Sasa nimeamini yule Bundi aliyetua Bungeni alikuwa na maana yake

Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,523
4,991
Katika Jamii zetu kuna imani mbalimbali zilizojengeka, mfano kuhusu Mnyama anaitwa KAKAKUONA, ndege anayeitwa BUNDI, na mdudu anaitwa KUNGUNI. Kakakuona akionekana huwa ni habari kubwa, na haminiwa kwamba ana uwezo wa kutoa ubashiri wa mambo yajayo. Bundi akionekana mahali huaminiwa kwamba ni ishara kwamba kuna jambo baya litatokea muda si mrefu. na mtu ukiambiwa una DAMU YA KUNGUNI, maana yake unaandamwa na lawama na kukataliwa na jamii bila sababu. Tatizo lako ni hiyo damu ya kunguni uliyonayo!

Hivi karibuni, tarehe 29 Januari 2019, tulipata taarifa kwamba Bundi alionekana katika bunge letu. Spika Job Ndugai alipotoa taarifa hiyo, alisisitiza kwamba Bundi ni ndege wa kawaida. lakini tarehe 6 Februari 2019, siku ya Mahakama, Rais Magufuli alimshauri Spika Ndugai apeleke viongozi wa dini wakaombee bunge ili asionekane tena. Inaonekana jambo hili lilimtisha Rais Magufuli. taarifa ya kuonekana Bundi ilijadiliwa sana kwenye mitandao ya jamii wakati huo, baada ya hapo maisha yakaendelea, watanzania kila mtu akipambana na hali yake.

Kufuatia matukio ya hivi karibuni, hususan uamuzi wa Bunge letu kupitisha azimio kutofanya kazi na CAG, pamoja na maamuzi mengine yaliandamana na uamuzi huo, likiwemo kuwafungia wabune Halima Mdee na Godbless Lema kuhudhuria mikutano ya bunge kwa muda tofauti, na pia vitendo mbalimbali vya kujenga chuki, vya dharau kwa watu mbalimbali. Hapa naongelea maneno ya kejeli aliyoongea Spika Job Ndugai, pale alipoamua kuongelea suala la Godbless Lema kujibizana na Naibu Spika, na kufikia hatua ya kutaja madeni ya Godbless Lema anayodaiwa, na kudai kwamba ndiyo sababu ya kumfanya aonekane kama "amechanganyikiwa". Kufuatia matukio yote hayo, nimetafakari sana tukio lile la Bundi kuonekana Bungeni.

Kwanza ni mara ya kwanza kusikia Bundi kaingia bunge letu, bila kukaribishwa kama alivyoalikwa Pierre Liquid na wengineo kabla yake. lakini pia ni mara ya kwanza bunge letu kupitisha azimio la aina hii, la kukataa kufanya kazi na CAG. kwa mujibu wa waliomnukuu spika wa zamani Pius Msekwa, uamuzi wa aina hii haujawahi onekana popote duniani. kwa hiyo tukubaliane kwamba hili pia ni tukio la pekee. Pia ni mara yangu ya kwanza kusikia mtu wa hadhi kama Job Ndugai kupandwa na ghadhabu na kutaja madeni ya mtu aliye chini yake akiwa na lengo la kumdhalilisha, na kumbe anajidhalilisha mwenyewe.

Siamini saana habari za bundi kuhusishwa na imani mbalimbali, lakini kwa hili, naomba kuweka tofauti. kwa hili tukio la bundi kuonekana bungeni na matukio haya ambayo yametikisa nchi na kutuingiza kwenye mgogoro wa kikatiba, nadhani Bundi alikuwa na ujumbe maalum kwa watanzania. Bundi alikuwa anatahadharisha kuhusu mambo mabaya yatakayotokea kupitia katika huo ukumbi wa bunge. Pamoja na Spika Ndugai kubeza uwepo wa bundi, na pia kubeza ushauri wa Magufuli wa kuleta viongozi wa dini waje kufanya maombi, mambo hayo mabaya kabisa yametokea.

Watanzania tusiache mambo haya kama yalivyo. tusimwachie CAG peke yake, au kuwaachia vyama vya upinzani peke yao. tunaona nguvu kubwa zinazotumika "kuwashughulikia" wale wanaoonekana kuunga mkono waziwazi kauli na msimao wa CAG. Watanzania kwa umoja wetu tujitokeze kupinga maamuzi haya ya kibabe, yaliyopitishwa na wabunge wa CCM, waliolewa madaraka na kujisahau kwamba wanatumikia wananchi. Mtumishi wa kweli wa wananchi, ni CAG na vyama vya upinzani.
 
mkuu bundi alikuja kuharibu mawazo ya wabunge wetu, sasa wananena maneno ya hovyo na wamekuwa watu wa hovyo... haiwezekani ukatae kufanya kazi na CAG then usifie mambo ya pierre liquid halafu uwe timamu..
 
Job ni mwanafunzi wa Mzee Msekwa, yeye ndo amemgroom Job, so asishangae, hiyo ni kazi ya mikono yake.
 
Hao ndio wawakilishi wa watanzania. Katika hili tukubali kwamba asilimia kubwa ya watanzania ni chini ya IQ 70; wapo wanaoshangilia kuona CIG anaadabishwa wakati alifanya kazi kwa ajili ya taifa.
 
Umeandika vizuri, ila naomba nikufungue macho kidogo kuhusu jambo hili.

Ukifuatilia au kuchambua nguvu ya kiroho kwa kila mbunge iliyotumika mpaka akawa hapo bungeni,ndipo unaweza kutambua nguvu iliyomvuta ndege huyu kwenye jengo la heshima kama tu ni kweli alikuwa ndege wa ulimwengu wa roho.

Mara nyingi nafasi za kisiasa tumesikia na kushuhudia zinavyotafutwa kwa ushirikishaji wa nguvu za kiza na matokeo ya kuzitafuta izo nguvu kama msaada yamekuwa yakionekana na hata kuwaumiza wanadamu wanyonge sana katika tabaka hili la Africa.Kwa awamu hii wote ni mashahidi kilio cha wenzetu kilipungua kwa sababu roho wa bwana aliingilia kati.

Kwa hiyo nguvu ya imani iliyotanda na inayotumika kwa waheshimiwa kama kinga na ulinzi wa vyeo vyao lazima ishara kama hizi zionekane ni jambo la kawaida tu.Asipoonekana Bundi ataonekana Nyoka mkubwa au wa maajabu fulani.Ishara kama hizi ni furaha kubwa kwa baadhi ya wahe.wakiamini wametembelewa na wazee na ni ishara ya kujiamini kwa kuwa Mungu wao yu pamoja nao.

Lakini pia nguvu ya kujitokeza kwa ndege huyu inaweza kutokana na vita ya walio nje na walio ndani.Hapa unakuta wote walio nje na walio ndani wana imani moja ya giza ila wametofautiana kutokana na tamaa zao.Kwa hiyo inakuwa ni ishara kwa upande mmoja kwamba vita ameshinda au anaelekea kushinda.

Uwezi kukuta Bundi au nyoka anajitokeza kwenye sehemu ambayo washirika wengi wana imani ya kweli kwa Mwenyezi Mungu.Ni lazima pawepo na watu wanaamini katika nguvu ya giza ndio utaona ishara hizo.

Umetaja matokeo ya kuonekana kwa ndege huyo,unaweza ukawa sahihi,ila si lazima hayo matokeo yaletwe na ishara hiyo.Nguvu inayotokana na dhambi ipo tu toka kuumbwa kwa ulimwengu,wala si shetani ameiumba.Shetani kazi yake ni kutushawishi tuiguse hyo nguvu kwa imani ambapo itatoa matokeo ya uaribifu mara moja.
Kama huyu Bundi katokea alafu ikakutwa hakuna anaye amini kwenye uwepo wake ,hata akitokeo kila siku hakuna kibaya kinachoweza kujitokeza.Pale imani yako ilipo ndipo na Mungu wako alipo.Kwa hyo usitarajie ukiweka imani kwenye Bundi utapata Amani kwa sababu Mungu wa Amani si Bundi,au Furaha kwa sababu Mungu wa furaha si Bundi.Kwa hiyo ni sawa kuonyesha kwamba mabaya yanakuja kwa sababu ya Bundi,ila kumbuka Mwenyezi Mungu ategemei Bundi kushusha kipigo ,huyo ndege hana nafasi kabisa labda dhambi ya kiburi,uongo,uonevu,uchoyo,wivu,ukabila, udini .Kwa hayo lazima kipigo kishuke.Bila kuyafuta haya kwa kuomba rehema usitarajie matokeo chanya.Kama Mhe.Raisi aliwasihi viongozi wa dini kuombea tukio hilo ni lazima walijikita kuomba rehema wala si ndege huyo kuonekana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi ya bunge ni kutunga sheria, kama watu hao wamefanyiwa maamuzi kinyume cha sheria nahakika kuna sheria wanayoweza itumia na kuisimamia kutafuta haki, ndio utawala wa sheria ulivyo (kama hawawezi kuzisimamia sheria walizotunga wenyewe, how do they expect watu wa kawaida wazisimamie??) . Kazi kubwa ya wananchi ni kuchagua mwakilishi anayefaa kuwawakilisha na kisimamia sheria ndio nguzo ya uwakirishi bora... Binafsi naona maombi yako yako kichochezi zaidi, chakufanya wananchi tuone mauzauza yanayoendelea na mwisho wa siku tuact katika uchaguzi wa wawakilishi.

Niko hapa naskiza wimbo wa senzo " who's gonna care"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeleta hoja nzuri sana na uchambuzi nzuri.

