Sasa ni dhahiri Dr. Kikwete (heshima-UDOM) naye anatamani miaka mitano iishe haraka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa ni dhahiri Dr. Kikwete (heshima-UDOM) naye anatamani miaka mitano iishe haraka!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Gosbertgoodluck, Feb 25, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  WanaJF,

  Hivi karibuni nilijumuika kwenye ziara ya Rais aliyechaguliwa na NEC, Dr. Kikwete (heshima-UDOM) ya kutembelea eneo la Gongolamboto lililoathiriwa na mabomu. Juzi nilijumuika pia kwenye hafla ya kumpokea uwanja wa ndege Rais aliyechaguliwa na NEC, Dr. Kikwete (heshima-UDOM) wakati akiwasili kutoka katika ziara yake aliyokwenda kusuluhisha mgogoro wa nchi nyingine ya kiafrika.

  Kwa wanaomfahamu Kikwete wa zamani (enzi zile akiwa hana udaktari wa heshima) hawatachelewa kubaini mabadiliko makubwa kwenye sura yake. Ukweli sasa amechoka, amechoka, jamani nasema amechoka, siyo utani amechoka, yupo hoi. Hata wananchi wanaompokea au kusalimiana nae kwenye hafla mbalimbali unaweza ukawasoma kwa kutumia 'body language' namna walivyokata tamaa na kukosa matumaini. Mimi naamini kabisa kwa jinsi hali ilivyo, hata Kikwete mwenyewe atakuwa amebaini mabadiliko hayo na lazima anatamani miaka mitano itimie haraka akapumzike. Wakati yeye anateseka hivyo, mafisadi anaowafuga mwenyewe wanakula maisha ya peponi!
   
 2. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Unajua urais kwa nchi maskini kama Tanzania siyo wa kuukimbila kwa sababu:-
  1. Nchi nyingi maskini hutegemea misaada na hivyo kuziweka rehani ahadi ulizotoa kipindi unagombea uchaguzi. Nadhani nalo hili linamtesa sana JK hajui aanzie wapi aishie wapi?
  2. Mikasa au mabalaa ambayo hakuitegemea na ile ya uzembe kama Gongo la Mboto.
  3. Kukosa support kubwa kutoka kwa marafiki wa karibu huunda ombe la upweke ukakosa wa kumuamini kwa kuogopa kusalitiwa. Marafiki wengi wa JK ni mafisadi ambao wanataka JK awalinde katika madeal yao, indirect wanamchonganisha na wananchi kwa kumuona ni rais asiye na maamuzi na mpenda mafisadi.
  4. CDM nayo imekuwa kaa la moto kwa serikali ya JK. Haelewi achukue hatua gani muafaka ili kuzima nguvu ya chama hiki ambacho taarifa zinaonyesha kinakuwa kwa kasi licha ya jitihada za kuhakikisha kinanukishwa kwa wananchi.
  Hayo kwa kiasi fulani yanamuumiza kichwa kukichagizwa na kushuka kwa uchumi, mfumuko wa bei n.k
  Dawa ya hayo hapo juu ni serikali inayowajibika na iliyolenga kukuza uchumi siyo kwa takwimu bali kwa uhalisia jambo ambalo kwa CCM linazidi kupotea kutokana na tamaa ya viongozi wake kupenda kujilimbikizia mali na kusahau walio wengi.
  Mwisho ni kutopenda kujifunza jinsi wenzetu walio maskini wamepitaje hadi hapo walipo fika na kuamini ni miujiza ya Mungu ndiyo imewafanya waendelee, huu ni uvivu kwa kiasi fulani.
   
 3. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Watoto wa mjini wanasema ndio akome ubishi. Misukule si anaifuga mwenyewe.
   
 4. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa. Akome ubishi. Alililia wembe sasa unaendelea kumkata.
   
 5. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Na afy ayake c unajua huwa ni spana mkononi? kazi kweli kweli!
   
