Sasa ni wakati wa kuianika mikataba yote ya Magufuli kama wao walivyoanika mkataba wa Bandari ya Bagamoyo na mingineyo

Mkuu umeandika mengi ila ni upupu mtupu. Hao unaosema wamejitokeza ni kutaka kuhakikisha kuwa mweli kaondoka.

Ile misafara yote na mitutu ya bundiki haikuwa kitu mbele ya kifo. Alifikiri walinzi wote wale wangeweza kumkinga na kifo. Ninyi ndiyo mjitafakari ktk hilo.

Aliwananga sana watangulizi wake juu ya mikataba. Sasa tunahitaji mikataba yake nayo iwe wazi ili tuchekeche. Je alikuwa na uhalali wa kuwananga watangulizi wake??
Wanafiki sana hawa jamaa.Nakwambia ni CCM hawa hawa walioitwa majizi ndio watamuanika Magu na madudu yake.
 
Huu ndio ushauri wangu kwa serikali hii mpya ili tuone ni nini kimo kwenye hiyo mikataba na tukigundua ni mikataba mbovu; basi tuisitishe na kisha tuifumue kabla ya kuendelea nayo.

Tukumbuke ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ulifutiliwa mbali kwa hoja mkataba wake ulikuwa mbovu na baaadhi yawatu wakapongeza hatua hiyo.Sasa tujiulize, mikataba aliyoingia Magufuli tunaijua?Kama hatuijua, tuna uhakika gani haiwezi kuwa kama ile ya wakati wa Kikwete ukiwemo huo wa Bandari ya Bagamoyo?

Kwa msingi huo, nashauri mikataba ya Magufuli yote ichunguzwe na iwekwe wazi na pia tuanze sasa utaratibu wa kupitisha mikataba yote Bungeni na utaratibu huu uwe wa kisheria.

Uzalendo ni vitendo na sio maneno au propaganda za kisiasa.

Naunga mkono hoja.
 
Sidhani kama serikali inahitaji kufanyia kazi maneno ya mitandaoni,na kama wewe ni mmoja ktk viongozi yamkini ni mbunge tutaenda kusema bungeni huko

Tunachojua JPM alikua kiongozi shupavu na tutamkumbuka,hatuamini kama aliweza kua na makando kando

Nje na hivyo utakua unatupigia kelele tu

Kama hana makandokando kwanini alimfukuza kazi CAG profesa Assad!
 
Huu ndio ushauri wangu kwa serikali hii mpya ili tuone ni nini kimo kwenye hiyo mikataba na tukigundua ni mikataba mbovu; basi tuisitishe na kisha tuifumue kabla ya kuendelea nayo.

Tukumbuke ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ulifutiliwa mbali kwa hoja mkataba wake ulikuwa mbovu na baaadhi yawatu wakapongeza hatua hiyo.Sasa tujiulize, mikataba aliyoingia Magufuli tunaijua?Kama hatuijua, tuna uhakika gani haiwezi kuwa kama ile ya wakati wa Kikwete ukiwemo huo wa Bandari ya Bagamoyo?

Kwa msingi huo, nashauri mikataba ya Magufuli yote ichunguzwe na iwekwe wazi na pia tuanze sasa utaratibu wa kupitisha mikataba yote Bungeni na utaratibu huu uwe wa kisheria.

Uzalendo ni vitendo na sio maneno au propaganda za kisiasa.
"UBAYA UBAYA TU" - JPM.
 
Back
Top Bottom