Sasa ni dhahiri kuwa CHADEMA si Mbowe, Dr. Slaa, Lissu wala Lema. CHADEMA ni imani na haitakufa kirahisi!

Chadema inafanywa kama ilivyofanywa CUF na hautokuja amini hizo iman kama zitaendelea kuwepo.
Chadema imeshapita hatua hizo. Mateso waliyopitia CUF haifiki hata asikimia tano ya mateso wanayopitia Chadema sasa hivi lakini ndiyo kwanza Chadema inazidi kujiimarisha mioyoni mwa Watanzania. Magufuli alipiga marufuku mikutano ya vyama vya upinzani akilenga kuimaliza Chadema na akaamini kuwa ameimaliza lakini kazi tuliyopiga kwenye operation Chadema Msingi hakuamini alipopewa taarifa na UWT kuwa tuliweza kusimamisha 95%ya wagombea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa ndipo akaamua kuuvuruga uchaguzi huo. Na sasa Chadema Digital ndiyo inazidi kuonyesha kuwa Chadema inazidi kupaa licha ya kuporwa wabunge wote kwa mtutu wa bunduki kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Huyu anahusika na hizi sandarusi
JamiiForums-827127231.jpg

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
kweli, There's a light at the end of the tunnel...

inafurahisha kuona bado kuna wanaCCM wanaamini kwenye siasa za ushindani wa huru na haki, ukiondoa hili wimbi la miaka hii la machawa wanaojua kusifu na kuabudu CCM haiwezi kusimama kwa hoja bila kutumia dola
Sio wote ni wahuni kama ambavyo polepole anataka kuaminisha watu.
 
Hata uchaguzi uliopita mimi bado sikuafiki sana cdm kushiriki na msimamo wangu ule uliufahamu. Nadhani hata nyie mliokuwa na mashaka na mtazamo wangu, mmejiridhisha pasi na shaka kuwa kwa muundo huu wa uchaguzi na tume hii ni kupoteza muda. Kwa tulipofikia sasa bila mabadiliko ya tume ya uchaguzi, na katiba mpya, machafuko pekee ndio njia ya uhakika ya mabadiliko.
Mkuu, 'Tindo', msimamo wako naujua saana, na sikuwahi na hata sasa sikubaliani nao. Tunaweza kurudi nyuma na kuangalia tuliposimamia toka huko nyuma na kujiridhisha juu ya hili.
 
Kwa wasionifahamu (angalau kwa ufahamu wa humu JamiiForums), mimi ni kada kindakindaki wa CCM. Nimejiunga na chama hiki miaka ya mwanzoni mwa 80 baada tu ya kuhitimu shahada yangu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Nilisomea sheria. Nikafanya kazi chamani, serikalini na hata kwenye vyombo vya ulinzi na usalama. Naijua nchi hii vyema, hasa kisiasa, ilipotoka-ilipo-na inapokwenda.

Katika utumishi wangu chamani, nimeshiriki kupanga na kutekeleza mipango mingi ya kisiasa. Mipango ya ushindi yenye na isiyo na ushindani. Mipango ya sirini iliyokwenda kutekelezwa sirini na hadharani. Mipango iliyoibakisha CCM madarakani kuanzia uchaguzi wa mwaka 1995 hata sasa. Kuanzia kurejeshwa kwa vyama vingi mwaka 1995, CCM imekuwa ikilenga vyama au chama pinzani chenye nguvu na ku-deal nacho.

Kwa mwaka 1995, NCCR-Mageuzi ililengwa na kusambaratishwa. Mwaka 2000 na 2005 ilikuwa zamu ya CUF. Kuanzia mwaka 2010 hadi sasa, CHADEMA imekuwa target ya CCM kisiasa. Imekuwa mpinzani wa karibu na wa kuharibu wa CCM uchaguzini, uraiani na hata maishani. Wapo makada waliokuwa wakiamini kuwa ili kuisambaratisha CHADEMA, ni lazima kuwasambaratisha viongozi wake. Kuwafanya wasiwe wamoja na hata kucheza na mmojammoja.

Hakika, CCM tulifanikiwa kwa Dr. Slaa na viongozi/wanachama waandamizi wa CHADEMA wengineo. Walinyoosha mikono na kujiunga nasi. Wakabaki akina Mbowe, Lissu, Lema na wengineo. Kazi ikaendelea. Iliendelea katika imani ya kuwa wakidhibitiwa na kumalizwa nguvu zao za kisiasa (zikiwemo na za kiuchumi) CHADEMA itasawajika na kusambaratika kwelikweli. Ilikuwa IMANI POTOFU.

Kama mkongwe wa kisiasa na kiserikali, nimejiridhissha kuwa CHADEMA si viongozi. Ni IMANI inayoishi ndani ya wanachama, wapenzi na mashabiki wao. CHADEMA imejitengeneza katika falsafa ya kiuanaharakati. falsafa ya kupambania usawa, haki, mshikamano, amani na utulivu. Imani hukaa moyoni na rohoni mwa watu. Ni ngumu kuichomoa huko. Wale makada wa CCM waliokuwa wakiamini katika kushughulika na viongozi ili kuidhibiti CHADEMA, sasa wamejiunga nami niliyekuwa nikipingana nao tangu mwanzo.

Sasa wamekuwa wafuasi wa msimamo wangu kuwa siasa ni kushindanisha na kuonesha sera na utekelezaji wake. Katika kuonesha mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya CCM, hakuna haja ya kutumika kwa Polisi au chombo chochote cha ulinzi kufanikisha hilo. Kitu halisi huonekana kiurahisi sana. Aliyekuwa Mwenyekiti wetu Mzee Jakaya Kikwete aliwahi kutuusia kuwa tusitegemee polisi hata katika kubishana kwa hoja.

Lakini, bado wapo makada wengi ambao bado wanaamini kuwa CHADEMA ni Mbowe, Lissu na viongozi wengine. Bado wanaamini kuwa 'muunganiko wa tangu enzi' wa CCM na vyombo vya usalama ni nguzo na nyenzo ya ushindi wa chama. Bado wanaamini katika siasa kale za kutumia ulaghai, wizi wa kura, mabavu na vitisho kubaki madarakani-eti tubaki kuwa chamadola. Wanajidanganya.

Utafika wakati, vyombo vya ulizi na usalama vitatamani kusikia kwanza sera bila hela na kushawishiwa na ahadi bila zawadi. Vitatamani kuona ushindani wa nje na ndani ya uwanja wa kisiasa kabla ya kuelendelea kulinda maslahi ya nchi badala ya chama. Vitatuacha solemba tukilia na kusaga meno. Tuoneshe maendeleo na maendeleo yaseme tukiwa tuko kimya. Na, imani ya wananchi kwa upinzani itapungua kwa kasi.

Wasiojulikana sasa wamejulikana?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)
Mzee Tupa Tupa uko wapi mazee au bado upon moro
 
Huo ndio ukweli
 
Huna lolote kawadanganye watoto wenzio. Huna hiyo experience CHADEMA unauyoizungumzia haipo tena. We mwenyewe ni CHADEMA uliyekata tamaa
 
Back
Top Bottom