1, bundi Ndege,wachawi huenda sana kumtumi ktk mambo yao.
Kwaivo yule bundi inaweza kuwa wa ndugai,bashite na bwana yule ili kutimiza malengo yao, au alikuwa kutabiri tu,na kwamba mabaya yalikuwepo njia,hivo hata angeombewa akaondoka bado asingezuwia yasiteke.
Bwana yule hakujua cha kusema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Spika kapoteza uelekeo, Bunge linaangamia kwa kufanya maamuzi yatakayolighalimu Taifa.
 
Umeandika vizuri, ila naomba nikufungue macho kidogo kuhusu jambo hili.

Ukifuatilia au kuchambua nguvu ya kiroho kwa kila mbunge iliyotumika mpaka akawa hapo bungeni,ndipo unaweza kutambua nguvu iliyomvuta ndege huyu kwenye jengo la heshima kama tu ni kweli alikuwa ndege wa ulimwengu wa roho.

Mara nyingi nafasi za kisiasa tumesikia na kushuhudia zinavyotafutwa kwa ushirikishaji wa nguvu za kiza na matokeo ya kuzitafuta izo nguvu kama msaada yamekuwa yakionekana na hata kuwaumiza wanadamu wanyonge sana katika tabaka hili la Africa.Kwa awamu hii wote ni mashahidi kilio cha wenzetu kilipungua kwa sababu roho wa bwana aliingilia kati.

Kwa hiyo nguvu ya imani iliyotanda na inayotumika kwa waheshimiwa kama kinga na ulinzi wa vyeo vyao lazima ishara kama hizi zionekane ni jambo la kawaida tu.Asipoonekana Bundi ataonekana Nyoka mkubwa au wa maajabu fulani.Ishara kama hizi ni furaha kubwa kwa baadhi ya wahe.wakiamini wametembelewa na wazee na ni ishara ya kujiamini kwa kuwa Mungu wao yu pamoja nao.

Lakini pia nguvu ya kujitokeza kwa ndege huyu inaweza kutokana na vita ya walio nje na walio ndani.Hapa unakuta wote walio nje na walio ndani wana imani moja ya giza ila wametofautiana kutokana na tamaa zao.Kwa hiyo inakuwa ni ishara kwa upande mmoja kwamba vita ameshinda au anaelekea kushinda.

Uwezi kukuta Bundi au nyoka anajitokeza kwenye sehemu ambayo washirika wengi wana imani ya kweli kwa Mwenyezi Mungu.Ni lazima pawepo na watu wanaamini katika nguvu ya giza ndio utaona ishara hizo.

Umetaja matokeo ya kuonekana kwa ndege huyo,unaweza ukawa sahihi,ila si lazima hayo matokeo yaletwe na ishara hiyo.Nguvu inayotokana na dhambi ipo tu toka kuumbwa kwa ulimwengu,wala si shetani ameiumba.Shetani kazi yake ni kutushawishi tuiguse hyo nguvu kwa imani ambapo itatoa matokeo ya uaribifu mara moja.
Kama huyu Bundi katokea alafu ikakutwa hakuna anaye amini kwenye uwepo wake ,hata akitokeo kila siku hakuna kibaya kinachoweza kujitokeza.Pale imani yako ilipo ndipo na Mungu wako alipo.Kwa hyo usitarajie ukiweka imani kwenye Bundi utapata Amani kwa sababu Mungu wa Amani si Bundi,au Furaha kwa sababu Mungu wa furaha si Bundi.Kwa hiyo ni sawa kuonyesha kwamba mabaya yanakuja kwa sababu ya Bundi,ila kumbuka Mwenyezi Mungu ategemei Bundi kushusha kipigo ,huyo ndege hana nafasi kabisa labda dhambi ya kiburi,uongo,uonevu,uchoyo,wivu,ukabila, udini .Kwa hayo lazima kipigo kishuke.Bila kuyafuta haya kwa kuomba rehema usitarajie matokeo chanya.Kama Mhe.Raisi aliwasihi viongozi wa dini kuombea tukio hilo ni lazima walijikita kuomba rehema wala si ndege huyo kuonekana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Shukrani kwa uchambuzi mzuri. Kumbuka Mungu alimruhusu ibilisi katika umbo la nyoka amjaribu Eva. kumbuka pia kwamba Roho Mtakatifu alichagua umbo la Hua kujidhihirisha katika Maandiko Matakatifu. nataka kusema kwamba si kwamba bundi mwenyewe anaamua kujitokeza au ana nguvu fulani, bali kujitokeza kwake ni ishara kwamba kuna nguvu fulani zinataka kusababisha tukio fulani. wakati huu nguvu za giza zimewachwa zifanye kazi yake kuwarubuni watu, na japokuwa Mungu anatoa njia ya kuziepuka, anaziruhusu ziendelee pia na ni hiari ya mtu kuzikubali au kuzipinga. Nilivutiwa na tukio la Bundi kwa sababu ni la pekee na hili la CAG kuwa nalo ni la pekee. ndio maana nikataka tuangalie kama kuna uhusiano hapo
 
Back
Top Bottom