Wadau, kwa hali ya upatikanaji wa huduma ya umeme ilivyo hapa Jijini Arusha, ni wazi kuwa Tanzania kwa sasa tumo kwenye tatizo kubwa la umeme. Tangu wiki hii ianze, kila siku umeme unakatika, majuzi eneo la Njiro umeme ulikatwa hadi usiku kabisa. Juzi umeme ulikatwa katikati ya mji kwa siku nzima, jana eneo la Themi halikuwa na umeme siku nzima, leo huku Njiro wamekata asubuhi na hadi sasa hawajarudisha na kwa siku zote hizo hawakutoa taarifa yoyote!
Kwa miezi ya Juni hadi Novemba nimekuwa huko Kilombero mjini Ifakara. Kwa muda huo wote umeme ulikuwa ukikatwa siku za Jumanne na Alhamisi, na wakazi wote wa Ifakara wanajua juu ya 'mgao huo' ambao haukuwahi kutangazwa!
Hivi kwa nini Wizara, Tanesco na Serikali zimekaa kimya bila kutoa taarifa rasmi ili tujipange namna ya kuishi bila umeme? Tutendeeni haki jamani.