Miaka 20 baada ya tukio la kigaidi (home-grown terrorism) la September 11 huko Marekani. Tanzania imejifunza nini?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Habari zenu waungwana wa JamiiForums.

Itakapofika tarehe 11 mwezi wa September mwaka huu wa 2021, itakuwa imetimia miaka 20 kamili tangu siku majengo pacha ya kibiashara katika jiji la New York nchini Marekani yalipuliwe na magaidi (kulingana na taarifa kamili ya serikali yao) kwa kutumia ndege za abiria.

images.jpg


Sisi kama Tanzania tumejifunza nini ndani ya kipindi hiki cha miaka 20?? Je, bado wasanii wa nyimbo za kizazi kipya wanawaambia watoto wetu kuwa wapo bongo (Tanzania) kwa bahati mbaya? Do foreigners still corrupt the minds of our little ones?

Ustawi na usalama wa Tanzania yetu unaaza kwa kupandikiza mentality njema ndani ya akili za watoto wetu ambao ndio taifa la kesho.

Wazazi katika familia na viongozi wa dini huko makanisani na misikitini wakitimiza wajibu wao ipasavyo, wanaipunguzia polisi/dola mzigo mkubwa sana wa kupambana na magaidi/wahalifu.

Mfundishe mtoto tabia njema angali akiwa bado mdogo hata akija kukengeuka ukubwani kamwe hawezi kuyasahau yale mambo ya msingi katika maisha (S/he will never forget za basics)

Ninajua humu JF kuna wataalam sana wa masuala haya na wanaweza kuhoji kwanini tukio lile nimeliita kuwa ni "home-grown terrorist act" ilhali magaidi waliofanya vile walitokea nje ya taifa la Marekani, hususan Afghanistan pamoja na Pakistan.

Siku zote inasemekana, hakuna adui wa nje anayeweza kukudhuru kama hakuna adui wa ndani na waswahili husema kikulacho ki nguoni mwako.

Kabla ya kutokea kwa tukio lile la kugongesha ndege katika ghorofa pacha, wahalifu wale tayari walikuwa na watu wao ndani ya Marekani waliowasaidia kuwapa taarifa - carrying out surveillance - (watoto wa mjini wanasema kuchora rada) kabla ya kupanga mpango mzima wa kuteka ndege na kuleta msiba mzito ndani ya ardhi ya rafiki zetu wa Marekani.

Masuala yanayohatarisha usalama wa nchi hubadilika kulingana na wakati pamoja na hali ya kisiasa ya dunia kwa muda huo. Nimeamua kusema hivyo kwa maana kwamba siku hizi kumekuwa na matukio machache mno ya nchi moja kuivamia nchi nyingine moja kwa moja pamoja na yale ya kupindua serikali halali.

Kulikuwa na uhusiano mkubwa sana baina ya serikali kupinduliwa na siasa za vita baridi (Cold War Politics) kati ya kambi ya Magharibi na ile ya Mashariki enzi hizo.

Tangia kusambaratika kwa umoja wa USSR miaka ya 1990s, matishio ya usalama wa taifa yamehama kutoa uvamizi wa nchi moja dhidi ya nyingine na sasa ugaidi ndio umechukua nafasi. Watoto wa kihuni wanakwambia ndio habari ya mjini. Ugaidi sasa umekuwa habari ya mjini.

TANZANIA NI NCHI YA TATU KWA UPELELEZI DUNIANI

Kwa wale vijana waliozaliwa miaka ya 1980s kama mimi ninadhani hii kauli si ngeni kabisa masikioni mwao.

Tanzania kuwa nchi ya tatu kwa upelelezi duniani ni kauli ambayo sisi watoto tuliyoisikia na kuiamini kutoka kwenye vinywa vya wakubwa zetu (wababa na wamama) kwa miaka nenda rudi.

Ni kauli ambayo iliwafanya vijana na watoto kutembea vifua mbele kwamba wanaishi ndani ya taifa lenye nguvu kuzidi nchi zingine mbili ndani ya baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa (UN) huundwa na mataifa matano (Marekani, Urusi, China, Uingereza, Ufaransa) yenye nguvu na kupiga kura turufu ya VETO.

Sasa jenga picha Tanzania (Tanganyika) iliyopata uhuru mwaka 1961 ikiwa bado na changamoto lukuki katika utoaji wa huduma muhimu za kijamii kama vile elimu, maji na afya, leo unaambiwa kuwa ni nchi ya tatu kwa upelelezi duniani baada ya Marekani na Urusi.

