Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,377
- 217,438
Ukiachilia mbali kwamba Mbowe ni Mwenyekiti wa CHADEMA , Chama cha siasa kilichoshambuliwa zaidi barani Africa kikifuatiwa na ANC ya Africa Kusini enzi za makaburu , Lakini pia duru za kisiasa za dunia zinamtaja Mbowe kama Mwenyekiti bora wa chama cha siasa kuwahi kuwepo barani Africa tangu kuumbwa kwa Mbingu na Ardhi.
Idadi ya vijana aliowafundisha siasa hakuna ukurasa wa hapa JF unaweza kutosha kuwaandika , wapo waliompongeza na kumheshimu , lakini wapo waliomtukana na kumdhalilisha bila kujali alikowaokota na kuwapa heshima mbele ya jamii , hata hivyo hajawahi kulipa kisasi , Mtu huyu si wa kawaida .