Sasa Nimeamini Mgawo wa Umeme Ulikuwa ni Man-Made. Long-Live Prof. Muhongo na Wenzio | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa Nimeamini Mgawo wa Umeme Ulikuwa ni Man-Made. Long-Live Prof. Muhongo na Wenzio

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NdasheneMbandu, Oct 30, 2012.

 1. NdasheneMbandu

  NdasheneMbandu JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 940
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wadau,

  Tuwe wakweli, kwa hali ilivyo sasa ya kutokuwepo kwa mvua na kusababisha mabawawa yetu kukosa maji, bila shaka hivi sasa tungekuwa hoi tukiogelea kwenye lindi la mgawo mkubwa wa umeme. Wapo ambao bahati mbaya hawataki kuamini kwamba mgawo wa umeme Tanzania ulikwa ni artificial kwa maana kwamba unatengenezwa na genge la wahuni na walafi wanaoshirikiana na wenzao wa TANESCO huku wakiacha watanzania wakiumia na kuteseka sana.

  Nakumbuka wakati wa sakata la kumsimamisha kazi aliyekuwa Mkurugenzi wa TANESCO Bw. Mhando ulitokea ubishani mkubwa kwamba Serikali imemwonea kwani tayari alikuwa ameruhusu umeme utolewe kwa mgawo. Mimi mwenyewe ni mojawapo ya watu waliopinga kusimamishwa kazi kwa Bw. Mhando nikiamini alikuwa ameonewa lakini sasa nimeamini kuwa mgawo wa umeme lilikuwa ni daraja la mafisadi la kupitishia fedha za walipa kodi wa nchi hii. Hapa lazima niwe mkweli, naanza kuwa na wasiwasi na credibility ya Zitto Kabwe na Kamati yake kama kweli nayo haikuwa miongoni mwa wanufaika wa mgawo wa umeme. Haiwezekani watu wachache akina Prof. Muhongo na wenzake including Katibu Mkuu Nishati na Madini waje na suluhisho la haraka kiasi hicho kama kweli mgawo ulikuwa unatokana na tatizo kubwa.

  Najua hatua hiyo imemjengea Prof. Muhongo maadui wakubwa kiutendaji ikiwa ni pamoja na Zitto Kabwe mwenyewe pamoja na wabunge wenzie. Lakini sisi wananchi wa kawaida tutaendelea kumwombea Prof. Muhongo na timu yake Mungu awalinde ili waendelee kupigania haki ya watanzania kwa mapana zaidi.
   
 2. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hata humu kwenyewe kuna watu hawataki kukubali kuwa mgao wa umeme haupo kisa eti maeneo wanayoishi umeme unakatika mara kwa mara. Ni bora ya umeme unaokatika katika ambao unaweza kurudi muda wowote kuliko kutangaziwa mgao rasmi. Hongera sana Prof kwa kuziba mirija ya wezi
   
 3. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hili kwa Bongo linawezekana. Kama wakubwa wako tayari kukodisha midege mibovu au mitambo ya kuzalishia umeme mibovu ili wapate chao wakikataa mipya na ya bei nafuu watashindwa nini kutengeneza mgao ili wahindi wao wauze majenereta yao? Kama watu wako tayari kununua rada mbovu ili wapate chao wakijua kesho itaharibika na kuwa hasara kwa taifa watashindwa nini kuanzisha mgao wa umeme ili bei za mafuta zipande? Hii ndiyo inafanya nisiamini hata daraja la Kigamboni maana litakuja ua.
   
 4. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Usichokifahamu kuhusu Tanesco ni kuwa, Professor keshapiga marufuku kutangaza mgawo. Mgao upo tena sana tu ila hairuhusiwi kutangaza kuwa kuna mgao isipokuwa unaruhusiwa kusema kuna marekebisho ya nyaya na kufunga kifaa sehemu fulani. Source: Ni rafiki yangu anafanya kazi tena ni one of the top guy in the company.
   
 5. h

  hamsinij JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 373
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wenzetu wanazungumzia energy mix na energy security. Sisi tunazungumzia mgao shame tz. Prof keep up brother. Mimi natumia solar for six yrs now tubadilike watz
   
 6. OMBUDSMAN mtoto

  OMBUDSMAN mtoto Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 28, 2012
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jaribio la kumlinganisha Prof Muhongo na Zitto kwa kweli linatakiwa iwekwe kwenye makosa ya jinai kwa kuwa ni watu walisolinganishwa kabisa!! Wakati mmoja ni mtendaji aliyeaminika (duniani) mwingine atafuta misifa tu kila kukicha; wakati mwingine anajulikana misimamo yake mwingine ni kigeugeu hata chamani kwake wanamshutukia; wakati mwingie yuko tayari kupambana na mafisadi bila uwoga mwingine amerudisha majembe nyuma na amejiunga na mafisadi tofauti na alivyokuwa. We are sio sad na jinsi Zitto alivyotulet down maana mimi nilikuwa namkubali sana huyu kijana na sijui nini kimembadilisha hivyo.

  Muhongo lazima atakuwa na maadui wengi kama ambavyo, Mwandosya na hata Magufuri wamekuwa na mapambano katika nchi yetu yenye mafisadi kila kona. Kazi yetu sisi wananchi ni kuwazomea hao wanaowadharau watu wanaotaka kutupunguzia kadhia dhidi ya maisha ya kimaskini wa kujitakia katika nchi tajiri. haijarishi mtu yuko chama gani, ukimpinga mtu tunayeona anatusaidia basi hata Mungu naye atakuaibisha!!
   
 7. NdasheneMbandu

  NdasheneMbandu JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 940
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  The top guys ndiyo haohao waliokuwa wananufaika na mgawo wala siyo watumishi wa ngazi ya chini. Kwa hiyo, sishangai taarifa aliyokupatia kwamba eti Prof. Muhongo ameamuru ukweli upindishwe.
   
 8. K

  Kulya JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 339
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  He hee... Bwana mkubwa... eti top guy?! He hee... Huyo ni mmoja ya hao viongozi waandamizi wa juu wanaopanda mgawo... Shame on him! Poor him, kama vile hakuzaliwa Tanzania akakua na watanzania kama sisi leo ni moja ya mijitu inayopanda mgawo feki! Kimsingi MGAWO wa umeme haupoooooo!!! Na kwa baadhi ya miji inayokatiwa kwa muda ni kwa masaa tu, unarudi. Na taarifa inatolewa na sababu wanatoa. Acha unafiki wewe, kama kwenu hakuna umeme basi hujawasha tu au hujanunua au na wewe umo kati ya waunda mgawo. Poor you and him (your top guy)
   
 9. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  sio kwamba ni mmoja wa mafisadi ndani ya tanesco?
   
 10. O

  Original JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mgao wa umeme umeleta hasara kubwa sana, hii ni kuanzia vifo hadi izalishaji viwandani. Uchumi wetu uliyumba sana tokana na mgao huo. Ninaishauri serikali kwamba waliosababisha mgao huo kwa lengo la kujipatia pesa wanyongwe hadi kufa mara moja. Hii ikiwa ni sambamba ni wale wanaotengeneza na kuuza ARV feki.
   
 11. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Mimi ni mnazi na mfuasi wa fikra pevu,prof. muhongo alisema kweli tupu jana,hakuuma maneno japo hakutaja moja kwa moja wahusika,japo kiutu uzima ni wazi ndani ya muda mfupi kapata maadui wengi sana.pia nilichopenda alisema yeye hawezi kusaini kitu chochote pasi kusoma na mambo mengi angependa kushirikisha wadau i.e wananchi,akaeleza umeme unaozalishwa kwa gas,maji na mafuta mazito pia makaa ya mawe,na kama mitambo yote ikiwashwa tunaweza kuzalisha umeme zaidi megawatt 1300 kitu ambacho ni zaid ya matumizi yetu ya megawatt 800,kimsingi kama asingalikuwa mkweli asingethubutu kueleza mbinu ya kuleta mgawo wa umeme kuhujumu shirika na watz kwa jumla,mh.zitto nilimjengea mashaka siku nyingi kwa kuwa kichwani kwake hufikiria anawezaje kupata kusifiwa ama kuonekana,kitu ambacho kinamgharimu na kwakweli asipokuwa makini ataporomoka kwenye medani ya siasa kuliko anavyotegemea.

