaji wa nafasi za kisiasa. Watanzania masikini sisi tunadanganyika na vitu rahisi sana na hata hatukumbuki tena ya nyuma. Hata kama huko nyuma tumeumizwaje, tukiambiwa tu mtapata hiki au kile basi tunasahau yote yaliyopita na kushangilia ahadi na kuona huyo ndio kiongozi wa kuchagua!

Watanzania kwa ujumla wananikumbusha kisa cha mwanamke anayepigwa na kunyanyaswa na mume, halafu kila akipigwa mumewe anamwambia si unaona sasa umenifanya nikupige, sipendi kabisa kukupiga ila wewe ndio unasababisha! Kisha mke anaomba msamaha kwa kumfanya mumewe ampige! Wapo wanawake wanapigwa kukaribia kufa na waume zao, na ndugu zao wanapowachukua kuwarudisha yumbani, utakuta baada ya siku chache wanasahau vipigo walivyopata kwa mume wanaanza kudai kurudi kwa mume. Wapo ambao hupoteza maisha kutokana na hili. Ukweli ni kwamba huu ni ugonjwa wa kisaikolojia.

Sasa watanzania tunakuwa kama watu wa kutekwa na waarabu kupelekwa utumwani, au mke wa kupigwa na mume na baada ya muda mfupi anasahau labda mume kasema basi nitakununulia bangili ya dhahabu.

Watanzania tujitafakari sana katika kuamua nani awe kiongozi wetu. Tusiwe wasahaulifu ka kuwa yajayo yanaweza kuliza sana - kipigo hata zaidi au kupelekwa utumwani ambako hata tutahasiwa. Inakuwaje mtu unaona hajafaa kabisa katika uongozi, amekuumiza sana, hajakujali, halafu wakati wa uchaguzi ukifika anakuja kukuomba kura unaanza kumshangilia?
 
Kama ulipelekwa utumwani unarudi kufanya nini kwetu huku afrika??

Nyie mlipenda kutumikishwa sababu mlikuwa wavivu msutuhusishe sisi hayatuhusu. Huku tulikataa bora kufa kuliko kuiacha africa
 
Back
Top Bottom