Sasa ni dhahiri Dr. Kikwete (heshima-UDOM) naye anatamani miaka mitano iishe haraka!

WanaJF,

Hivi karibuni nilijumuika kwenye ziara ya Rais aliyechaguliwa na NEC, Dr. Kikwete (heshima-UDOM) ya kutembelea eneo la Gongolamboto lililoathiriwa na mabomu. Juzi nilijumuika pia kwenye hafla ya kumpokea uwanja wa ndege Rais aliyechaguliwa na NEC, Dr. Kikwete (heshima-UDOM) wakati akiwasili kutoka katika ziara yake aliyokwenda kusuluhisha mgogoro wa nchi nyingine ya kiafrika.

Kwa wanaomfahamu Kikwete wa zamani (enzi zile akiwa hana udaktari wa heshima) hawatachelewa kubaini mabadiliko makubwa kwenye sura yake. Ukweli sasa amechoka, amechoka, jamani nasema amechoka, siyo utani amechoka, yupo hoi. Hata wananchi wanaompokea au kusalimiana nae kwenye hafla mbalimbali unaweza ukawasoma kwa kutumia 'body language' namna walivyokata tamaa na kukosa matumaini. Mimi naamini kabisa kwa jinsi hali ilivyo, hata Kikwete mwenyewe atakuwa amebaini mabadiliko hayo na lazima anatamani miaka mitano itimie haraka akapumzike. Wakati yeye anateseka hivyo, mafisadi anaowafuga mwenyewe wanakula maisha ya peponi!
Anajuuliza jinsi ya kutumia u Dr (heshima-UDOM) kukanusha tangazo la Sheikh Yahya kuhusu kumwongezea ulinzi usioonekana ili wananchi wasimuone mpunga mapepo na kujitenga naye (Kuogopa mapepo yasije yakawadakia )
 
Unajua urais kwa nchi maskini kama Tanzania siyo wa kuukimbila kwa sababu:-
  1. Nchi nyingi maskini hutegemea misaada na hivyo kuziweka rehani ahadi ulizotoa kipindi unagombea uchaguzi. Nadhani nalo hili linamtesa sana JK hajui aanzie wapi aishie wapi?
  2. Mikasa au mabalaa ambayo hakuitegemea na ile ya uzembe kama Gongo la Mboto.
  3. Kukosa support kubwa kutoka kwa marafiki wa karibu huunda ombe la upweke ukakosa wa kumuamini kwa kuogopa kusalitiwa. Marafiki wengi wa JK ni mafisadi ambao wanataka JK awalinde katika madeal yao, indirect wanamchonganisha na wananchi kwa kumuona ni rais asiye na maamuzi na mpenda mafisadi.
  4. CDM nayo imekuwa kaa la moto kwa serikali ya JK. Haelewi achukue hatua gani muafaka ili kuzima nguvu ya chama hiki ambacho taarifa zinaonyesha kinakuwa kwa kasi licha ya jitihada za kuhakikisha kinanukishwa kwa wananchi.
Hayo kwa kiasi fulani yanamuumiza kichwa kukichagizwa na kushuka kwa uchumi, mfumuko wa bei n.k
Dawa ya hayo hapo juu ni serikali inayowajibika na iliyolenga kukuza uchumi siyo kwa takwimu bali kwa uhalisia jambo ambalo kwa CCM linazidi kupotea kutokana na tamaa ya viongozi wake kupenda kujilimbikizia mali na kusahau walio wengi.
Mwisho ni kutopenda kujifunza jinsi wenzetu walio maskini wamepitaje hadi hapo walipo fika na kuamini ni miujiza ya Mungu ndiyo imewafanya waendelee, huu ni uvivu kwa kiasi fulani.

AHADI ZA KIKWETE KWA WAPIGA KURA KATIKA KAMPENI ZA URAIS 2010.
Je atazitekeleza?...Mimi na wewe ni Mashahidi, na kama zitatekelezwa tuweke tiki!
Lakini kinachotisha zaidi, ahadi hizi gharama yake ni jumla ya shs trilioni 90!...upo hapo?

1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora
1. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
2. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
3. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
4. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
5. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
6. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
7. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
8. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
9. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
10. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
11. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
12. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
13. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
14. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
15. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera
16. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
17. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza
18. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
19. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
20. Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba
21. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
22. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini
23. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
24. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
25. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
26. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
27. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
28. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
29. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
30. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
31. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
32. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
33. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
34. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
35. Kulinda haki za walemavu- Makete
36. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
37. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
38. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
39. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora
40. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
41. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
42. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
43. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
44. Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
45. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
46. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
47. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
48. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
49. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
50. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
51. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
52. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
53. kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
54. kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa
55. ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
56. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kabandamaiti mjini Zanzibar
57. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
58. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
59. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
60. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
61. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
62. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
63. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
64. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
65. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
66. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha

Mungu Ibariki Tanzania!
 
42. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
43. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
44. Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
45. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
46. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
47. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
48. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
49. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
50. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
51. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
52. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
53. kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
54. kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa
55. ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
56. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kabandamaiti mjini Zanzibar
57. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
58. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
59. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
60. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
61. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
62. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
63. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
64. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
65. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
66. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha

Mungu Ibariki Tanzania!

For real!!
 
WanaJF,

Hivi karibuni nilijumuika kwenye ziara ya Rais aliyechaguliwa na NEC, Dr. Kikwete (heshima-UDOM) ya kutembelea eneo la Gongolamboto lililoathiriwa na mabomu. Juzi nilijumuika pia kwenye hafla ya kumpokea uwanja wa ndege Rais aliyechaguliwa na NEC, Dr. Kikwete (heshima-UDOM) wakati akiwasili kutoka katika ziara yake aliyokwenda kusuluhisha mgogoro wa nchi nyingine ya kiafrika.

Kwa wanaomfahamu Kikwete wa zamani (enzi zile akiwa hana udaktari wa heshima) hawatachelewa kubaini mabadiliko makubwa kwenye sura yake. Ukweli sasa amechoka, amechoka, jamani nasema amechoka, siyo utani amechoka, yupo hoi. Hata wananchi wanaompokea au kusalimiana nae kwenye hafla mbalimbali unaweza ukawasoma kwa kutumia 'body language' namna walivyokata tamaa na kukosa matumaini. Mimi naamini kabisa kwa jinsi hali ilivyo, hata Kikwete mwenyewe atakuwa amebaini mabadiliko hayo na lazima anatamani miaka mitano itimie haraka akapumzike. Wakati yeye anateseka hivyo, mafisadi anaowafuga mwenyewe wanakula maisha ya peponi!

sio lazima hiyo miaka 5 iishe alivyochoka yeye basi ajue wale aliotuahidi kwa ahadi
zake nyingi ndio tuko hoi bin taabani,tutamsamehe hata kesho akijiuzulu tu.
aachie wengine wajaribu kubebea msalaba kuanzia hapo.
 
Isije ikawa tunajipa moyo tu hapa.
Nitaamini kwamba anapata shida kama tu, ataamua kuachia, kwani kuna mtu amemfungia pale?
Otherwise huu utaratibu wa kupeana moyo na stori za vijiweni, eti JK anakonda; Haujanikamata bado :hand:
MKUU, You ar very smart!! Hizi ni story za vijiweni tu kujifurahisha na kupeana moyo kwa wivu na chuki isiyo na maelezo. Ndguzanguni,, mtamaliza vituko, matusi na kashfa zooote, walakini, Tanzania ina Rais mmoja tu, mpendwa Jakaya Mrisho Kikwete. Hizo, Dr. Mh, Sir nk zisiwaumize sana hata wewe mtoa mada hii unaweza ukajiita Dr UKITAKA.
 
picha iliyopo kwa kila aliyeahidiwa baada ya kile ninachokiita kutupa kura yako kwa ccm wakati wa uchaguzi 2010,kwa rais na wapiga kura wake wa-tz hakina tofauti na wale wanaodaiana,mdaiwa unakuwa ktk hali mbaya unalutana na mdai wako unazeeka ghafla,maake ulikopa kwa kutumia misamiati na maneno mengi ili ufanikishe hitaji lako.
SASA NI WAKATI WA KULIPA LILE DENI ILA KWA CCM HATUSHANGAI UCHAWI WALIONAO KWA WA-ZT
huwa wana majibu kwao hata kama wao ndio wanadai utashangaa kwa SISIEM huwa wanageuka kuwa wadaiwa.
 
wanajf,

hivi karibuni nilijumuika kwenye ziara ya rais aliyechaguliwa na nec, dr. Kikwete (heshima-udom) ya kutembelea eneo la gongolamboto lililoathiriwa na mabomu. Juzi nilijumuika pia kwenye hafla ya kumpokea uwanja wa ndege rais aliyechaguliwa na nec, dr. Kikwete (heshima-udom) wakati akiwasili kutoka katika ziara yake aliyokwenda kusuluhisha mgogoro wa nchi nyingine ya kiafrika.

Kwa wanaomfahamu kikwete wa zamani (enzi zile akiwa hana udaktari wa heshima) hawatachelewa kubaini mabadiliko makubwa kwenye sura yake. Ukweli sasa amechoka, amechoka, jamani nasema amechoka, siyo utani amechoka, yupo hoi. Hata wananchi wanaompokea au kusalimiana nae kwenye hafla mbalimbali unaweza ukawasoma kwa kutumia 'body language' namna walivyokata tamaa na kukosa matumaini. Mimi naamini kabisa kwa jinsi hali ilivyo, hata kikwete mwenyewe atakuwa amebaini mabadiliko hayo na lazima anatamani miaka mitano itimie haraka akapumzike. Wakati yeye anateseka hivyo, mafisadi anaowafuga mwenyewe wanakula maisha ya peponi!

mwenye picha ya 2009 atuwekee na mwenye picha ya 2011 aweke pia tuone kama kuna ukweli
 
Na hivi tunavyomchokonoa, ndo anazidi kudorora. Mie simpendi kabisaaaaa!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom