Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,780
- 10,710
Ndugu wanaJF, kufuatia sakata la LAAC na PAC, imedhihirika wazi kuwa CHADEMA kimejengwa kuzunguka watu maarufu. Ukikipima kwenye mizani ya taasisi kinaanguka vibaya sana.
Kitendo cha kuwakataa wabunge wake na wale wa UKAWA kuongoza kamati mpaka aongoze Mbowe ni cha kutia shaka. Hakizingatii weledi bali umaarufu wa kisiasa kuliko usomi. Mbaya zaidi ni pale lilipofanyika jaribio la kumpigia chapuo Kubenea kuongoza mojawapo ya kamati hizo, wakati ni kinda bungeni. Kigezo hapa pia ilikuwa ni umaarufu wake.
Kwa siasa za aina hii CHADEMA haina maisha marefu. Leo hii mwenye nguvu kuu ndani ya CHADEMA ni Lowassa ambaye wala si mjumbe japo wa mtaa. Ni aibu kubwa kwa taasisi iliyojengwa kwa muda mrefu kuongozwa pasipo kufuata misingi.