JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,112
- 3,536
Amani na iwe kwenu wanabodi!
Kwa muda mrefu nimekuwa nasoma maandiko mbalimbali ya mwandishi mkongwe na mchambuzi wa mambo ya siasa duniani ndugu Jenerali Ulimwengu, nafikiri sasa ndio nimemwelewa alikuwa ana maanisha nini akisema Nchi imekumbwa na ombwe la uongozi.Mgogoro wa Zanzibar polepole unatuonesha ukweli huo.uchaguzi juu ya uchaguzi sababu ya msingi haijulikani.
Huwezi kuamini kuwa Nchi hii ina hazina kubwa ya viongozi walio pata kusifika duniani lakini wote wapo kimya kana kwamba Nchi haina tatizo lolote la kisiasa.Yuko wapi Salim Ahmed Salim?,yuko wapi Rais mstaafu ALLI Hssan Mwinyi? yuko wapi John Samwel Malecela? yuko wapi balozi AMMI MPUNGWE? Hivi hawoni kuwa Zanzibar inaingizwa kwenye mgogoro mkubwa wa kisiasa? Jitokezeni na msaidie kuikwamua Zanzibar kwenye mgogoro huu wa kisiasa ambao muda siyo mrefu utasababisha matatizo makubwa ya kiuchumi na kijamii
Mimi huwa najiuliza hivi viongozi wetu hawa hawakujifunza mbinu za kutatua migogoro kutoka kwa mwalimu JK Nyerere?Huwa hawasikilizi hata baadhi ya hotuba zake alizo zungumzia Nchi ya Znzibar na mambo yanayo weza kuikumba kwenye mfumo wa vyama vingi? Nchi ina marais wasitaafu chungu nzima lakini mgogoro wa Zanzibar unawashinda kuutatua! sasa tunawalipa kwa kazi gani kama jambo dogo linawashinda?
Binafsi nina uhakika kama Mwalimu JK Nyerere angekuwepo hii sintofahamu angeimaliza ndani ya muda mfupi sana tena kwa solution ambayo ingewaacha wanasiasa wote hoi bila kuwa na hoja ya ziada.Mfano mgogoro wa g55 walio taka Tanganyika irudi, alimaliza mgogoro ule kwa kutumia nyenzo chache sana.sasa leo Taifa linajidhalilisha duniani utadhani hatuna akina Nyerere wengine! mtajisikiaje siku moja mkiona viongozi kutoka nje wanakuja kutupatanisha?