  Moja ya maeneo ambayo kama watz na serikali yetu hatukupaswa kuletea mzaha ni kwenye umeme,power is a unit of development so kuchezea eneo hili ni kuporomosha uchumi,wawekezaji wengi tumeona wakidemand kuondolewa kodi fulani fulani ikiwemo ya kuingiza mafuta mazito ya kuendeshea mitambo migodini na maeneo mengine kiasi cha kutupotezea mapato makubwa,wengine wanashindwa kuwekeza kwa kutokuwa na uhakika na umeme n.k,tunahitaji kuwa waungwa kwenye mambo yanahusu nchi.kama mtz nampa pongezi za dhati prof. muhongo kwa walau ktk kipimdi kisichozid miezi sita kubaini tatizo na kushughulikia pasipo kumwogopa yeyote.naamini tanesco itaimrika na haitojiendesha kwa hasara tena kama wezi wachache walivyotaka kutuaminisha na tutakwenda hasa kupunguza gharama za nishati ya umeme ili mpaka vijijini tuweze kupata umeme.
   
 12. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Prof.muhongo azuie kutangaza mgawo wa umeme kwa manufaa ya nani?yeye wasipotangaza mgawo wa umeme ananufaikaje?nadhani amewagusa penyewe mmeanza kuhanyahanya,who is the top guy by the way?tangu prof.muhongo ameingia sijaona mgawo wa umeme mimi,kwangu umeme ukikatika labda two hours na vinginevyo tanesco wamekuwa wakitoa taarifa kama watakata na sababu wamekuwa wakiainisha,tuache uzushi wakuu.kama huyo top guy ana hakika na anenalo mwambie akaombe dk 45 itv mi na wanakijiji wenzangu tutazilipia akaseme kuwa prof.muhongo ni mwongo.tumekuwa tukilia na kujuta ktk awamu ya nne kwasababu ya watu wachache,waroho,wachoyo,wabinafsi,mafisadi wakubwa kwao umimi mbele.kujiona wao ndo wenye haki ya kuchezea rasilimali na kila upenyo wa kuiba wao ni kukwapua.huyo top guy pia aseme mipango mizuri aliyomsikia prof.muhongo amelitaka shirika kufanya ili tuone yeye hasukumwi na njaa ama kisirani kwakuwa kitumbua kimetiwa mchanga.
   
 13. MWILI NYUMBA

  MWILI NYUMBA JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 819
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35

  Huyo aliyekwambia itakuwa amesahaulika kwenye lile fagio lililowapitia wakina Mhando na wenzake,kama ni top guy lazima na yeye ni miongoni mwa wale mafisadi waliotajirika kwa kutuweka gizani makusudi!
   
 14. K

  Kimla JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 8, 2008
  Messages: 1,497
  Likes Received: 1,370
  Trophy Points: 280
  Ngoja tusubili ujinga wa kamati ya Gwiliza unaopendekeza kuwa prof awaombw ladhi wabunge eti kwa kuwa alisema kunawatu wanamaslahi na Tanesco.Wabunge watakaomrazmisha prof kujiudhuru ili waendele kufisadi, tutapambana nao.Hatutajali wabunge hao kama wanatoka upinzani and CCM.Mimi naishi Shinyanga, umeme unakatika kwa mda tu huwezi kulinganisha na mwaka jana hali ilivyokuwa.
   
 15. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Ukimtaja Zitto, binafsi nafumba macho kwa aibu! Anaendelea kuwa mtu anayepungukiwa ufahamu kadri siku ziendavyo. Nadhani ni sahihi atafute kazi nyingine kwa wajerumani kuliko kuhangaikia siasa ambayo hana njia ya kueleweka.

  Ni kawaida ya mwanasiasa yeyote anayekuwa na 'bei'. utamnunua na kumtupa ukimchoka.
   
 16. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Prof. Muhongo anastahili sifa kwa kuonyesha uwazi ktk suala la mgao wa umeme na tabia yake ya kuchukia waharibifu ndani ya Tanesco. Tumekuwa tukimpa sifa na naamini amekuwa akizipokea lakini nahisi anaanza kulewa sifa au kama siyo hivyo, bado hajatofautisha tabia aliyokuwa akiwaonyesha wanafunzi pale chuo kikuu na ile inayostahili kuonyeshwa kwa jamii nje ya vyuo.

