Sasa ni rasmi Wafanyakazi wengi sekta binafsi 'tumelizwa' na serikali fao la kujitoa!

papason

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
5,119
5,683
Hatimaye msimamo wa serikali juu ya kupeleka marekebisho ya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii umeota mbawa rasmi baada ya kuthibitika rasmi mbele ya kamati ya kudumu ya maendeleo ya jamii ya Bunge iliyokutana na Kamati ya wafanyakazi wa migodini.

Imethibitika rasmi kuwa wizara ya kazi na ajira haijaandaa muswada huo, akitoa maelezo ya wizara mbele ya kamati katibu mkuu wa wizara hiyo ndugu shitindi amedai kwamba wizara ya kazi imejipanga kupeleka miscellaneous amendments kwa mwanasheria mkuu wa serikali badala ya kupeleka bungeni mswaada wa marekebisho ya sheria hiyo kandamizi iliyopitishwa na wabunge mwanzoni wa mwaka huu huko Dodoma. Pamoja na kubanwa kila kona na wanakamati wa wafanyakazi wa migodini, bwana shitindi alikomaa ‘kibabe’ kabisa kwenye msimamo wa serikali kupitia wizara ya kazi na ajira ni kupeleka miscellaneous amendments kwa mwanasheria mkuu wa serikali na si vinginevyo!.
Katika amendments hiyo katibu mkuu alisema kifungu kitakachorekebishwa ni kile Na.44 cha sheria ya PPF ambacho ndo pekee kitaruhusu wanachama wa PPF kuchukua mafao yao. Wanachama wa mifuko mingine kama NSSF fao la kujitoa halitarudishwa kamwe! Na hivyo sheria hiyo kubaki kama ilivyo kwa wafanyakazi waliopo kwenye mifuko mingine kusubiri miaka 55 au 60 kuchukua mafao yao.

Mwanakamati mmoja wa wafanyakazi wa migodini alitaka kujua ni kwa nini wizara imekaidi kuandaa muswada wa sheria kama ilivyo pendekezwa na bunge lililopita badala yake inaleta miscellaneous ammendments, mpiganaji huyo aliishia kupigwa ‘beat’ zito kabisa na katibu mkuu wa wizara ya kazi na ajira-Shitindi, tena huku akisaidiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya maendeleo ya jamii ya bunge.

Kwa kweli wafanyakazi na hasa wa sekta binafsi tujilaumu wenyewe, kwa maana hatuku- ungana wala ufanya jitihada kubwa ktk kutetea fao hilo, tuliiamini serikali na kamati ya bunge ambao nao wametuingiza mjini rasmi!

Matumaini yetu yamebaki kwa wabunge wachache wa upinzani kututetea!

Lakini bado wafanyakazi tuna nafasi ya mwisho na hasa tukiitumia vizuri kabla ya kuanza bunge mwezi ujao!


 
michango yetu ndo hiyo wanajengea madaraja na kwendea ulaya kupigana kavu....shenzi kabisa
 
Hivi wafanyakazi mbona hamuungani katika hili?
Naona mumewaachia sekta ya madini tu ndo wanapambana.

Wapi vyama vya wafanyakazi...TUICO, TPAW, FIBUCA, shirikisho TUCTA mbona kimya? Ni wakati gani mnapaswa kuwatetea wafanyakazi kama si sasa?
 
Tangu mwanzoni issue hii ilinisikitisha sana kwa namna tulivyo ichuilia kimzaa mzaa!

Sijui wafanyakazi uoga na unyonge huu utaisha lini?
 
Hivi wafanyakazi mbona hamuungani katika hili?
Naona mumewaachia sekta ya madini tu ndo wanapambana.

Wapi vyama vya wafanyakazi...TUICO, TPAW, FIBUCA, shirikisho TUCTA mbona kimya? Ni wakati gani mnapaswa kuwatetea wafanyakazi kama si sasa?
Nashauri hivi vyama vya wafanyakazi waanzishe petition online ambayo itasainiwa na wahusika wote ili kushinikiza mswada upelekwe kwa hali yoyote ile hata kwa dharura. Labda itasaidia kuamsha wote waliolala.
 
Upuuzi huu wa serikali umetugharimu wengine nafasi ya kujiendeleza kielimu Ilikuwa niprocess mafao yangu mwezi wa tisa.
 
Jamani tusiishie kunung'unika tu tuchukue hatua sio kazi ya kulalamika tu mitandaoni tusonge mbele
 
Back
Top Bottom