sasa ni wazi si kimya kimya kuna Mgawo wa umeme TZ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

sasa ni wazi si kimya kimya kuna Mgawo wa umeme TZ

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lukwangule, Mar 17, 2010.

 1. L

  Lukwangule Senior Member

  #1
  Mar 17, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kutakuwapo na mgao wa umeme katika mikoa yote ya Tanzania Bara kuanzia saa 12 jioni hadi saa nne usiku kila siku,Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco Stephen Mabada amesema leo.
  Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari alieleza sababu ya kuwepo mgao huo kuwa ni kuharibika kwa baadhi ya mitambo katika vituo mbalimbali vya kuzalishia umeme.
  Mitambo iliyotajwa kuharibika iko katika vituo vya kuzalisha umeme vya Kidatu, Kihansi, Pangani na kile cha Ubungo Gas Power Plant. Hata hivyo tarifa hiyo haikueleza kiasi cha megawati kitakachokosekana baada ya mitambo hiy kuharibika.
  “Athari za upungufu huo zimelilazimu shirika kuanza mgao wa umeme kwa maeneo mbalimbali wakati wa matumizi makubwa ya umeme kuanzia saa 12 jioni hadi saa nne usiku,” ilisema taarifa hiyo.
  Ofisa mmoja wa tanesco alikiri kuwa mgao ulishaanza wiki kadhaa zilizopita na walisita kutangaza kwa kuamini kuwa matengenezo hayo yangechukua siku chache.
  Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja alipoulizwa lini mgao huo utamalizika alisema hajui ila akasisitiza kuwa mafundi wako ‘site’ usiku na mchana kuhakikisha hali inatengemaa.
   
 2. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,389
  Likes Received: 3,706
  Trophy Points: 280
  Yaani mnaacha kutangaza kwa imani kuwa pengine tatizo litaisha mapema...!!! Kimsingi hata mkikata kwa dakika moja inabidi mtueleze na mtupe sababu
   
 3. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
 4. L

  Lukwangule Senior Member

  #4
  Mar 17, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sure hii ngoma noma kwelikweli unarejea nyumbani laptop nayo imebakiza nusu saa unachemka pwaaa.Si ajabu, lakini sijui inakuwaje nimeagiza wa nyumbani vile vibatari waviweke sawa manake nimeenda kuuliza sola jamaa weshapandisha leo leo tu hii hesabu haikubaliki
   
 5. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Duh! Sijui niahirishe safari? Manake nilikua napanga kuja huko.
  Mambo ya kuingia kitandani saa 12 noma.

  Na wale wapenda mpira, huu mgao ukiendelea hadi mwezi wa World Cup watoto watabaki na nani nyumbani jamani?

  Hivi, wanafahamu kuwa kuna kitu kinaitwa "service agreement"?

  Yaani mashine zote zinaharibika ghafla bin vuu kwa mpigo? Mh, hata mtoto mdogo hawezi kutunga kwa mtindo huu uliotumika na TANESCO!!
   
Loading...