 6. Plato

  Plato JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 421
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  Mnapata shida,phd za heshima huandikwa kwa kutanguliwa na H.c Dr. Kikwete.wanaojua wanajua hiyo ni ya heshima tu
   
 7. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Asante kwa kutujuza lakini kwa uelewa wa wengi bora kuandika kwa kirefu ili kuepuka lawama. Manake wapambe wake hawakawii kusema tunamwonea wivu PhD zake alizopata uarabuni na udom!
   
 8. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Nafikiri umesahau ule usemi unaosema:Dalali miaka kumi (10)jela mwizi anakunywa bia bar
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Feb 25, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,516
  Likes Received: 19,940
  Trophy Points: 280
  duh,hapa sikubaliani na wewe mkuu kwa sababu ile misukule haifugi ila ndio imemuweka pale
   
 10. il dire

  il dire Member

  #10
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  i think its time huyu bwana mkubwa mwenye dr (heshima-udom) achague moja kunyoa ama kusuka coz mafisadi kwa speed hii watampeleka kaburini kabla ya muda wake. na afya yake ilivyokua mgogoro. hii nchi haiwezi akae pembeni tu.
   
 11. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #11
  Feb 25, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Isije ikawa tunajipa moyo tu hapa.
  Nitaamini kwamba anapata shida kama tu, ataamua kuachia, kwani kuna mtu amemfungia pale?
  Otherwise huu utaratibu wa kupeana moyo na stori za vijiweni, eti JK anakonda; Haujanikamata bado :hand:
   
 12. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #12
  Feb 25, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Great thinker, it's time we should be vivid with what we say!
  Tuache majungu, tuseme kweli, tuwe tayari ku-justify pale itakapohitajika..
  Kwa mfano, unaweza kuitetea hii hoja yako?
  Au na wewe ni mmoja wao?
   
 13. Dyslexia

  Dyslexia Senior Member

  #13
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  akimfikiria Dr Slaa na Tundu Lissu,lazima azeeke! ningekuwa yeye ningejiuzulu tu nikalee maelfu ya watoto wangu!
   
 14. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #14
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kama kachoka ana ruhusiwa kujiuzulu aka pumzika....just a thought.
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,814
  Likes Received: 83,210
  Trophy Points: 280
  Miye nilijua kazi imemshinda siku nyingi tu tangu pale alipotudanganya kwamba mafisadi wa EPA wamerudisha shilingi bilioni 67 kati ya 133 bilioni walizokupua lakini akashindwa kutoa majina ya mafisadi waliorudisha pesa hizo na kutwambia zimewekwa katika bank ipi na pia kuiweka hadharani account #

   
 16. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #16
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Mtoa mada anasema 'kwa wale wanamfahamu vizuri Kikwete'. Wewe inaonekana humfahamu vizuri kikwete. Labda ni wa kijiweni kama unavyotaka mtoa mada awe hivyo. Kama hujui kikwete kuwa kikwete amechuja basi bora ukae kimya. Sisi tulio karibu nae ndiyo tunaweza kuthibitisha vizuri ukweli wa hoja hii. Mimi binafsi nilikuwa Dodoma wakati wa kilele cha sherehe za miaka 34 ya sisiem. Ni ukweli usiopingika kuwa rais sasa hana furaha. Anailazimiha tu. Lile tabasamu la bashasha tulilozoea limebaki la kinafiki tu. Kwa mtu mzima hahitaji kufanya utafiti kubaini hilo.

  Kwa ujumla nakubaliana na mtoa hoja kwamba wakati yeye anateseka hivyo, mafisadi wenzie wanaishi kwa furaha na amani. Uamuzi upo kwake ama kuendelea kufuga au anyoe.
   
 17. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #17
  Feb 26, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kingine kinachomkosesha raha ni zile ahadi alizomwaga wakati wa kampeni..
   
 18. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #18
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Shauri yake nani alimtuma azimwage! Akome na kukomaa!
   
 19. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #19
  Feb 26, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Duu, mzee unaonekana una hasira sana na jk.
   
 20. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #20
  Feb 26, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  heshima gani!!
   
Loading...