Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,600
- 218,003
Wakuu natanguliza salamu , na baada ya salamu najikita moja kwa moja kwenye mada .
Nilikuwa kimya kwenye Kauli za uchochezi zilizoambata na viashiria vya kupanga utekaji na mauaji kutoka kwa anayejiita mwanaharakati wa Magufuli aitwaye Musiba , bado haijafahamika kama uanaharakati wa Musiba anaodai kuwa nao ni kwa Magufuli binafsi au ni uanaharakati kwa Magufuli ambaye ni Rais wa Tanzania.
Bali kinachofahamika ni kwamba kwa kauli zile bila kujali anayemharakatia alipaswa kukamatwa na kuhojiwa kwa tuhuma za uchochezi pamoja na kupanga mauaji , ni aibu kubwa sana kwa kiongozi wa nchi kuwa na mpambe wa aina ya Musiba na pia ni aibu kubwa sana kwa nchi ya Tanzania kumnyamazia mtu wa aina hii hata angekuwa " mtoto wa nje ya ndoa " wa Rais , pamoja na ukweli wote kwamba Sheria za mitandao inapinga mtu yeyote kusambaza uchochezi wa namna hii , lakini si TCRA wala jeshi la polisi waliothubutu kukemea jambo hili , hawa wote WAMEUFYATA , tena wameufyata kweli kweli.
Huu ni uthibitisho kwamba wote hawa wanamuogopa na kumtii Musiba , swali la kujiuliza ni hili , kwanini mamlaka za Tanzania zinamtii na kumuogopa raia huyu asiye na dhamana yoyote hata kwenye eneo la nyumba 10 ?