'sasa ni zamu ya mhe pinda, na yeye apigwe tu!!!'

Rose Mayemba

JF-Expert Member
May 7, 2012
721
1,000
Tangu Mhe Pinda awe Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumekuwa na sintofahamu kubwa sana juu ya utendaji wa wale anaowaongoza na kuwasimamia( yeye akiwa kama kaka mkuu).

Tumeshuhudia Twiga wakikunjwa kama karatasi huku wakiwa wamepuliziwa madawa ya kulevywa na kupelekwa ughaibuni chini ya usimamiza wa mheshimiwa huyu..

Tumeshuhudia watu wakijibatiza ubilionea kwa kuuza meno ya tembo na kuyasafirisha bila hata uoga huku watanzania wengi wakilia hali ngumu ya maisha yeye akiwa amejivika kofia ya mtoto wa mkulima.

Aliipokea nchi yetu ikiwa katika giza nene, bahati mbaya ameendelea kuitokomeza na kuipeleka kusikojulikana kwa maslahi ya waliompa dhamana..

Tunaowaona wanajiuzulu na wengine kutenguliwa nyadhifa zao ni kwasasabu ya utendaji na ufuatiliaji mbovu wa kiongozi huyu( japo kujiuzulu kwao hakuna tija kwa taifa) na watanzania hatuko tayari kuyavumilia haya.

Na kwasababu ameshindwa kuwajibika, na hana uhakika wa kufanya jambo lolote lenye manufaa kwa watanzania

Na kwa sababu ameikosea ardhi pamoja na viumbe vyote vilivyomo na mimi nashauri na yeye APIGWE TU..

EE APIGWE TU...TUMECHOKA SASA.
 
Jino Kwajino

Senior Member
Dec 22, 2012
191
0
Apige chini tu maana hatuna namna nyingine. Ameambiwa asimaie kazi kiuadilifu halafu yeye anajifanya jeuri zaidi anaamuru watu wauawe, watu wapigwe anshuhudia upotevu wa mali za umma na uingizwaji wa dawa za kulevya apige chini tu. Maana lazima tukubaliane nchi hii inaongozwa kwa misingi ya kisheria ee maana tumemchoka sasa.
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,891
2,000
Yaani nimecheka sana. Eti Wakati wa Pinda Twiga wamepindwa? Ah kwani sakata la twiga limetokea wakati wa pinda?
 
Mkuu, Pinda hana shida na uwaziri mkuu. Last week alibainisha kuwa hata kama wabunge wataamua kuchukua hatua au Rais, yeye hatachukia sana sana ahtafurahi tu. sasa wabunge mbona hawatumii fursa hiyo? Pinda ni Mtani Jembe
 
bily

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
8,032
2,000
Yaani nimecheka sana. Eti Wakati wa Pinda Twiga wamepindwa? Ah kwani sakata la twiga limetokea wakati wa pinda?

ndio alikuepo huku waziri akiwa Maige . Pinda ni mzigo zaidi ya hile ujuayo. I think he should go.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom