Sasa Ni wazi uchawi hakuna tatizo Ni umaskini na maradhi

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,557
44,744
Wale wanaoendelea kuamini mambo ya kijinga wanazidi kuabika kwa sababu ukiuliza Watu kumi wakutajie tatizo kubwa linalowakabili watakwambia kuwa hawana pesa au wanaumwa ugonjwa fulani gakuna ambaye atakwambia kalogwa kwa sababu Majibu ya maswali yote yapo tayari maarifa yanasema wazi ukiumwa ukafa ukafanyiwa uchunguzi wanajua Kama Ni pressure imekuua wanasema watalaam Sasa imejulikana zamani Watu walikuwa hawajui vyanzo vya vifo hivyo wakaamua kusema Ni uchawi ndo unasababisha.
 
Kwani uchawi unauelewa vp mkuu? Kwahiyo kama mtu kamfanyia mwenzie uchawi wa kuuwa kwa ajari ndio unataka maiti ipimwe na kukuta chanzo cha kifo ni chawi?
 
Ajali Ina sababu zake
Sasa ndio hizo sababu zinasababishwa na uchawi,ndio maana nikatoa huo mfano wa mtu kufanya uchawi wa kumuuwa mtu kwa ajari kwa maana tutaona kabisa chanzo cha ajari ni sijui gari ilifeli break ila uchawi ndio umesababisha hayo.
 
Ajali inasababishwa na
1.ubovu wa miundominu
2.kukosa umakini
3.ulevi
Na haina maana kwa kuwepo hizo sababu basi lazima ajari itokee,kuna watu wanaendesha gari huku wamelewa na wanaendesha vizuri tu hawajawahi kupata ajari. Sasa mtu kama huyo akifanyiwa uchawi afe kwa ajari unategemea chanzo kitaonekana nini kama sio ulevi?
 
utakua umelogwa wewe,au elimu ya kukremisha inakuchanganya ,au hujatembea, au umezaliwa kuanzia 1995..,na mwisho au umezaliwa mjini ambapo si uswazi
 
hakuna uchawi

uchawi ni ujanja kwa watu wajinga, utapeli na ulaghai kwa watu wasio na akili.

Mtu aliyekuzidi ujanja akifanya jambo lisilolingana na akili yako ndio wengi huita uchawi.
 
Ndugu uchaw upo mimi ni shuhuda wa haya mambo matatu uko nyuma katika mkoa wa nyumban kigoma
Tukio la kwanza ni mimi kuona msukule wazi wazi kwa macho yangu kagongo mida ya saa 8 Mchana ukiwa na nywele ndefu ukitoka ndan ya maji na kwenda nchi kavu sehem io sio makazi ya watu Kwan nilikua Napita na boat na niliuona peke yangu wakat wote tulikua tunaangalia ule Upande


Pili tukio la mama yangu mdogo kuelea angani mwaka 2001 mkoan kigoma ujiji swahili ilikua majira ya saa 10 usiku mama mdogo alikua kagombana na wenzake na wakaahid kummaliza mama mdogo alianza kwa kuumwa vibaya siku kama tano kabla ya tukio na alitakiwa afe kabla ya siku Tatu Sema marehem bibi nae hakua wa mchezo mchezo nilishuhudia usiku ule ambao ulikua wa mwisho kwa mama mdogo akielea angan na asubui yake akafa ilikua jmos
Kwa anae pajua ujiji mtaa wa swail karibia na fund redio au mwalim sufian


LA Tatu ni mimi na vijana we zangu watatu
Mrisho suma Amri kufatwa na jin miaka io na lilikua linakimbia hewan na haikua na sura usiku hii ni baada ya ndugu yetu Amri kuiba nazi ya Mganga wa kienyeji yenye dua na Kuja nayo hom wahun tukaila uzur yule Mganga alijua kua ni tatizo kubwa akawa anatangaza mtaani uzur mama yetu mdogo alikisikia na kumfata Mganga ila Mganga akasema amechelewa Na inatakiwa awahi nyumban atupeleke kwenye nyumba yenye kisima cha maji ya Bata wanayo wekewa chakula tunywe Yale maji kama adhabu ukwel siku Ile sito I sahau

Niwapongeze tukio na matukio yangu yote ni kwel sababu nakutajia had eneo uende ukaulize chukua na hii

Kuna dogo mmoja alikua anaitwa Amri manyoka wa Kibirizi alikua kaenda ujiji kujifundisha uganga siku moja alitokea mgonjwa alie rogwa kwa kutupiwa jin kali yule mgonjwa alipo fika pale kwa Mganga Mganga akapima akaona lile jin haliwez sababu akilitoa toa tu basi na yeye anakufa kwakua alikua anataka hela akampa dogo msala na kwel dogo aliweza kulitoa lile jin ila dogo na yeye alifia pale pale ila mgonjwa alipona

Uchawi upo ila miaka hii hauna ngugu Tena huenda Kuna watu Wana pambana Uchawi wa muafrica upotee mimi Binafsi napanga niwatafute wazee wachawi wote waongee na mizim yetu tutumie Uchawi wetu kama teknoloji naamin itawezekana
 
Uchawi haupo. Ukishalielewa hili maisha yako yanakuwa ya amani kabisa, ukipata tatizo unatafuta sababu halisi kisha unakua na majibu kama unaweza kulitatua au la.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom