Sasa ni muda wa michezo mingine pia kupatiwa nafasi

Shareef Conscious

JF-Expert Member
Jul 19, 2016
522
338
Umuhimu wa michezo kwa miaka mingi umekua ukihusishwa na faida za kiafya, kujipatia kipato, kutambulika mahala tofauti Duniani na hata sifa nzuri kwa Taifa.

Kwa hapa kwetu Tanzania kwa miongo mingi sana Michezo imekua na umuhimu wa kipekee kwa upana wake hasa hasa kwa Taifa na wanamichezo husika.
Mchezo wa mpira wa miguu una nafasi ya kipekee, kwakuwa umekua ukipewa kipaumbele katika nyanja tofauti, ila matunda yake bado hayafanani na juhudi za makusudi na uwezeshwaji ambao umekwishafanyika mpaka sasa.

Naona sasa ni muda wa michezo mingine pia kupatiwa nafasi. Kuna michezo ambayo vijana ushiriki wao ni mkubwa lakini msukumo wa kuwawezesha Bado ni mdogo.

Michezo yenye nafasi ni kama:-

1. Masumbwi
2. Riadha
3. Mpira wa kikapu
4. Uendeshaji wa Baskeli n.k

Kama kutakuepo na jitihada za makusudi kabisa kutoka serikalini, wadau wa michezo, Taasisi binafsi na jamii kwa ujumla naamini michezo itakua ni dirisha zuri la kupunguza mdororo wa ajira na kuongeza pato kwa Taifa.

Makabila kama Wamasai ni watu wenye ustahimilivi mzuri ktk kukimbia umbali mrefu kutokana na Jiografia yao ilivyo. Rasilimali watu kama hii ni mwanzo mzuri wa kutengeneza msingi katika Riadha.

Wasukuma wana physic nzuri sana hasa ktk kulima na utumiaji wa usafiri wa baiskeli. Katika maeneo mengi ya wazawa wa kisukuma baiskeli inatumika si tu inatumika ktk kusafiria ila pia kiuchumi kama sehemu ya kujipatia kipato kwa kubeba abiria. Najua si wasukuma pekee ila yapo makabila mengine pia kama Wakurya n.k

Masumbwi vilevile ukiangalia utagundua kuna ongezeko kubwa la vijana wanaocheza ngumi zisizo rasmi. Hivyo ni sehemu nzuri ya kuweka mazingira shawishi ili kupata mabondia wa ngazi zote. Mabondia kama Mike "iron" Tyson, Pacquiao na Watu kama Sony Liston ni watu ambao walitoka ktk hali mbaya za maisha ya mtaani lakini wakafanikiwa kupitia Mchezo wa Masumbwi.

Kwa kifupi vipaji ni vingi sana, ila watu wa kutengeneza mipango madhubuti(STRATEGIESTS) ndio bado tatizo. Na si tu ktk michezo, hata ktk uchumi wetu ndio suala ambalo bado lina Ukakasi mno.

Muda si Rafiki,ingawa Roma haikujengwa kwa Siku Moja!!
TUJIPANGE
 
Back
Top Bottom