What a great nation was this? Inawezekana kauli hii ilikuwa na mapungufu kadha wa kadha (sijasema kuwa haikuwa sahihi) kutokana na kwamba internet access ya wakati ule haikuwa kama ya sasa ili watu kuweza kudhibitisha hilo, lakini ni kauli iliyowafanya watoto wajisikie wapo katika mikono salama. Ni kauli yenye mapungufu mengi iliyotufanya tujivunie kuwa watanzania.

A WELL-MANNERED SOCIETY MAKES THE FIRST LINE OF DEFENCE.

Ndugu zangu mimi sio mtumishi wa chombo chochote cha ulinzi na usalama hapa Tanzania, lakini kuwa mambo machache sana huwa ninayafahamu kuhusiana na kazi hizo kwa sababu mimi ni msomaji mzuri sana wa vitabu.

Kama kuna mada ambayo wadau wengi, hususan wale wafuasi wa vyama vya upinzani, walinitukana na kunikejeli, basi ni ile ya mwaka 2007 humu JF ambayo niliwaambia BASATA waufungie wimbo wa bongo bahati mbaya (BBM) ulioimbwa na msanii Young Dee.

Nilitukanwa sana katika uzi ule mpaka nikaamua kukaa nje ya JF kwa muda wa wiki mbili kwa lengo la kupunguza kiwango cha "panic" nilichokuwa nacho by then.

Ndugu zangu, vita huanzia akilini (Psychological Warfare) kabla ya uvamizi unaoonekana kwa macho (overt operations) wa ndege, vifaru pamoja na askari waliovaa sare (Camo). Hakuna vita yoyote magaidi au nchi ya kigeni (mfano Marekani) inaweza kushinda pasipo kukubaliwa na raia wa nchi inayovamiwa (Mfano Iran). Hivi unakumbuka kifo cha Major General (MG) Kassim Suleiman wa Iran?

Unakumbuka wananchi wa Iran walifanya nini? Kama haukumbuki ngoja nikukumbushe. Baada ya MG kuuwawa, wananchi wa Iran walipandisha bendera nyekundu juu kuashiria kwamba wapo tayari kupambana na Marekani, na kama USA wangethubutu tu kuingia Iran baada ya kambi yao kule Iraq kuvurumishiwa makombora basi ule ndio ungekuwa mwisho wa ubabe wa Marekani Middle East.

Ogopa sana nduvu ya umma mzee baba. Umma ukikuamulia jambo hata uwe na pesa kiasi gani, lazima uombe poo, yaaani ni lazima uake, ndio maana kabla nchi haijavamiwa ni lazima raia wa nchi husika waaminishwe kuwa uongozi uliopo madarakani ni ovu na wa kishetani (hii inaitwa Demonization).

Americans had to demonize Saddam, a man they helped to mould, as he gased his own people, so they could make a case for invading Iraq.

Sasa unajua demonization pamoja na psychological warfare inapiganwa vp mkuu, ni kupitia nyimbo za kuaminisha watoto mentality za kijinga kama hizo kuwa wapo Tanzania (Bongo) kwa bahati mbaya, something which is totally unacceptable..........

SWALI: Miaka 20 baada ya tukio la kigaidi la September 11, je tuna mifumo dhabiti ya kuzuia uhalifu wa ndani kabla ya kuleta misiba kwa taifa?

Nitaendelea...........

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Nimechomekea kidogo tu wakuu;
Wakili Mwanadamizi Slyvester Mwakitalu ni moja ya Mawakili waliokuwa chini ya DDP aliyepita na ambao walisimama kidete kutete Jamhuri kuhusu watuhumiwa kunyimwa dhamana.
Beatrice Kamugisha, mambo mengine ni ya mslahi ya Taifa zaidi mkuu. Huko Marekani magaidi waliokubali kuwa recruited na kutumika kama double agents wa Al Qaeda walifutiwa mshikata na ofisi ya DPP wa Marekani na kuachiwa kwa kazi maalum kwenda nchi kama Jordan na Lebanon kupeleleza viongozi waandamizi wa makundi mengine ya kigaidi.

Ofisi kama hizo za D.P.P na ile ya mwanasheria mkuu wa serikali - AG (Attorney General) zinafanya kazi kwa ukaribu mkubwa sana na vyombo vya ulinzi na usalama kama vile Police hivyo msiwalaumu wanapotimiza wajibu wao unaoweza kuwakera nyie ila ni kwa maslahi ya taifa.

Kwa nchi kama Marekani, kuna wakati kunyima watu dhamana (Coercion) ni muhimu ili mtuhumiwa aweze kutoa ushirikiano kwa dola.
 
Sikusoma habari ndefu, ila najibu kichwa cha habari.
Kwa nini unaliita "Home grown"?
Kabla ya kutokea kwa tukio lile la kugongesha ndege katika ghorofa pacha, wahalifu wale tayari walikuwa na watu wao ndani ya Marekani waliowasaidia kuwapa taarifa (watoto wa mjini wanasema kuchora rada) kabla ya kupanga mpango mzima wa kuteka ndege na kuleta msiba mzito ndani ya ardhi ya rafiki zetu wa Marekani.
 
Kabla ya kutokea kwa tukio lile la kugongesha ndege katika ghorofa pacha, wahalifu wale tayari walikuwa na watu wao ndani ya Marekani waliowasaidia kuwapa taarifa (watoto wa mjini wanasema kuchora rada) kabla ya kupanga mpango mzima wa kuteka ndege na kuleta msiba mzito ndani ya ardhi ya rafiki zetu wa Marekani.
Lakini kuwepo washiriki toka ndani inatosha kusema tukio lilikuwa "home grown"?
 
Wazazi katika familia na viongozi wa dini huko makanisani na misikitini wakitimiza wajibu wao ipasavyo, wanaipunguzia polisi/dola mzigo mkubwa sana wa kupambana na magaidi/wahalifu.
Siyo siku hizi mkuu.

Utawalaumu sana wazazi bure. Influence ya nje ya nyumbani ni kubwa mno kiasi kwamba huwezi kuwafungia wanano isiwaguse.

BTW, sijasahau ile 'definition' uliyoniomba, lakini siko kwenye mood wa kujibu hilo sasa hivi.
 
Habari zenu waungwana wa jamiiforums.

Nini kimekufanya kufikia mawazo hayo ktk uzi huu.

Uzuri vyombo vya usalama husoma tetesi kama hii na kuanza kuingia mitaani, ktk jamii na vijijini kujaribu kufahamu hii hofu yako uliyo iwakilisha hapa JF. Watakusanya taarifa inayoshabiana na hofu yako zilizopo ktk jamii, kuichakata, kuipima kama kuna viashiria au la na kama kunahaja ya kuchukua hatua stahiki watafanya hivyo .

Mfano jinsi vyombo vya ulinzi na usalama vinavyochukua uzito wa habari mitandaoni:

17 May 2021

IGP SIRRO - “NILIKUWA NAFUATILIA MITANDAONI, UNA FULL SUPPORT”



“Nilikuwa naangalia kwenye mitandao unajua siku hizi lazima uangalie kwenye mitandao Watu wanasema nini (ikiwemo) teuzi zikifanyika, nimeangalia kwenye mitandao una full support ya Watanzania naamini utawatendea haki Watanzania”—IGP Sirro baada ya kumvisha cheo cha Ukamishna CP Hamduni
 
Tuangalie kwa umakini movement kueleka upande wa kusini mwetu hasa Msumbiji, kuna vijana hawana hili wala lile wanaweza kupotoshwa na baadaye kuleta hayo matatizo ya domestic terrorism
 
Mkuu, kwa hiyo kwa muktadha huu 9/11 sio domestic terrorism? Vp kuhusu lile sakata la MKIRU?
Kwa definition, kama terrorist na victim ni wa uraia mmoja ndani ya hiyo nchi, ndio inakuwa domestic terrorism. Kwa MKIRU victims walikuwa Watanzania na kwa taarifa magaidi walikuwa Watanzania, ni domestic terrorisms.
 
Siyo siku hizi mkuu.

Utawalaumu sana wazazi bure. Influence ya nje ya nyumbani ni kubwa mno kiasi kwamba huwezi kuwafungia wanano isiwaguse.
Suala sio kuweka overprotection kwa watoto thidi ya ushawishi wa nje, lakini je unashughulika nao vp? Mtoto ananyooshwa katika taasisi kuu tatu;

(1) Familia yao
(2) Taasisi za dini
(3) Shuleni

Mtoto akiponyoka kutoka katika nguzo hizo tatu, huyo atakuwa gaidi/jambazi sasa.
 
Back
Top Bottom