Sasa ni wakati wa wananchi kufanya maamuzi magumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa ni wakati wa wananchi kufanya maamuzi magumu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Inkoskazi, Aug 19, 2010.

 1. I

  Inkoskazi Member

  #1
  Aug 19, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kumekuwa na vilio vingi kutoka kwa wadau anuai kumtaka rais achukue maamuzi magumu ili kuleta mabadiliko katika chama na serikali yake, lakini imekuwa ni kama kumpigia mbuzi gita kwani hakuna lolote lililofanyika na isitoshe wadau kadhaa wamekejeliwa na rais mwenyewe au kwa kupitia wapambe wake.
  Hivyo basi, sasa ni wakati wa wadau wote - mashirika yasiyo ya kiserikali, mashirika ya kidini, majukwaa yote (km: Mwl. Nyerere Foundation), wapiganaji wa haki za binaadamu, wananchi wote kwa ujumla ndio WAFANYE MAAMUZI MAGUMU hiyo Oktoba kwenye sanduku la kura. Hakuna nafasi adimu kama hii na amini nawaambieni tukishindwa kipindi hiki ndio basi tena, tuna kila sababu ya kuuangusha huu mbuyu uliokaa miongo kadhaa bila kutupatia matunda ya maana zaidi ya ufisadi na utawala mbovu. Tumejionea wenyewe jinsi walivyomalizana kwanye kura zao za maoni kilicho baki kwetu ni kumalizia tuu kama kumsukuma mlevi. Tuhamasishane tufanye kweli - nawasilisha.


  "Moringe wote ni wamasai lakini sio kila mmasai ni Moringe"
   
Loading...