  Jana tar.29 October nimemsikiliza Waziri wetu ktk kipindi cha dk 45 ndani ya ITV. Nilichokisikia nahisi ni kulewa sifa kwa waziri huyu. Naona anaelekea kuwa na dhalau kwa kila mtu anayempa maoni kinyume na fikra zake. Anaweza kuwa sahihi kwa jinsi nchi hii ilivyo kwa sasa hivi. Binafsi siamini.

  Kibaya nilichokisikia ni maneno kwamba kuna watu aliowaita wanaingilia kazi yake kwa kutoa uelewa wao wakati wana vyeti alivyoviita “certificate of attendance.” Maoni haya aliyarudia mara mbili ikanipa ‘picha’ kwamba ni maneno aliyoyatunga kabla ya kuingia studio.

  Kwa maoni yangu Waziri huyu anajaribu kutishia yeyote mwenye elimu chini yake asitoe maoni. Nionavyo mimi, Elimu ya vyeti aliyonayo Profesa huyu, sidhani kama ni ishara ya ufahamu wake ktk kila kitu. Hata alivyojieleza jana kuna mengi aliyoonyesha hana ufahamu wa kutosha. Kwa mtindo wake huo nadhani anajaribu kuifanya nchi yote kuwa ni Darasa la Nishati na madini jambo ambalo hatulikubali maana wapo wengi wenye ufahamu kuliko yeye.

  Tabia ya umwamba wa kielimu anayoonyesha, NIMEICHUKIA!
   
 17. kaangwa

  kaangwa JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 644
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Huyo "one of the top guys in the company ''ni mmojawapo wa mabaki ya akina Mhando,alikuwepo kwenye kampuni na kampuni ilikuwa ikifanya vibaya mpaka pro. alipoingilia kati.Kila mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi hii hawezi kuacha kuwapongeza Pro.Mhongo,Magufuri,Mwakyembe na Mlugo kwa kazi wanayoifanya.mimi nimfanyakazi mmojawapo wa taasisi zinazofanya kazi kwa ukaribu na TANESCO najua shughuli anayoifanya Prof.na wasaidizi wake baadhi kuhakikisha nchi haipo gizani, tena kwa nia thabiti.WTZ tumuunge mkono bila kusikiliza propaganda za wanaotaka kuwaaminisha mamilioni ya watanzania kwamba TANESCO imeshindikana.
   
 18. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #18
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,739
  Likes Received: 8,005
  Trophy Points: 280
  Mkuu NdasheneMbandu, nimeamini kweli penye wengi hapakosekani mengi, mimi binafsi hapa sikuwahi kulifikiri hilo na sasa umeniamsha.

  Ni kweli kwa kuzingatia matukio ya nyuma basi saa hizi tungekuwa gizani. Kwa kweli hawa tuliowaamini tunapaswa kuwatazama upya. Leo hii wakati bunge limeanza, tutashuhudia unafiki mwingi na hatma ya Kamati ya Bunge ya kuchunguza tuhuma za rushwa ikibakia kuwa kiini macho kama ilivyo desturi.

  Huyu Zito huyu, nina mashaka. Kuna wakati huwa napata mashaka kuwa labda ni usomi tu ndio unamfanya asiwe wazi kama Shibuda
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,739
  Likes Received: 8,005
  Trophy Points: 280
  Kweli akili nzuri ukiwa nazo. Sasa wewe unaamini nini zaidi, kauli ya jamaa yako MR.TOP GAY au kuona umeme unawaka?

  Unanishangaza kuukataa ukweli sababu kuna mtu unayemwamini wewe kasema vinginevyo. Ni ujuha sawa na kuniambia kuwa leo hakutakuwa na mvua wakati hapo tunapoongea tayari tumelowa mpk chupi na bado inatunyeshea.
   
 20. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #20
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,863
  Likes Received: 3,308
  Trophy Points: 280
  Kuna majizi na washabiki wa majizi zitto ni Shabiki
   
Loading...