Sasa ni dhahiri kwamba CHADEMA Digital yaanza kusambaratisha upande wa pili

Sijawahi kusikia kama kuna wakati wowote, Masiha Yesu Kristo au Mtume Mohamad, alikodi ukumbi ili kuwahubiria watu neno la Mungu.

Walitumia nyika, barabara, pembezoni mwa nyumba za ibada, na mara chache ndani ya nyumba za ibada. Lakini mpaka leo, ujumbe wao unaendelea kusambaa na kuishi.

CHADEMA, endeleeni kupiga kazi, iwe nyikani, barabarani, vichochoroni au kumbini, cha muhimu ni jukumu kuu linafanyika.
 
Amina
 
Ni kweli kaka, watu wameamua kusonga kidigitali - simu yako kadi yako
 
Imefahamika sasa kwamba kazi ya Kitume inayofanywa na Chadema ya kusajili wanachama wake kwa njia ya kisasa iitwayo Chadema Digital ni kama MHURI WA MOTO, ni alama isiyofutika, iko kama chanjo ya NDUI, kila anayejisajili anahisi kama sasa ndio kapewa Uraia wa Tanzania.

Njama zote za kishamba za kuzuia wenye kumbi za mikutano kuwapa kumbi hizo Chadema zimegonga mwamba, na zimeshindwa kuzuia mafuriko ya wananchi kujitokeza kusajiliwa, tunazo taarifa za wenye kumbi kupewa vitisho ambapo wameelezwa kwamba atakayeruhusu Chadema Digital kwenye ukumbi wake atapewa kesi ya Uhujumu Uchumi ama utakatishaji pesa.

Wilaya ya Kyela ni miongoni mwa maeneo kulikotolewa onyo hili, ambako CHADEMA DIGITAL ilifanyika kwenye Ukumbi wa MUNGU, chini ya miti na kufanikiwa kwa kishindo. Nachukua nafasi hii kuwapongeza Wenye kumbi za mikutano waliopuuza Vitisho na kukubali Chadema digital kwenye kumbi zao, wala hawana haja ya kuogopa, kwa vile hakuna mahali popote kwenye dunia tuliyomo ambako SHETANI aliwahi kumshinda Mungu.

Maeneo mengine walikozuiliwa waliamua kufanyia usajili kwenye Kolido na kwenye vichochoro vya wazi, lakini zoezi hili halijawahi kukwama na halitasimama, Gari lishawaka, Pisha njia.

View attachment 2021336
Mungu ibariki CHADEMA
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom