Sasa nimeelewa kwanini Diamond alimtunishia msuli Naibu waziri wa sekta yake, kumbe CCM bado ina wenyewe!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
34,203
2,000
Baada ya Waziri wa mazingira mh January Makamba kuweka wazi nafasi ya Diamond katika kampeni za urais mwaka 2015 nimeelewa ni kwanini Diamond huwa na jeuri hata anapozungumza au kujibishana na watu wa serikali.

Kitendo cha Platnumz kumtunishia msuli mh Juliana kilinishtua kidogo lakini baada ya ufafanuzi wa January Makamba kuwa hata kauli mbiu ya uchaguzi ilibidi ipitiwe kwanza na Dai na kuifanyia marekebisho madogi na kuwa Hapa Kazi Tu, imeonyesha umuhimu wa Diamond ndani ya CCM.

Wasanii ni nguzo muhimu, kumbe ndio maana Wema ilibidi apokewe na kamati kuu yote chini ya Mbowe siku anahamia Chadema.

Maendeleo hayana vyama!
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
5,040
2,000
Lumumba troll

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,777
2,000
Sasa ndiyo umeijua ccm, ccm inamuheshimu sana darasa la saba kuliko profesa wa uchumi kama wakina lipumba n.k.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom