Sasa ni dhahiri kesi ya Mbowe imekaa vibaya. Mashahidi 24 na vielelezo 19 vya serikali si mchezo. Ni mkao wa kunyolewa

Ku

Kuna mtu alishangilia kifo cha magufuli akachinja na mbuzi wakala na wapambe wake
Nasikia nae kafa usiku wa kuamkia leo,
Sasa najiuliza mbona hata muda haujaenda kwa nini afe sasa wakati alihisi ana mkataba na mungu?
Na ni wale wanazi wa chadema.
Eboo!! Mkuu unasema kweli?
 
Aisee..ninadhani ni ukosefu wa maadili ndio inatuathiri watz. mtu unaanzaje kufanya sherehe kushangilia kifo cha mwenzako ? Mungu amsamehe madhambi yake na awafariji familia yake kwa msiba huu.
Tuanzie na sababu ya mtu kufurahia wewe ukifa, wakati akifa mwingine watu wanalia sana?? Hivi kwa nini kwenye dini tunaambiwa kuna watakaoenda peponi na kuna watakaoenda motoni??
 
Kwa mashtaka yaliyosomwa leo tarehe 23 Agosti 2021 ni wazi serikali imejipanga ipasavyo kwa kesi hii ya Mbowe ya ugaidi.

Serikali kuwa mashahidi 24 na vielelezo 19 siyo mchezo. Sasa tunafahamu kwa nini IGP alilizungumzia hii kesi kwa kujiamini sana na kueleza kuwa Mbowe kama ni mkristo mkweli atawaeleza ukweli wafuasi wake. Yote kwa yote, mahakama ndicho chombo cha juu cha kutoa hukumu.

Kupitia hukumu hiyo tutajua ukweli wa jambo hili. Kwa hatua iliyofikia kesi hii, ni vyema sasa tuiache mahakama ifanye kazi yake. Mabango na kauli za kisiasa kutoka Chadema sasa siyo mahali pake. Bahati nzuri katiba za vyama vyote vya siasa vinasisitiza juu ya kutambua utawala wa kisheria ambapo masuala ya mahakamani yanaachwa kwa mahakama kuamua na siyo kuyaleta kwenye majukwaa ya kisiasa.

Tutaishangaza dunia ikiwa bado chama fulani kitaendelea na kuweka mashinikizo nje ya mahakama. Pamoja na kwamba shinikizo zenyewe hazina hata nguvu ya kufungua soda na haziwezi kubadili lolote kuhusu mwenendo wa hii kesi, bado ni bora tukaachana na kuonesha shinikizo hizo ambazo kwangu naziona ni za kitoto na zinazidi tu kuwadhalilisha wanaoziweka.

Court decisions are based on what the law says and what the evidence proves. There is no place in the courts for suspicion, bias or favouritism. Tuachane na hizo empty rhetoric
Wingi wa MASHAHIDI Wingi wa Vielelezo Sio Ukubwa au Ugumu wa Kesi Kama Hujui Sheria kaa kando

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Kwa mashtaka yaliyosomwa leo tarehe 23 Agosti 2021 ni wazi serikali imejipanga ipasavyo kwa kesi hii ya Mbowe ya ugaidi.

Serikali kuwa mashahidi 24 na vielelezo 19 siyo mchezo. Sasa tunafahamu kwa nini IGP alilizungumzia hii kesi kwa kujiamini sana na kueleza kuwa Mbowe kama ni mkristo mkweli atawaeleza ukweli wafuasi wake. Yote kwa yote, mahakama ndicho chombo cha juu cha kutoa hukumu.

Kupitia hukumu hiyo tutajua ukweli wa jambo hili. Kwa hatua iliyofikia kesi hii, ni vyema sasa tuiache mahakama ifanye kazi yake. Mabango na kauli za kisiasa kutoka Chadema sasa siyo mahali pake. Bahati nzuri katiba za vyama vyote vya siasa vinasisitiza juu ya kutambua utawala wa kisheria ambapo masuala ya mahakamani yanaachwa kwa mahakama kuamua na siyo kuyaleta kwenye majukwaa ya kisiasa.

Tutaishangaza dunia ikiwa bado chama fulani kitaendelea na kuweka mashinikizo nje ya mahakama. Pamoja na kwamba shinikizo zenyewe hazina hata nguvu ya kufungua soda na haziwezi kubadili lolote kuhusu mwenendo wa hii kesi, bado ni bora tukaachana na kuonesha shinikizo hizo ambazo kwangu naziona ni za kitoto na zinazidi tu kuwadhalilisha wanaoziweka.

Court decisions are based on what the law says and what the evidence proves. There is no place in the courts for suspicion, bias or favouritism. Tuachane na hizo empty rhetoric
Kuwa na mashahidi 23 na vielelezo 19 siyo sawa na kusema kesi imeelemea upande wa fulani. Kuna baadhi ya kesi Jamhuri inaweza kuwa na mashahidi na mshtakiwa kutokuwa na shahidi yeyote na still ushindi ukawa upande wa mshtakiwa. Kinachotakiwa kwenye kesi ni the weight of evidence and persuasion.
 
Huo utitiri wa mashaidi ndio utakaoivuruga hiii kesi
Kuna uwezekano wa baadhi ya mashahidi kusahau script verse zao na Mh.Mbowe akanusurika dhisi ya watesi wake.
Huo wingi wa mashahidi pia ni mbinu ya kurefusha muda wa kuendesha mashauri yenyewe.Delaying Tactics kwa Hoja za Katiba yetu ya Wananchi.Mbinu za kizamani!
 
Kuna kila dalili ni kupotezeana muda ili kuwatoa watu kwenye hoja ya katiba mpya kwa either kumfunga au kumwachiwa wakati wameshajiandaa na lifuatalo. Hili halitaenda kwa funika KOMBE MWAHARAMU APITE LA HASHA utashi, uelewa na dhamira ya kuokoa nchi kutoka kwenye aibu hii tunayoishuhudia sasa hivi. Utamfunga Mbowe ila halitaishia hapo suluhisho la kisiasa linamalizwa kisiasa, watanyanyuka wengine watakuja na hoja hiyo hiyo la katiba mpya msikilizeni wazee wetu Msekwa/Warioba hawa ni CCM. Hili ni hitaji la hata CCM wenyewe utaniambia siku za usoni.
 
Kwa mashtaka yaliyosomwa leo tarehe 23 Agosti 2021 ni wazi serikali imejipanga ipasavyo kwa kesi hii ya Mbowe ya ugaidi.

Serikali kuwa mashahidi 24 na vielelezo 19 siyo mchezo. Sasa tunafahamu kwa nini IGP alilizungumzia hii kesi kwa kujiamini sana na kueleza kuwa Mbowe kama ni mkristo mkweli atawaeleza ukweli wafuasi wake. Yote kwa yote, mahakama ndicho chombo cha juu cha kutoa hukumu.

Kupitia hukumu hiyo tutajua ukweli wa jambo hili. Kwa hatua iliyofikia kesi hii, ni vyema sasa tuiache mahakama ifanye kazi yake. Mabango na kauli za kisiasa kutoka Chadema sasa siyo mahali pake. Bahati nzuri katiba za vyama vyote vya siasa vinasisitiza juu ya kutambua utawala wa kisheria ambapo masuala ya mahakamani yanaachwa kwa mahakama kuamua na siyo kuyaleta kwenye majukwaa ya kisiasa.

Tutaishangaza dunia ikiwa bado chama fulani kitaendelea na kuweka mashinikizo nje ya mahakama. Pamoja na kwamba shinikizo zenyewe hazina hata nguvu ya kufungua soda na haziwezi kubadili lolote kuhusu mwenendo wa hii kesi, bado ni bora tukaachana na kuonesha shinikizo hizo ambazo kwangu naziona ni za kitoto na zinazidi tu kuwadhalilisha wanaoziweka.

Court decisions are based on what the law says and what the evidence proves. There is no place in the courts for suspicion, bias or favouritism. Tuachane na hizo empty rhetoric
Itabidi mtumie mabavu ili kulazimisha hukumu muitakayo. Ushahidi mliyo nao mpaka sasa ni porojo kama za watoto.
 
Back
Top Bottom